Pages

Subscribe:

Monday, 15 February 2016

UTAMU WA NENO LA MUNGU

BIBLIA NI NENO LA MUNGU LILILO HAI Katika Biblia Yako Soma Zaburi 119: 9-11,105; Waebrania 4:12; Marko 4:21-29. Mstari Wa Kukariri Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki; ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema (2Tim 3:16, 17). Baadaye Zungumzieni Jambo Hili Je, unaamini kuwa Neno la Mungu ndilo lenye mamlaka yote katika maisha? Jambo La Kufanya Kabla Hatujakutana Tena Jitahidi kutenga muda maalum kila siku kwa ajili ya kutulia na kutafakari. Tekeleza mpango wa kusoma Biblia. Andaa alama saba za kuweka katika Biblia yako pale unapoachia kusoma ili uweze kupapata kirahisi utakapoendelea kupasoma tena wiki inayofuata. Kazi Ya Kuandika Ya Stashahada Kutoka katika 2Fal 22:8-13 na 2Fal 23:1-32 andika mageuzi yote aliyoyafanya mfalme Yosia baada ya kulisikia neno la Mungu. Tafakari Andiko Hili Mathayo 7:24-27 Tumia Dakika Moja Kuubadilisha Ulimwengu Ombea taifa la Ujerumani. Idadi ya watu: 80,000,000. Idadi ya Wakristo ni 75% Ujerumani Mashariki maskini na Ujerumani Magharibi tajiri sasa zimeungana. Makanisa ya zamani yanapoteza watu. Uamsho unatakiwa haraka 1. Biblia Ni Neno La Mungu Kwa kila mwamini neno la Mungu ni la kipekee na la thamani kubwa. Kwa karne nyingi zilizopita watu wengi wametoa maisha yao katika kuhifadhi kweli ya neno la Mungu kwa ajili yetu ili tupate kusoma. Kwa kuzingatia thamani kubwa ya neno la Mungu, na andiko kutoka Mk 4:21, swali ni hili, ‘Biblia iko wapi katika maisha yako?’ Je, imefichwa mbali; Au imewekwa mahali pa juu ili ipate kumulika kila eneo la maisha yako? 2. Baraka Katika Neno La Mungu Neno lake li hai, linanena nawe na kutenda kazi ndani yako (Ebr 4:12,13). Neno lake ni kioo kinachokufanya ujione ulivyo kadiri unavyoendelea kulisoma. Neno lake kamwe halitakufanya ujidanganye mwenyewe, wala kuficha ukweli (Yak 1:22-24) (Mk 4:22). Neno lake litakuandaa kikamilifu ili uwe, na ufanye kile Mungu anachotaka (2 Tim 3:15-17). Kuanzia ulipokuwa mtoto hadi sasa umeyajua Maandiko Matakatifu yanayoweza kukupa hekima unayoihitaji kwa ajili ya kupata wokovu kwa imani katika Kristo Yesu. Maandiko yote yana pumzi ya Mungu na yanafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki, ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema. Inasemekana, na ndivyo ilivyo, kwamba Biblia ni Mwana wa Mungu katika maandishi, kwa sababu Yesu anaitwa ni Neno, na vilevile anaitwa Kweli (Yn 1:1). Je, Unataka Kufanikiwa Na Kustawi? Basi fanya yale Yoshua aliyoagizwa kufanya (Yos 1:8). Na kama unataka kustawi kwa kila kitu zingatia Zab 1:1-3. 3. Je, Unaposoma Unasikia? Je, umewahi kugundua kuwa unaposoma neno la Mungu ‘unasikia’ kwa ndani na si kwa masikio ya nje? Hiyo ni sauti ya Mungu. Yapasa tuwe makini na kile tunachosikia kwa sababu kwa kipimo kilekile tunachotumia, ndicho tutakachopimiwa (Mk 4:24). 4. Je, Unalitumiaje Neno La Mungu? Unalitumia hilo neno kufanya upya moyo wako (Rum 10:17). Unalitumia hilo neno kufanya upya mawazo yako Rum 12:2). Unalitumia hilo neno kufanya upya maneno yako (Rum 10:10) (Mit 18:2). Ulitumie hilo neno kufanya upya matendo yako (Yn 14:15). Ulitumie hilo neno kuimarisha ushindi wako. Shetani hakuwa na usemi Yesu aliposema, ‘Imeandikwa’! (Mt 4:1-11)-zingatia mistari ya 4,7 na 10. Litumie Neno Kuhuisha Maombi Yako Waamini wa kwanza mara kwa mara walinukuu maandiko ili yawaongoze katika maombi, na Mungu alijibu haraka (Mdo 4:23-31). Iwapo utaomba kwa kutumia neno la Mungu, yafuatayo yataanza kutokea: Kwanza, unapanda mbegu ya neno. Kisha kwa uvumilivu katika kuliomba neno, na saburi, huja masuke. Na kwa kadiri unavyoendelea kuwa na imani kwa Mungu na katika neno lake, huja ngano pevu, nafaka kukomaa na hatimaye mavuno. (Mk 4:14, 26-29) (Isa 55:10, 11) (Mwa 8:22). Ni Muhimu Kuwapa Wengine Neno La Mungu Ni muhimu kwa sababu ye yote mwenye neno la Mungu anaweza kuokolewa na kupewa zaidi, mathalani: uponyaji, uhuru, uongozi, baraka na ustawi, kwa kuliamini. Lakini mtu asiye na hilo neno la Mungu ili kuliamini na kulifanyia kazi, hana baraka yo yote katika hizo zilizotajwa, na atapoteza hata hicho alichonacho, yaani maisha yake na nafsi yake milele (Mk 4:25). 5. Unapataje Kulisikia Neno? Mungu amefanya iwe rahisi sana kuisikia sauti yake. Wewe kaa peke yako na Yeye, na kisha fungua Biblia yako. Kiri udhaifu wako na omba kujifunza kwa msaada wa Roho Mtakatifu. Chukua muda kutafakari yale uliyosoma na kusikia, kwa sababu kwa njia hiyo utashangaa kuona jinsi Mungu atakavyozungumza na wewe na kujibu maswali yako. Nikiwa mwamini mpya sikuyajua mambo haya. Nilihudhuria kwenye kusanyiko la maombi na kimyakimya niliomba kwa ajili ya kazi yangu, nikamwombea mke wangu na watoto kwa sababu ya matatizo yote tuliyokuwa nayo. Baada ya muda mfupi nilihisi msukumo wa kuichukua Biblia yangu na ikafunguka yenyewe katika Zaburi ya 128. Na nilipoanza kusoma Mungu alinistusha na baadaye akanipooza kwa neno lake akiuambia moyo wangu: “Wamebarikiwa wote wamchao Bwana na kutembea katika njia zake. Utakula matunda ya kazi yako, baraka na kustawi vitakuwa vyako. Mkeo atakuwa kama mzabibu uzaao, na wanao kama matawi ya mtende mezani pako”. Naliliamini neno la Mungu na leo hii, baada ya miaka kadhaa kupita naweza kuona jinsi Mungu alivyoitunza ahadi yake kwa kuibariki familia yangu na kazi yangu. 6. Namna Ya Kufurahia Usomaji Wa Biblia Watu wengi huanza na kitabu cha Mwanzo na baadaye huacha wanapokutana na sehemu ngumu katika Agano la Kale ambazo hawazielewi. Sisi sote tunapenda kula vyakula mbalimbali siku kwa siku, na hivyo ndivyo ilivyo hata kwa chakula cha kiroho. Jaribu kufuata mpangilio ufuatao nawe utapata mlo tofauti kila siku. Kila siku soma Zaburi za kuabudu na Mithali kwa ajili ya kupata hekima.

UMUHIMU WA KULIJUA NENO LA MUNGU. By Ev. Elimeleck Ndashikiwe

Upo umuhimu wa kujua neno la Mungu katika maisha ya Mkristo halisi. Biblia inatuambia Yesu Kristo ndiye Neno la Mungu. Kwa maneno mengine Yesu ndiye Neno ambalo Mkristo anapaswa kuwa nalo (Yohana 1:1). Kwa kusema hivyo kuna umuhimu wa kumjua Yesu na kumshika, kwa maana yeye ndiye Neno la Mungu. Katika Biblia mtume Petro anasema mbele za Yesu kwamba, twende kwa nani na wewe ndio mwenye maneno ya uzima? Petro alijua upo umuhimu wa kumjua Yesu kama Neno maana ndani ya Neno kuna uzima Biblia inasema neno la Kristo likae kwa wingi ndani yetu (Wakolosai 3:16). Kwa nini basi neno la Kristo likae kwa wingi ndani yetu? Ni kwa sababu lina mambo yafuatayo ambayo ni muhimu katika maisha yetu ya Ukristo. Mambo hayo ni… A) Neno la Mungu li Hai B) Neno la Mungu lina nguvu (Mwanzo 1:6). C) Neno la Mungu lina ukali kuliko upanga D) Neno la Mungu linachoma hata kuzigawanya nafsi, roho viungo na mafuta yaliyomo ndani yake E) Neno la Mungu li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo KWA NINI NENO LA MUNGU LI HAI? Neno la Mungu li hai kwa sababu Mungu mwenyewe analithibitisha kwamba li hai maana a) Linafanya mabadiliko (Isaya 55:10-11). b) Linatupa kushinda dhambi (Zaburi 119:11). c) Neno la Mungu li hai kwa sababu linatupa mafanikio katik mwili. Petro anasema ”kwa neno lako tunatupa nyavu zetu.“ Hapa tunaona kuwa Neno la Mungu pekee yake ndilo linaloweza kuleta majibu katika maisha yetu (Luka 5:3-6). Uhai wa Neno la Mungu kwa mtu ndio unaoleta kushinda dhambi. Nao wakamshinda kwa neno la ushuhuda wao (Ufunuo 12:11). Daudi aligundua au kwa maneno mengine alifahamu umuhimu wa neno la Mungu katika maisha, kama vile mtume Paulo anavyosema na Wakolosai kwa habari ya neno la Kristo kwamba likae kwa wingi ndani ya mioyo yetu Neno la Mungu lina nguvu na ndio maana tunamshinda shetani kwa neno la Mungu. Yesu kama kielelezo yeye mwenyewe ni neno ndani ya neno anamshinda shetani (Luka 4:1-12). Katika mistari hiyo tunaona Yesu anamwambia shetani ”imeandikwa“ Shetani nae anageuza usemi nae anamwambia Yesu ”imeandikwa kwamba atakuagizia malaika usije ukajikwaa mguu wako.“ Kwa kuwaYesu neno la Mungu limo ndani yake hamwambii tena shetani imeandikwa ila anamwambia imenenwa. Kwa maneno mengine tukiwa na neno la Yesu ndani yetu hatuwezi kuyumbishwa. Kwanini? Kwa sababu tumeshaona jinsi ambavyo shetani anajaribu kutumia neno la Mungu kwa kusema ”imeandikwa.“ Na ni kweli imeandikwa ananukuu kutoka kitabu cha Zaburi 91 :1-12. Hata kama shetani ananukuu maandiko haina sababu yamimi kushindwa na shetani maana Yesu tayari alikwisha mshinda. Yesu kumshinda shetani ina nipelekea mimi kusoma neno la Mungu kwa bidii sana. Kwa mfano, ni kweli kabisa imeandikwa mtakula vitu vya kufisha havitawadhuru lakini je, ninywe sumu sitakufa kwa sababu imeandikwa? Hapana, ukinywa hakika utakufa. Shetani hutumia mandiko kuwafunga wasiojua neno la KristoYesu. Katika Biblia tunasoma pia kwamba ”imeandikwa“ Wanandoa MKE na MUME wasinyimane. Kwa kutojua neno vijana wa kiume na wa kike wamedanganywa. Si hao tu hata walioko kwenye ndoa wametegwa kwa andiko hilo. Neno linasema katika Mithali 6:32 ”Aziniye na mwanamke hana akili kabisa“ na Mwanamke vivyo hivyo akizini na mwanaume hana akili kabisa. Watu wamepata hasara ya mambo mengi kwa kutojua neno la Mungu. Ili tuweze kumshinda shetani ni lazima neno la Yesu liwe ndani yetu ndiposa tutamshinda shetani. Ayubu kwa neno la Mungu alishinda. (Ayubu 19:25-27, Waefeso 6:17). Nataka nikwambie neno la Mungu ni msaada katika maisha yetu maana hutupa majibu ya maisha yetu. Katika Luka 5:3-6 tunasoma jinsi Petro na wenzake walivyopata samaki wengi kwa kutii neno la Kristo. Kumbuka pia juu ya yule akida, alimwambia Yesu ”...sema neno tu na mtumwa wangu atapona“ (Luka 7:2-10). Yesu akisema neno lazima mabadiliko yatokee. Neno la Mungu lina ukali kuliko upanga. Kwa nini neno la Mungu lina ukali kuliko upanga? Upanga unaweza kukukata na usipone. Lakini neno linakata na kuponya. Kwa neno hili wafalme wanatubu. Yona alitumia neno la Mungu likawa kali watu wakatubu. (Yona 3:1-10; Matendo ya Mitume 8:18-24). Neno la Mungu linachoma hata kuzigawa nafsi na roho na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake (Matendo 7:51-54, Yohana 4:16 -18, 27-29). Mwanamke akaambiwa mambo yake; Neno likachambua kila tabia.. Neno la Mungu li jepesi kutambua mawazo na makusudi ya moyo. Yesu kama Neno la Mungu anajua mambo ambayo watu wanawaza ndani ya mioyo yao (Luka 5:17-24, 6:6-8 ; Mathayo 16:1-4). Yapo makusudi ya moyo ambayo ni ya siri sana kwa mwanadamu lakini nataka nikuambie neno la Mungu ni jepesi kutambua makusudi ya moyo. Mtume Petro aliyependa kujua neno la Mungu, naye pia Mungu alimjalia neema ya kuyajua makusudi ya moyo wa mwanadamu (Matendo 5:1-11). Elisha aliyajua makusudi ya moyo wa mfalme ya kuwatenda Israeli kwa siri ila Mungu alimpa neema ya kuyajua mawazo ya mfalme (2 Wafalme 6:8-12). Hili ni jambo la msingi katika maisha ya Mkristo yaani kulijua neno la Mungu. Neno la Mungu tukiwa nalo na likitenda kazi ndani yetu lazima tufanikiwe (Yoshua 1:8) . Je unahitaji kuwa na imani katika neno la Mungu? Basi, ni neno la Mungu peke yake ambalo laweza kuumba imani, maana pasipo neno la Mungu hakuna imani (Waebrania 11:3 ; Warumi10:17). Ili uwe mwanafunzi wa Yesu ni lazima ulijue neno la Mungu na kulishika.(Yohana 8:31 ; Luka 2:19). Kama neno halimo ndani yetu tunayoyafanya yanakuwa hayana Mungu, hata twaweza kusalitiana. Mtu anayelitamani neno la Yesu huling’ang’ania na kulitenda maana kwake ni nguvu. (1Wakorintho 1:18). Si kwamba Neno la Mungu ni nguvu tu: bali huleta faida (Mathayo 13:23). Watu wengi tunapotea kwa kutokujua uwezo (nguvu) iliyomo katika neno la Mungu (Mathayo 22:29). Yesu anasema, mtu anayelitenda neno la Mungu na kulishika huyo amepanda mbegu ambayo itazaa sana, maana ndani ya moyo wake imo mbegu ambayo ni neno la Mungu la uponyaji na mafanikio, msamaha, utu wema na mengi yanayofanana na hayo. Yapaswa maisha yetu yawe yenye neno (mbegu) la Mungu ili tuweze kuzaa mambo mazuri. Wokovu wetu unaimarika kwenye neno la Mungu. Hilo neno la Mungu tunalipata wapi? Isaya 34:16. Upo umuhimu wa kuyachunguza maandiko ili kujua Mungu anasema nini (Matendo 17.10-11). Je, tangu ulipowekwa msingi wa wokovu, neno limo ndani? (Hagai 2:18-19). Kila kitu kinaweza kupita lakini sio neno la Mungu (Isaya 40:8, Mathayo 24:35). Ili neno litende kazi katika kinywa chako unapolitamka na kuamini ni lazima iwepo nguvu ya Roho Mtakatifu. Bila hii nguvu hamna kitakacho endelea. Utasema umeamini lakini hakutakuwa na matokeo. Mungu mwenyewe alipotamka neno liliambatana na nguvu ya Roho Mtakatifu (Mwanzo1:2-3). ****************

Wednesday, 10 February 2016

UCHAMBUZI YOHANA 17:11-26

Sura ya 17 ya Kitabu cha YOHANA, kwa kutafakari YOHANA 17:11-26.

Ingawa kichwa cha somo letu la leo ni, “UMOJA ALIOTUOMBEA YESU“,

kuna mengi zaidi ya kujifunza katika mistari hii.
Tutayagawa mafundisho yote tunayoyapata katika mistari hii katika vipengele kumi na viwili:-

(1) MAOMBI YA UMUHIMU WA KWANZA (MST. 11-24);
(2 KUTOA HOJA ZENYE NGUVU KATIKA MAOMBI (MST. 11-24);
(3) UWALINDE HAWA (MST. 11-12); (4) WAJIBUWA KUWATUNZA WATOTO WACHANGA KIROHO (MST. 12);
(5) UMOJA ALIOUTUOMBEA YESU (MST. 11, 21-23);
(6) KUWA NA FURAHA YA YESU ILIYOTIMIZWA NDANI YETU (MST. 13);
(7) KUCHUKIWA KWA MTU ANAYELIPOKEA NENO (MST. 14); (8) SIOMBI UWATOE KATIKA ULIMWENGU (MST. 15);
(9) WAO SI WA ULIMWENGU (MST. 16);
(10) UWATAKASE (MST. 17, 19); (11) KAMA ULIVYONITUMA NAMI NALIWATUMA (MST. 18);
(12) YATUPASAYO KUFANYA BAADA YA KUMJUA MUNGU (MST. 25-26).

(1) MAOMBI YA UMUHIMU WA KWANZA (MST. 11-24)
Katika mistari hii, tunaona maombi ya Yesu akiwaombea wanafunzi wake na wale watakaomwimini kwa sababu ya neno lao.

Kuna jambo kubwa la kujifunza hapa katika maombi ya Yesu. Katika maombi yake yote hakuwaombea wanafunzi wake wawe matajiri, au wawe na mali za dunia hii; wala hakuwaombea mambo ya mwilini yoyote. Maombi yake yote yalikuwa yanahusu mambo ya roho zao.

Aliomba kwamba Baba awalinde na yule mwovu na wawe na umoja (MST. 11, 15).
Aliomba kwamba furaha ya Yesu itimizwe ndani yao (MST. 13).
Aliomba kwamba watakaswe na kuishi maisha ya utakatifu (MST. 17),
na tena aliomba kwamba wawe pamoja naye mbinguni (MST. 24).

Yesu Kristo, hapa, anatufundisha maombi ya umuhimu wa kwanza. Hatuna budi kutamani KWANZA mafanikio ya kiroho kuliko kuwaza mafanikio ya kimwili tu. Katika maombi kwa ajili yetu na kwa ndugu zetu wengine, tuweke uzito zaidi kuomba maombi ya roho zetu zitakazoishi milele. Tuutafute KWANZA Ufalme wa Mungu na mengine yafuate baadaye.

(2) KUTOA HOJA ZENYE NGUVU KATIKA MAOMBI (MST. 11-24)
Yesu anatufundisha kueleza mambo yetu kwa ufasaha, na kutoa hoja zenye nguvu, tukieleza vizuri kwa nini tunataka tupewe sawasawa na kuomba kwetu. Tukifanya hivyo, tutaona Bwana akitujibu, maana neno la Mungu linatufundisha hivyo (ISAYA 43:26; 41:21).

(3) UWALINDE HAWA (MST. 11-12) Sisi kama wanafunzi wa Yesu, ni kondoo kati ya mbwa-mwitu (MATHAYO 10:16; MATENDO 20:29). Shetani anatafuta kuturarua na kutuondolea wokovu.

Hatuna budi kumwomba Mungu atulinde na yule mwovu wakati wote, na kuomba vivyo hivyo kwa wanafunzi wenzetu au kondoo wetu katika Kanisa. Hatupaswi kujiamini kupita kiasi na kutupilia mbali uwezekano wa Shetani kurarua wokovu wetu kwa kuwatumia mbwa mwitu wake.

Alimtumia mbwa-mwitu Delila kumrarua Samsoni aliyekuwa shujaa sana wa kiroho. Alimtumia mbwa-mwitu mkewe Uria kumrarua Daudi, mtu aliyeupendeza sana moyo wa Mungu. Aliwatumia mbwa-mwitu wengi (wanawake wageni), wakamgeuza moyo Sulemani aliyekuwa mwenye hekima kuliko yeyote mwingine mpaka akafuata miungu mingine (1 WAFALME 11:1-4).

Shetani aliwatumia mbwa-mwitu kumfanya Yuda ajinyonge baada ya kumsaliti Yesu na kumfanya Petro kumkana Yesu mara tatu. Anaweza kufanya hivyo kwetu pia tusipomwomba Mungu atulinde na yule mwovu wakati wote (MATHAYO 6:13). (

4) WAJIBU WA KUWATUNZA WATOTO WACHANGA KIROHO (MST. 12) Siku ya mwisho, kila mmoja wetu itamlazimu kutoa ripoti ya jinsi alivyowatunza watoto wake wachanga kiroho aliokabidhiwa na Mungu. Katika kumi na wawili,

Yesu aliwatunza wote isipokuwa mmoja tu aliyekuwa mwana wa upotevu. Yesu hapa anatuonyesha kielelezo cha kutimiza mapenzi ya Mungu katika MATHAYO 18:14.

(5) UMOJA ALIOTUOMBEA YESU (MST. 11, 21-23)
Watu wengine kwa kukosa maarifu, wanafikiri Yesu alituombea umoja wa madhehebu yote yanayojiita ya Kikristo.
Siyo sula la umoja au muungano wa makanisa yote linalotajwa hapa. Hatuna budi kuwa waangalifu na kuzijua fikra za Shetani.

Uomja wetu hauna budi kuwa kama umoja wa baba, Mwana na Roho Mtkatifu. Umoja wao unaambatana na Neno la Mungu katika Utakatifu wote. Baba ni Baba Mtakatifu,
(YOHANA 17:11).
Yesu ni Yesu Mtakatifu (MATENDO 4:30),
na Roho, ni Roho Mtakatifu (YOHANA 14:26).
Umoja wetu Wakristo lazima uzingatie misingi yote ya Utakatifu. Hivyo hatupaswi kuwa na umoja na watu wanaoabudu sanamu au wasioukiri wokovu.

Vivyo hivyo Umoja huu siyo kuwa kitu au kiungo kimoja, au muungano wa makanisa yote na kuwa kanisa au dhehebu moja tu, bali ni viungo MBALIMBALI vinavyotenda kazi kwa ushirikiano kama katika mwili wa mtu. Jicho linabaki Jicho, Sikio linabaki sikio n.k., lakini vyote vinashikiana bila kujali tofauti zao za kiutendaji kazi (1 WAKORINTHO 12:14, 17-20, 27). Kila Kanisa linabaki na jina na uongozi wake ila ikiwa wote tunaamini misingi ya wokovu na Utakatifu, basi tunashikiana bila kujali tofauti ndogo ndogo za kiutendaji.

(6) KUWA NA FURAHA YA YESU ILIYOTIMIZWA NDANI YETU (MST. 13)
Hatuna budi kuwa na furaha aliyokuwa nayo Yesu. Kilichomfurahisha kuliko vyote ilikuwa ni kuona watu wanaookolewa na kuishi sawa na m apenzi ya Mungu. Hii ndiyo kazi aliyoifurahia kuliko zote yaani kumpata kondoo au shilingi iliyopotea (LUKA 15:3-10).

Kuwa na furaha ya Yesu iliyotimizwa ndani yetu ni kufurahia kazi hii kuliko lolote jingine. Ikiwa tunafurahia mizaha, karata, bao, masengenyo, kazi za dunia hii n.k., kuliko kazi hii, tujue tumepungukiwa.

(7) KUCHUKIWA KWA MTU ANAYELIPOKEA NENO (MST. 14)
Awaye yote anayepewa neno la Mungu na kulipokea jinsi lilivyo na kuokolewa, sharti atachukiwa na ulimwengu, yaani watu ambao hawajaokoka.
Hatupaswi kuona ajabu tukichukiwa (YOHANA 15:24-25; 7:7).

(8) SIOMBI UWATOE KATIKA ULIMWENGU (MST. 15)
Baada ya kukutwa na magumu, Musa, Eliya na Yona; wote waliomba waondolewe katika ulimwengu kama wengine wanavyoomba. Yesu hatufundishi kufanya hivyo. Tunahitajika duniani kuangaza na kuwa chumvi ya ulimwengu na kuwahubiria walimwengu. Tukitolewa, nani ifanye kazi hii? Vivyo hivyo ni muhimu kufahamu kwamba kwa kuwa tuko duniani wazinzi na wenye dhambi wote watatuzunguka na kutushawishi tuwe kama wao.

Dawa siyo kutafuta kisiwa cha kukaa kama alivyowaza Yeremia (YEREMIA 9:2), bali ni kuushinda ulimwengu na majaribu yake ( 1 YOHANA 5:4).

(9) WAO SI WA ULIMWENGU (MST. 16)
Mwanafunzi wa Yesu hapaswi kuwa mtu anayeupenda ulimwengu na mitindo yake kama Dama (2 TIMOTHEO 4:10).

Kuwa rafiki wa dunia yaani kufanya mambo kama watu wa dunia hii, ni kuwa adui wa Mungu na kuonyesha kwamba hatujaokoka (YAKOBO 4:4; 1 YOHANA 2:15). Hatupaswi kuifuatisha namna ya dunia hii katika kujipamba, mavazi, usemi, n.k. (WARUMI 12:2).

(10) UWATAKASE (MST. 17, 19)
Wanafunzi wa Yesu walikuwa wameokoka, lakini bado walijawa na hasira, chuki (MARKO 10:41; LUKA 9:49-50, 51-55).

Aliomba watakaswe. Sisi nasi hatuna budi kuhakikisha kwamba tumetakaswa baada ya kuokolewa kwa kuomba Utakaso tukijua ni ahadi na mapenzi ya Mungu kwetu (1 WATHESALONIKE 5:23-24).

(11) KAMA ULIVYONITUMA NAMI NALIWATUMA (MST. 18)
Yesu Kristo anatuhakikishia kwamba ametutuma VIVYO HIVYO alivyotumwa na Baba. Ni neema iliyoje!
Kwa uhakikisho huu, ni muhimu kufahamu kwamba kuna uwezekano mia kwa mia wa kutenda kazi alizozitenda Yesu na kuzidi, tukiamini tu! (YOHANA 14:12).

(12) YATUPASAYO KUFANYA BAADA YA KUMJUA MUNGU (MST. 25-26)
Baada ya kumjua Mungu kwa kuzishika Amri zake (1 YOHANA 2:3-4), kila mmoja wetu anawajibika kuwajulisha wengine Jina la Yesu linalookoa tena na tena! ………………………………………………………………………………………………………………………………….. Ni sifa ipi ya kutuwezesha kuingia mbinguni? Ni utakatifu (WAEBRANIA 12:14).

Ndani yake hakitaingia kamwe chochote kilicho kinyonge (UFUNUO WA YOHANA 21:27).

Kinyonge ni kipi? Ni yule anayetenda dhambi.
Huyu ni mtu asiyefaa, ni mnyonge! Je, wewe ni mtakatifu?
Jibu ni la!
Maisha yako yamejaa dhambi, pamoja na kusema una dini;
hivyo wewe pia ni mnyonge, hufai kuingia mbinguni.

Ukitubu leo dhambi zako zote kwa kumaanisha kuziacha, na kuifuata njia ya Yesu Kristo, ndipo utakapopata rehema ya kuingia mbinguni (MITHALI 28:13; YOHANA 14:6).

Je, uko tayari kutubu sasa ili upate rehema hii? Najua uko tayari. Basi fuatisha sala hii ya toba kwa dhati kutoka moyoni;

Mungu Baba asante kwa ujumbe huu. Hakika mimi ni mnyonge, mwenye dhambi. Sistahili kuingia mbinguni. Natubu dhambi zangu zote kwa kumaanisha kuziacha. Kuanzia leo nataka niifuate njia ya Yesu Kristo. Bwana Yesu niwezeshe. Asante kwa kunisikia katika Jina la Yesu. Amen

0767/15 445846

Ni Mimi Ndugu yako
Ev. Elimeleck S Ndashikiwe
       
elimelck@gmail.com.

Tuesday, 9 February 2016

WORLD WAR

Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia Shirikiano za kijeshi katika Ulaya mwaka 1915. Nyekundu: Mataifa ya Kati; kijani: Mataifa ya Ushirikiano; njano: mataifa yasiyoshiriki vita Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia:

1.Mifereji huko Verdun (Ufaransa) baada ya kulimwa kwa mizinga mikubwa;
2. Ndege za kijeshi na faru za kwanza;
3. bunduki ya mtombo na manowari Ramani ya dunia ikionyesha nchi na maeneo yaliyoshiriki katika Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia.
Kijani: Mataifa ya Ushirikiano; njano: Mataifa ya Kati; nchi zisizoshiriki kwa rangi ya kijivu Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia ilikuwa vita iliyopigwa kuanzia mwaka 1914 hadi 1918. Mataifa wapiganaji yalikuwa Ujerumani, Austria-Hungaria, Bulgaria na Uturuki (ziliitwa "Mataifa ya Kati") kwa upande mmoja dhidi ya Ufaransa, Urusi, Uingereza, Italia, Marekani na nchi mbalimbali zilizoshirikiana nazo (zilitwa "Mataifa ya Ushirikiano"). Vita hii ilianza katika Ulaya ikapanuka haraka hadi Mashariki ya Kati, Afrika na Asia ya Mashariki ikasababisha kifo cha takriban watu milioni tisa. Yaliyomo 1 Sababu na matokeo 2 Hali kabla ya vita 3 Mwanzo wa vita 4 Vita katika nchi mbalimbali 5 Vita katika makoloni 6 Mwisho wa vita 7 Mkutano wa Paris 8 Vita ya kwanza ya dunia? 9 Tanbihi 10 Marejeo 11 Viungo vya nje 11.1 Ramani hai Sababu na matokeoEdit Sababu yake ilikuwa mashindano makali kati ya mataifa ya Ulaya kuhusu kushika nafasi ya kipaumbele barani Ulaya na duniani kote. Matokeo yake yalikuwa mwisho wa kipaumbele cha Ulaya duniani na kupanda ngazi kwa Marekani, mapinduzi katika nchi mbalimbali, mwisho wa falme za Ujerumani, Austria na Urusi pamoja na mwanzo wa utawala wa kikomunisti katika Urusi, mwisho wa Dola la Austria-Hungaria na wa Dola la Uturuki la Kiosmani pamoja na mwisho wa ukoloni wa Kijerumani duniani. Katika Ulaya nchi mpya zilijitokeza kama vile Chekoslovakia, Finland, Latvia, Estonia na Yugoslavia pamoja na nchi za zamani zilizotokea tena katika uwanja wa kimataifa ndizo Austria, Hungaria, Lithuania na Poland. Hali kabla ya vitaEdit Sehemu kubwa ya Ulaya iliwahi kuwa na kipindi kirefu cha amani tangu vita kati ya Ufaransa na Ujerumani mnamo 1870-1871. Mataifa ya Ulaya yalikuwa na mfumo wa mikataba na mapatano kati yao yaliyolenga kuhakikisha uwiano wa mataifa. Mataifa makubwa ya Ulaya yalikuwa Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Urusi na Italia. Hali ilikuwa tofauti katika Kusini-Mashariki mwa bara hilo. Hadi nusu ya pili ya karne ya 19 sehemu kubwa ya Balkani ilitawaliwa na Milki ya Osmani iliyokuwa milki ya Kiislamu ya kutawala Wakristo wengi. Milki hii iliendelea kudhoofika wakati wa karne ya 19. Nchi mbalimbali zilijitenga na kupata uhuru, kama vile Ugiriki, Serbia, Bulgaria na Romania. Nchi hizi mpya zilipigana kivita kati yao na Milki ya Osmani hadi mwaka 1912. Mwanzo wa vitaEdit Vita Kuu ilianza kutokana na ugomvi kati ya Austria-Hungaria na Serbia. Kutokana na muundo wa mikataba ya kusaidiana kati ya nchi za Ulaya mwanzo huo ulisababisha mfululizo wa hali ya vita kati ya mataifa, na mengine ya Balkani yalitafuta uhuru wao. Tarehe 28 Juni 1914 katika mji wa Sarayevo, Bosnia, mwana wa Kaisari wa Austria aliyekuwa mfalme mteule aliuawa pamoja na mke wake na mgaidi Mserbia mwanachama wa kundi la "Mkono Mweusi" lililopinga utawala wa Austria-Hungaria katika Bosnia. Austria ilidai Serbia ifuate masharti makali katika uchunguzi wa tendo lile. Serbia ilipokataa sehemu ya masharti, Austria ilitangaza hali ya vita dhidi ya Serbia tarehe 28 Julai 1914. Agosti ya 1914 iliona kupanuka kwa vita hii: Warusi walikuwa na mkataba wa usaidizi na Serbia wakatangaza hali ya vita dhidi ya Austria-Hungaria. Hapo wakaingia Wajerumani waliokuwa na mapatano ya usaidizi na Austria-Hungaria wakitangaza hali ya vita dhidi ya Urusi. Urusi kwa upande wake ulikuwa na mkataba wa kusaidiana na Ufaransa, hivyo hali ya vita ikajitokeza pia kati ya Ufaransa na Ujerumani. Uingereza ulijiunga na vita baada ya Wajerumani kuanza kuingia eneo la Ubelgiji kwa shabaha ya kuvuka haraka ili wavamie Ufaransa Kaskazini. Kuanzia Oktoba 1914 Milki ya Osmani (Uturuki) ilijiunga na vita kufuatana na mkataba wake wa siri na Ujerumani. Mwaka 1915 Italia ilijiunga na Wafaransa na Waingereza kwa kushambulia Austria-Hungaria, ingawa awali ilikuwa na mkataba na dola hilo. Vita katika nchi mbalimbaliEdit Vita ilipigwa kwa ukali miaka ya 1914-1918. Wajerumani waliingia ndani ya Ufaransa lakini walikwama kabla ya kufikia mji mkuu wa Paris. Kwa muda mrefu mstari wa mapambano ulibaki palepale. Katika Mashariki Wajerumani walifaulu kurudisha mashambulio ya Kirusi na kuteka sehemu za Urusi. Katika Kusini mwa Ulaya Waustria walifaulu kwa shida kubwa kuteka Serbia na Montenegro pamoja na Albania. Waturuki walishindwa kwa ujumla katika mashambulio yao dhidi ya Warusi katika eneo la Kaukazi na dhidi ya Waingereza katika Misri. Lakini walifaulu kuzuia Waingereza wasifike Uturuki penyewe. Waingereza walipeleka jeshi katika Irak ya kusini wakafaulu kuwarudisha Waturuki hadi kaskazini ya nchi hii. Vita katika makoloniEdit Vita ilienea haraka baharini na katika makoloni ya Ujerumani yaliyovamiwa na Waingereza, Wafaransa, Afrika Kusini na Japani. Makoloni yalikuwepo Afrika na kwenye visiwa vya Pasifiki pamoja na China. Ujerumani ilikuwa na vikosi vya kijeshi katika makoloni ya Afrika na pia huko Qingdao nchini China. Kwa ujumla makoloni yote yasiyokuwa na jeshi yalitekwa na mataifa ya ushirikiano bila mapigano. Afrika ya Kusini-Magharibi ya Kijerumani ilivamiwa na Afrika Kusini na jeshi la ulinzi la Kijerumani likajisalimisha mnamo Julai 1915. Kamerun ilivamiwa na Ufaransa na Uingereza kutoka makoloni yao ya Nigeria na Afrika ya Kati ya Kifaransa. Jeshi la ulinzi likajisalimisha katika Februari 1916. Afrika ya Mashariki ya Kijerumani ilikuwa mahali pa mapigano yaliyoendelea kwa miaka yote ya vita. Jeshi la Ulinzi wa Kijerumani chini ya uongozi wa Paul von Lettow-Vorbeck lilifaulu kutetea eneo la koloni dhidi ya mashambulio ya kwanza ya Waingereza kutoka Kenya hadi 1916. Kwenye Novemba 1914 jeshi la askari 8,000