Pages

Subscribe:

Saturday, 12 November 2016

METHUSELA MTU ALIYEISHI MIAKA 969 NDIPO AKAFA. Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi.BWANA Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi.Akamwita Adam,Adam akaishi miaka 130 ndipo akazaa mtoto wake wa kwanza akamwita jina lake Kaini(Cain).Siku zote za Adam ni miaka 930 naye akafa.Vikapita vizazi vichache akazaliwa HENOKO mtu huyu inasadikika kuwa hakufa bali MUNGU alimchukua kwakua huyu jamaa alikua mtakatifu duniani.Wakati Mungu anamchujua Henoko alikua na miaka 365.Wakati Mungu anamchukua alikua amemzaa METHUSELA mtu huyu ndiye aliishi miaka mingi kuliko mwanadamu mwingine.Methusela aliishi miaka 969 akafa. Tazama picha hii hapa chini.  KIMO Henoko ambaye hakufa,yaani kifo hakijui wala hakimjui,alikua na Urefu wa futi 450 kwenda juu.Lakini mwanadamu wa sasa anafuti chache sana.Hilo ni badiliko kubwa sana ambalo BWANA MUNGU alilifanya kwani kiwango cha hewa ya oksijeni kilikua ni kikubwa sana.Hivyo mwanadamu pamoja na viumbe wengine walikua na maumbo makubwa.Na kupungua kwa umri kulikua hivi: Soma Kitabu cha MWANZO 6:4. MALAIKA Malaika wa Mbinguni waliomwasi Muumba wao walishuka duniani''wana wa Mungu'' wakawapenda mabinti''wana wa wanadamu''wakajitwalia wake wowote walio watamani''.Hapa akataja WANEFILI yaani majitu makubwa.Majitu haya ilikua ni machotara ya malaika na wanadamu. Tazama picha hii.  KITABU CHA HENOKO. Kitabu hiki alikiandika Henoko mwenyewe japo nakala zake ni nadra kupatikana.Aliandika akionesha jinsi maovu yalivyokua yamezidi duniani kiasi kwamba MUNGU akaamua kuangamiza kila kitu chenye uhai.Yaani uumbaji wa Munguulichakachuliwa na malaika waasi kwa msaada wa shetani waka fanya dhambi na wanadamu,wanyama wa mwituni,wanyama wa kufungwa,ndege wa angani na samai wa baharini.Hivyo dunia yote ikajaa viumbe bandia ambao kwenye orodha ya ADAM aliyoandika na kumkabidhi BWANA MUNGU viumbe hao majina yao hayakuwemo. Yasemekana wanadamu hao wapya walikua wakubwa sana kupita umbile alilokua nalo Henoko japo yeye mwenyewe alikua na urefu wa futi 450 hao machotara wenye damu mchanganyiko ya malaika na mwanadamu walikua watu wenye nguvu sana na wakubwa sana kwa upana na urefu.Ndio walioleta uchawi duniani.Wanadamu hao hujulikana kwa majina mbalimbali kama vile:-WANEFILI''NEPHILIM'' au WANA WA ANAKI''ANUNNAK''Soma katika Kitabu cha biblia Hesabu13:33 Machotara hao MUNGU hakuwapenda kabisa kwani walikua nusu wanadamu nusu malaika.Yaani wana nguvu za kibinadamu lakini pia wananguvu za kiroho nyingi sana kuliko wanadamu wakawaida.Hapo ndipo Mungu akashusha gharika a.k.a GHARIKA YA NUHU''lengo ni kufutilia mbali viumbe wote wa ajabuajabu.Ambao yeye hakuwaumba.Lakini baadhi ya viumbe hao waliikwepa gharika kutokana na nguvu za kiroho walizokua nazo maana walikua ni ''wana wa mungu'' waliooa wana wa wanadamu''hivyo watoto waliozaliwa baba zao walikua ni MALAIKA na mama zao walikua ni WANADAMU. Malaika hao walio asi ndio walio sababisha sayansi ya ajabu sana inayoitwa HYBRID kuzalisha viumbe wapya kwakuchanganya damu ya viumbe mbalimbali waliona maumbile mbalimbali sana.KITABU CHA HENOKO kinasema wakatenda dhambi na samaki wa baharini''akazaliwa samaki mtu''wakatenda dhambi na wanyama''akapatikana mtu mwenye sura nusu mtu nusu ng'ombe,nk.DHAMBI MBAYA SANA MUNGU AKAKASIRIKA,AKAUA DUNIA NZIMA YA WAKATI ULE. DUNIA YA SASA. Wamejitahidi kumkosoa MUNGU,wametenda dhambi na wanyama''kuna wanyama leo hii wanaitwa LIGER=lion+tiger Tazama picha chini.  Maana yake ninini kama wanyama wote Mungu aliowaumba ADAM akapewa jukumu la kuwaita majina na orodha akamkabidhi Mungu huyu ''liger''yuko kwenye orodha gani?Tunamkasirisha MUNGU alete adhabu nyingine ya kubakisha viumbe orijino na kuharibu viumbe feki wote. AMERIKA Nchini Marekani kwasasa wanasayansi wamefaulu kuvumbua ''steam gene''yaani mashina ya chegmbe za mwili ambapo mwanadamu hawezi kuzeeka kamwe.Na majaribio kadhaa yamefanyika yakaonekana kua ni sahihi kabisa.Watu waliofanyiwa majaribio mwaka 1816 mpaka leo wametimiza miaka 200 wakionekana ni vijana wenye umri uleule walipopandikizwa seli hizo wakiwa na umri wa miaka26.Je,jaribio kama hilo Mungu afanyeje? Tazama picha hii tena.  Wanadamu wametenda dhambi kwa punda+pundamilia=zedonk. Kitoto cha punda huyo..punda mwenyewe anashangaa heee!Wewe nani maana wamechukua chembe za wanyama waliokaribu wakazalisha feki yake. Tazama picha hii tena.  Huyu mnyama ukimtazama juujuutu unaweza sema ni funda au ni farasi,lakini ndugu msomaji huyu anaitwa''mule''punda+farasi.Mnyama huyu yeye sio punda wala sio farasi hata kwenye orodha ya ADAM aliyoandika majina hayupo.MUNGU MUUMBAJI AFANYE JE KUTETEA SIFA YAKE YA KUUMBA? MWANADAMU ANAVYO FURAHIA DHAMBI YAKE. Kuku wa kisasa,bata wa kisasa,punda wa kisasa''zedonk''simba wa kisasa''liger''Farasi wa kisasa''mule''machungwa ya kisasa,nk.Vyakula vyote unavyo fahamu vya kisayansi ni dhambi kwa MUNGU,Kwakua ni dhambi kamwe haviwezi kumaliza njaa duniani''kuku feki=kuku wa kisasa'',mayai feki=mayai ya kisasa''uyonga feki,ngano feki,mahindi feki''hybrid maize''.HYBRID ZOTE UNAZO ZIFAHAMU KATIKA VIUMBE HAI.Vinamkasirisha sana Mungu kwa kuingilia kazi yake ya uumbaji.Ndiyo maana amevilaani haviwezi kumshibisha mwanamu.Bali njaa kila mahali haiishi.

Friday, 4 November 2016

KUFUNGA NA KUOMBA KWANGU MKRISTO

AINA ZA KUFUNGA.
Zipo aina tano ( 5 ) za kufunga.

1. TOTAL FAST (FUNGA KAVU).
Absolute fasting (Funga iliyo sahihi)

Hii ni funga ya kutokula chakula kabisa wala kunya maji kwa siku zisizo zidi tatu (3)
kama (Esta 4:16).

b. Supernatural Fasting (Funga ya Kiungu).
Funga ya kutokula chakula kabisa wala kunywa maji kwa siku zaidi ya tatu (3) kama Musa
(Kumb.9:9 & 9:18) kwa siku 40.

2. PARTIAL FASTING (FUNGA NUSU)
a. Yohana Mbatizaji aliamua kufunga maisha yake yote akila asali na Nzige tu. Dan. 10:2-3
Kuacha kula aina maalumu ya vyakula ambavyo ungevipenda.

b. Funga ya milo miwili au mmoja kwa siku.
c. Funga ya kawaida (Normal fasting).Kunya maji tu.

3. FUNGA YA KULAZIMISHWA (IMPOSED FAST).
Matendo 28:1
Safari ya Paulo akielekea Rumi.Kwasababu ya misukosuko ya mawimbi majini watu wanashindwa kula.

Pia kama mtu anaumwa unakosa hamu ya chakula.Mala nyingine tunapata misukosuko kama sehemu ya Maisha kiroho pia.

4. FUNGA YA WAZI/KANISA, HADHARA AU TAIFA.
(PUBLIC AND NATIONAL/CHURCH FASTS).
Hii inakuwa funga ambayo inatangazwa na inakuwa wazi kwa kila mtu.Sio za siri.
Yona 3:6. 5.

Funga ya mtu binafsi Hii hufanywa na mtu mmoja kwa siri na mungu wake hapana anayejua mtu huyo kama amefunga.

SIFA 7 ZA KUFUNGA NA KUOMBA KUNAKOONGEA
1. Huongozwa na roho wa Mungu
Marko 1:12-14,
Yesu aliongozwa na roho kufunga nyikani ndio
maana hakutenda dhambi katika kufunga na kuomba kwake.

2. Lazima iwe katika kweli ya Mungu. Kama funga na kuomba huko hakuko katika
roho hakuwezi kuwa katika kweli kwa kuwa roho wa mungu hatenganishwi na kweli ya Mungu.
2samwel12:16-17

Daudi alijaribu kufunga na kuomba ili motto aliyezaliwa katika zinaa asife hakufanikiwa
kwa kuwa Mungu tayari alisema atakufa hakika.

Hata alipokuwa ameshakufa daudi aliendelea kufunga hii inadhihirisha kuwa hakuwa rohoni kwa sababu alijua anachoomba
siyo mapenzi ya Mungu.

Angekuwa rohoni roho angemjulisha aache kuomba kwa kuwa Mungu amekataa.

3. Lazima uwe mtu wa Mungu uliyeitwa kwa jina lake 1cronicles
(2Nya 7:14a

Hapa tunaona Mungu anadhirisha kuwa si kila mtu wa Mungu ameitwa kwa jina lake. Aliyeitwa kwa jina lake ni Yule aliyezaliwa mara ya pili katika roho mtakatifu
(Yohana 1:11-13) 4.

Lazima funga ifanywe katika unyenyekevu wa hali ya juu wa rohoni.

Mtu anayefunga kwa kiburi cha uzima hawezi kupata matokeo yaliyokusudiwa. Mfano
unafunga ili ujilipizie hasira yako kwa mtu anayekudharau au kutesa, unataka kushindana na wengine,
unataka kuonesha kwamba wewe ni mwamba kanisani kwenu nk.
Isaya 58:3-4)

“Husema mbona tumefunga lakini huoni, mbona tumejitaabisha nafsi zetu lakini huangalii?

Fahamuni siku ya kufunga kwenu mnatafuta anasa zenu wenyewe, na kuwalemea wote watendao kazi kwenu, Tazama
ninyi mwafunga mpate kushindana, kugombana na kupiga ngumi ya uovu” 5.

Lazima ifanywe katika furaha ya roho mtakatifu na siyo kwa kujilazimisha na kunung’unika Ukifunga kama andiko la
Isaya 58:3
inasema (mbona tumefunga lakini huoni,
mbona tumejitaabisha nafsi zetu lakini huangalii?

Hutapata matokeo yaliyokusudiwa. Badala yake fanya funga na maombi yaliyojaa furaha ya roho mtakatifu
Mathayo 6:16-18

“tena mfungapo msiwe kama wanafiki, wenye uso wa kukunjamana, maana hujiumbua nyuso zao ili waonekane na watu kuwa wanafunga,

amini nawaambia wamekwishakupata thawabu yao.

Bali wewe ufungapio jipake mafuta kichwani,
unawe uso ili usionekane na watu kuwa unafunga, ila na baba yako aliye sirini na baba yako aonaye sirini atakujazi” linganisha andiko hilo na
Isaya 58:5 6.

Lazima kufunga kuambatane na kuomba na kuutafuta uso wa bwana 2Nya 7:14, 7.

Lazima kufunga na kuomba kufuate kanuni ya upendo na si ubinafsi. Yaani kumpenda
Mungu na jirani kama nafsi yako mwenyewe.

Matendo ya upendo kwa mungu na watu ni kama
1. hicho ambacho ungekula mpe Yesu ale. Unadhani Yesu anapatikana kanisani?
Hapana, msikie mwenyewe anapatikana wapi katika

Math 25:34-40

“Kisha mfalme akawaambia wale walioko mkono wake wa kuume, njooni mliobarikiwa
na baba yangu, urithini ufalme muliowekewa tayari tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu kwa maana nalikuwa
na njaa mkanipa chakula, nalikuwa na kiu mkaninywesha, nalikuwa mgeni mkanikaribisha, nalikuwa uchi mkanivika,

nalikuwa mgonjwa mkaja kunitazama, nalikuwa kifungoni mkanijia………………………………………amini nawaambia yoyote mliyowatendea mmojawapo ya hao ndugu zangu walio wadogo mlinitendea mimi”

NB: Linganisha andiko hilo na
Isaya 58:6a, 7

Je, Swaumu niliyoichagua mimi siyo ya namna hii?……………. je siyo kuwagawia wenye njaa chakula chako na kuwaleta maskini waliotupwa nje nyumbani mwako?

Umwonapo mtu aliye uchi umvike nguo, wala usijifiche na mtu mwenye damu moja nawe”

2. Ombea watu wengine kama familia, jamii yako, familia na taifa kwa nguvu ileile unayotumia kuombea mahitaji yako binafsi.

Isaya 58:6,
2Samweli 22: 25-26.
“ kwa mtu mwenye fadhili utakuwa mwenye fadhili, kwa mkamilifu utajionyesha
kuwa mkamilifu, kwake ajitakasaye utajionyesha kuwa mtakatifu na kwa mpotovu utajionyesha kuwa mkaidi”

Nehemia 1:1-11
jinsi Nehemia alivyolia na kutubu kwa habari ya mabaya yaliyoipata Israel na Yeusalem
hakujali kuwa alikuwa mahali salama.

Danieli 9
jinsi alivyolia kwa Mungu kwa habari ya wayahudi hata kama yeye mwenyewe alikuwa ikulu akiheshimika sana.

Au Ester ambaye alikuwa mke wa mfalme Ahusueoro angeweza kubaki alivyo lakini alifunga na kupomba kwa ajili ya
ndugu zake

SABABU /FAIDA 12 ZA KUFUNGA NA KUOMBA KATIKA KANISA
(MTU AU USHIRIKA)

1. Tunafunga kuonyesha utii kwa neno la Mungu
(Yoeli 2:12)
Biblia kuanzia agano la kale hadi agano jipya inaonyesha umuhimu wa kufunga.

Watumishi wote wa Mungu walikuwa wanafunga katika siku za maisha yao hivyo
unavyofunga unaonyesha utii katika kulifuata neno la Mungu na kuliamini.

Yesu Pia alisema kuwa siku zinakuja ambapo tutalazimika kufunga.
(Mathayo 9:15)

2. Tunafunga ili kujinyenyekeza mbele za Mungu na kupata nguvu na neema yake.
Tunahitaji neema ya Mungu siku zote ili tuweze kuishi, na ili kuipata inatubidi kujinyenyekeza chini ya mkono wake ulio hodari,

Ebrania 4:16, na Yakobo 4:10.

Ezra aliwaamuru watu wafunge ili wapate kujinyenyekeza
mbele za Mungu na kupata neema yake kwa ajili ya taifa lao,
Ezra 8:21. 3.

Tunafunga ili kuomba rehema Yesu alichukua dhambi zetu zote msalabani, inawezekana kuna jambo unaona unashindwa
kuacha na umejaribu sana. Hapo unatakiwa kufunga na kuomba rehema ili Mungu akuwezeshe kushinda. Pia unafunga kuomba rehema kwa ajili ya wengine mfano familia, jamaa na taifa pia.

Daniel alifunga na kuomba rehema kwa ajili ya dhambi za taifa la Israeli na kubeba uovu wao mbele za Mungu. Danieli 9:3-5.

Taifa la Ninawi walifunga na kuomba rehema kwa Mungu kutokana na uovu wao.
Yona 3:5-10 4.

Tunafunga ili katika udhaifu wetu Nguvu ya Mungu ionekane Unapofunga unakuwa umeikana nafsi na kumchagua Mungu,
uankuwa umedhamiria moyoni kutaka kuona nguvu ya Mungu ikionekana na sio nguvu yako.
Zaburi 109:24-28,
2Korintho 12:9-10 5.

Tunafunga kupata msaada wa Mungu katika kukamilisha kusudi lake Viongozi wa
kanisa la Antiokia walifunga na kuomba kabla ya kuwatuma Paulo na Barnabas.

Walifanya hivi ili waweze fanya uchaguzi sahihi chini ya uongozi wa Mungu.

Na Paulo na Barnabas
walikuwa wakifanya hivyo katika miji waliyotembelea kila walipokuwa wanataka
kuchagua viongozi.

Kutokana na jambo hili makanisa yale yalizidi kusonga mbele maana walimshirikisha Mungu kwa kufunga katika maamuzi yao yote.
Matendo 13:3-4, 14:23 6.

Tunafunga wakati wa taabu Mordekai na Esta walitangaza kufunga kwa wayahudi wote pale
ilipofahamika kuwa kuna mpango wa kuwateketeza wayahudi wote, na kupitia kufunga na kuomba huku wayahudi walisalimika.
Ester 4:15-16.

Wakati wa taabu ni wakati wa kufunga na kumlilia Mungu na hakika Mungu ataonekana.
Mfalme Yehoshafati pia alitangaza kufunga pale walipokuwa wamevamiwa na maadui wengi na wao hawakuwa na uwezo
wa kupigana nao
2Nyakati 20.

Tumeona kwa uchache jinsi kufunga kulivyo muhimu katika maisha yetu ya kila siku. 7.

Kufunga hunoa Imani (ili iwe kali) na huongeza ujasiri.

Esta 4:16.
Huyu mama asingefunga alikuwa hana ujasiri
wala imani ya kuingia kwa mfalme kinyume cha sheria – kwasababu adhabu yake ilikuwa ni kifo.

Ndio maana aliomba wayahudi wote walio kuwa shushani wambebe kwa maombi.

8. Kufunga huleta unyenyekevu mbele za Mungu.
Luka 14:11 & 18:14 Ezra 8:21.

Mungu huwapa wanyenye kevu neema,na kuwainua.
(1Petro5:5-6).

Ukitaka kuwa mnyenyekevu mbele za Mungu basi jifunze kuwa mfungaji. 9. Kufunga huongeza/huleta nguvu ya Maombi na kuondoa ukame wa kiroho.
Zaburi 35:13

Kufunga ni kama 4WD ya maombi.
ISAYA 40:31
na Mithali 20:13. 10.

Kufunga hufanya ulimwengu wa roho uwe wazi.

Daniel 10:14.
Baada ya Danieli kufunga siku 21 alianza kuonyeshwa na Mungu mambo ya siku za mwisho
za dunia ambako hata 11. Kukuza kanisa na huduma ya Mungu a. Hili tendo lililofanywa sana na mitume na wafuasi wao.
Mdo 14:22.

Kukua kwa Kanisa la kwanza kulitegemea Maombi ya kufunga.

b. Ushuhuda wa Paulo kuhusu maisha yake.Akafanikiwa sana kwa sababu ya maombi ya kufunga.

2Koritho 6:4-6. 12.

Kutiisha miili yetu ipate kumtii Kristo. Miili yetu siku zote hupingana na Roho Mtakatifu.

Galatia 5:16-17.
nia ya Mwilini uadui dhidi ya Mungu
Rumi 8:7-8
hivyo inabidi tuiitiishe kwa kufunga
1Kor.9:27.

Mungu akubariki mpendwa wangu!

Ni Mimi ndugu yako

Ev. Elimeleck S Ndashikiwe
   +255767445846 &
    +255715445846

Thursday, 3 November 2016

MAISHA YA WOKOVU, MTUME PAULO

Pasaka/Mikate Isiyo na Chachu Kristo aliishika Idi au Sikukuu ya Mikate Isiyo na Chachu, sawa na Paulo na wengine, kwa hiyo na sisi tunapaswa kuishika. Matendo 12:3 Na akiona ya kuwa imewapendeza Wayahudi akaendelea akamshika na Petro. Siku hizo zilikuwa siku za mikate isiyochachwa. Matendo 20:6 Sisi tukatweka baada ya siku za mikate isiyotiwa chachu, tukatoka Filipi, tukawafikia Troa, safari ya siku tano, tukakaa huko siku saba. 1Wakorintho 5:8 basi na tuifanye karamu, si kwa chachu ya kale, wala kwa chachu ya uovu na ubaya, bali kwa yasiyochachika, ndio weupe wa moyo na kweli. Miandamo ya Mwezi Wakolosai 2:16 Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato; Kwa suala la Mwandamo wa Mwezi, hapa tunamuona Paulo akiwaambia wamataifa wasione haya kushika na kuadhimisha zile zilizokuwa zinajulikana kama Sikukuu za Wayahudi ambazo sasa ni zao pia. Kristo alitilia maanani Miandamo ya Mwezi na kuichukulia kama jambo muhimu, kwa kuwa kama Paulo angeenda kinyue na kupingana na Kristo na Paulo akaishika Miandamo ya Mwezi inaonyesha kuwa Kristo alifanya hivyo pia. Aliziishika sheria na Sikukuu, na Miandamo ya Mwezi na ziliadhimishwa kwa uaminifu mkubwa kwenye imani au dini ya Kiyahudi hadi kuangamizwa kwa Hekalu, na Kristo alikuwa ni Mfalme na ni Kuhani Mkuu aliyewekwa asiye na dhambi. Kuidai na kuamini kuwa andiko hili limeondoa umuhimu wa kuziadhimisha Sabato, Miandamo ya Mwezi na Sikukuu zilizoamriwa ni kutumia vibaya kabisa matumizi ya lugha zote mbili, yaani Kyunani ya Kiingereza. Sikukuu ya Vibanda Yohana 7:2 Na sikukuu ya Wayahudi, Sikukuu ya Vibanda, ilikuwa karibu. Kama Kristo alivyoishika Sikuuu ya Vibanda, ndivyo pia Paulo alivyofanya na ndivyo hata sisi tunavyotakiwa kufanya. Matendo 18:18-21 Baada ya hayo Paulo akazidi kukaa huko siku nyingi, kisha akaagana na ndugu akaabiri kwenda Shamu; na Prisila na Akila wakaenda pamoja naye, alipokwisha kunyoa kichwa chake huko Kenkrea; maana alikuwa ana nadhiri. 19 Wakafika Efeso, akawaacha huko. Yeye mwenyewe akaingia katika sinagogi, akahojiana na Wayahudi. 20 Walipomtaka akae wakati mwingi zaidi, hakukubali; 21 bali aliagana nao, akisema, Nitarejea kwenu tena, Mungu akinijalia. Akatweka, akatoka Efeso, Hii ni nadhiri ambayo inapaswa ikamilike huko Yerusalemu wakati alipokwenda huko kama tunavyoona hapo juu. Kwa kuwa wasomaji wengi wa Injili ya Yohana walikuwa sio Wayahudi, ilikuwa muhimu kutumia neno “Wayahudi” katika kuitja sikukuu hii kama Sikukuu ya Vibanda ya Wayahudi (Yohana 7:2). Matendo na mwenendo wa Kristo unaonyesha kutilia kwake umuhimu utunzaji wa Sikukuu, kama alivyo waambia na kuwasisitiza watu wa familia yake waende kuishika kwenye Yohana 7:8, na aya ya 10 tunaona kwamba yeye mwenyewe pia alikwenda kuishika Sikukuu hii. Ingawaje viongozi wa dini wa wakati ule walitafuta kumuua, hii haikumzuia Kristo kwenda kuishika na kuingia hadi ndani ya Hekalu ambako alikuwa anafundisha pia (Yohana 7:14). Ukweli huu unatuacha sisi tukwa hatuna udhuru wowote wa kutoishika au kuadhimisha siku hizi za muhimu. Sikukuu ambayo Paulo alikuwa anaitaja inaweza kuwa ilikuwa ni Sikukuu ya Vibanda tu. Kupangilia upya kwa ratiba ya safari ya Paulo unaonyesha kuwa alikuwa makini kuiadhimisha. Alifika huko Korintho (Matendo 18:1) na akakaa nyumbani kwa Yusto kwa miezi 18 (Matendo 18:11). Ksha akasafiri hadi Yerusalemu, ambako aliwasili majira ya kipupwe ya mwaka 52-53 BK. Paulo kwa wazi anaona hitaji na umuhimu wa kuitunza Sikukuu ya Vibanda mjini Yerusalemu, ambako ndiko yalikuwa makao makuu ya Kanisa kwa wakati ule. Upatanisho Matendo 27:9 Na wakati mwingi ulipokwisha kupita, na safari ikiwa ina hatari sasa, kwa sababu siku za kufunga zilikuwa zimekwisha kupita, Paulo akawaonya, Bullinger anasema kwenye ufafanuzi wake kuhusu aya ya 9 juu ya mfungu huu wa saumu kuwa ulifanyika siku ya kumi ya mwezi wa saba, ambayo ni Siku ya Upatanisho. Anadhani kuwa ilikuwa ni tarehe 1 Oktoba ya mwaka ule (Companion Bible). I wazi kabisa kwamba Paulo alishika sheria ama torati kama alivyofanya Kristo. Tunajua kwamba Torati haikutanguliwa na yeyote kwa kuwa Kristo anasema kwenye Mathayo 5:17-18 kwamba: Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza. 18 Kwa maana, amin, nawaambia ,Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka,yodi moja wala nukta moja ya torati haitaoondoka ,hata yote yatimie. Ufunuo 22:6 Kisha akaniambia, Maneno haya ni amini na kweli. Naye Bwana, Mungu wa roho za manabii, alimtuma malaika wake kuwaonyesha watumwa wake mambo ambayo hayana budi kuwako upesi. Hadi matukio haya yalipokuwa yanatimilika yote yalikuwa hayajatimilika Dhambi ni uasi na uvunjaji wa sheria (1Yohana 3:4). Kama Paulo hakushika sheria, basi alikuwa akitenda dhambi. Na iwapo kama alizivunja sheria kwa kiufanya mambo aliyokuwa anayafanya Kristo, basi tutasema kuwa Kristo alikuwa anafanya dhambi pia. Lawama atakayopewa Paulo kwa kuishika kwake sheria ni lawama ya kumshambulia Kristo pia. Ni nani hawa watakatifu wa Mungu? Hawa ni wale wanaoishika sheria au Amri za Mungu na ushuhuda wa Yesu Kristo (Ufunuo 12:17; 14:12). Na ni lini ilitimilika? Utimilifu wa Ufufuo wa wafu na Hukumu na kushuka kwa Mji wa Mungu ndiko kukamilika kwa mpango au mchakato huu na kufanya mwisho na hitimisho kuukomesha uasi na kuwaleta viumbe wote kwa Mungu, mbingu na dunia havitapita na sheria itasimama. Tuna kazi nginyine mbele yetu ambayo itagharimu maisha yetu na imani kuendelea katika sheria au Torati ya Mungu kama zilivyotolewa kutoka asili yake ambayo tutairithi.

HISTORIA YA MTUME PAULO

Paulo na Torati Huyu Paulo Ni Nani Juna asilia la Paulo hapo mwanzo lilikuwa ni Sauli ndlo alilopewa. Matendo 13:9 Lakini Sauli, ambaye ndiye Paulo, akijaa Roho Mtakatifu, akamkazia macho, akasema... (Tafsiri ya RSV ililitumia mahali pengi ila pale tu ilipokuwa lazima ndipo hailitumii.) Matendo 9:11 Bwana akamwambia, Simama, enenda zako katika njia iitwayo Nyofu, ukaulize katika nyumba ya Yuda mtu aitwaye Sauli, wa Tarso; maana, angalia, anaomba; Sehemu ya kwanza kulitaja jina hili la Sauli ni kwenye kitabu cha Matendo, mapema kabla ya kuongoka kwake kwenye tukio la kuuawa kwa kupigwa mawe kwa Stefano. Matendo 7:58 wakamtoa nje ya mji, wakampiga kwa mawe. Nao mashahidi wakaweka nguo zao miguuni pa kijana mmoja aliyeitwa Sauli Matendo 8:1a inasema “Na Sauli alikuwa akiona vema kwa kuuawa kwake”. Akitokea kabila ya Benyamini, Paulo alilelewa akiwa ni Muisraeli. Alikuwa ni wa madhehebu ya Mafarisayo. Wafilipi 3:4b-5 Mtu ye yote akijiona kuwa anayo sababu ya kuutumainia mwili, mimi zaidi. 5 Nalitahiriwa siku ya nane, ni mtu wa taifa la Israeli, wa kabila ya Benyamini, Mwebrania wa Waebrania, kwa habari ya kuishika torati, ni Farisayo, Paulo alifundishwa kazi ya utengenezaji wa wa mahema. Matendo 18:1-3 Baada ya mambo hayo, Paulo akatoka Athene akafika Korintho. 2 Akamwona Myahudi mmoja, jina lake Akila, mzalia wa Ponto; naye amekuja kutoka nchi ya Italia siku za karibu, pamoja na Prisila mkewe, kwa sababu Klaudio amewaamuru Wayahudi wote watoke Rumi, naye akafikilia kwao; 3 na kwa kuwa kazi yao ya ufundi ilikuwa moja, akakaa kwao, wakafanya kazi pamoja, kwa maana walikuwa mafundi wa kushona hema. Paulo alikuwa na uraia wa Taso ya Kilikia, na alisomea mjini Yerusalemu (Matendo 26:4). Matendo 22:3 Mimi ni mtu wa Kiyahudi, nalizaliwa Tarso, mji wa Kilikia, ila nililelewa katika mji huu, miguuni pa Gamalieli, nikafundishwa sheria ya baba zetu kwa usahihi, nikawa mtu wa jitihadi kwa Mungu kama ninyi nyote mlivyo leo hivi; (pia nsoma atendo 9:11; 21:39) Alikuwa na hati ya uraia wa Rumi pia. Matendo 22:25-27 Hata walipokwisha kumfunga kwa kamba, Paulo akamwambia yule akida aliyesimama karibu, Je! Ni halali ninyi kumpiga mtu aliye Mrumi naye hajakuhumiwa bado? 26 Yule akida aliposikia, akaenda akamwarifu yule jemadari, akisema, Unataka kufanya nini? Kwa maana mtu huyu ni Mrumi. 27 Jemadari akaja, akamwuliza, Niambie, u Mrumi? Akasema, Ndiyo. (sawa na inavyosema pia matendo 16:37) Pia alikuwa ni mwanachama wa Baraza la kidini la Wayahudi. Matendo 26:10 10 nami nikayafanya hayo Yerusalemu; niliwafunga wengi miongoni mwa watakatifu ndani ya magereza, nikiisha kupewa amri na wakuu wa makuhani; na walipouawa nalitoa idhini yangu. Paulo alilitesa na kulitawanya kanisa na wengi walitiwa gerezani. Matendo 8:1b,3 … Siku ile kukatukia adha kuu ya kanisa lililokuwa katika Yerusalemu; wote wakatawanyika katika nchi ya Uyahudi na Samaria, isipokuwa hao mitume. 2 Watu watauwa wakamzika Stefano, wakamfanyia maombolezo makuu. 3 Sauli akaliharibu kanisa, akiingia kila nyumba, na kuwaburuta wanaume na wanawake na kuwatupa gerezani. Matendo 9:1-2 Lakini Sauli, akizidi kutisha na kuwaza kuwaua wanafunzi wa Bwana, akamwendea Kuhani Mkuu, 2 akataka ampe barua za kuenda Dameski zilizoandikwa kwa masinagogi, ili akiona watu wa Njia hii, waume kwa wake, awafunge na kuwaleta Yerusalemu. Matendo 22:4-5 nikawaudhi watu wa Njia hii hata kuwaua, nikawafunga, nikiwatia gerezani, wanaume na wanawake. 5 Kama Kuhani Mkuu naye anishuhudiavyo, na wazee wa baraza wote pia, ambao nalipokea barua kwao kuwapelekea ndugu wale, nikaenda Dameski, ili niwalete wale waliokuwa huko hata Yerusalemu, hali wamefungwa, ili waadhibiwe. Paulo alikuwa mtu mwene bidii sana kwenye mapokeo ya dini ya Kiyahudi ambayo yalienezwa na dhehebu la Mafarisayo na ambalo Kristo alikuwa akilishutumu. Bilashaka hii ilikuwa ndiyo sababu kwa yeye kuwachukia Wakristo kwa kuwa dini hii ilikuwa inashutumu imani hii ya Mafarisayo hasa kuhusiana na mapokeo yaliyokanganya kwa kiasi kikubwa tafsiri halisi ya Kiroho la Torati ya Mungu. Wagalatia 1:14 Nami naliendelea katika dini ya Kiyahudi kuliko wengi walio hirimu zangu katika kabila yangu, nikajitahidi sana katika kuyashika mapokeo ya baba zangu. (sawapia na Wafilipi 3:5; Matendo 22:3; 23:6; 26:5) Kristo alikuwa na maneno haya ya kusema kuhusu mapokeo haya ya wazee ambayo yaliendelezwa na Waandishi na Mafarisayo kwa kusema: “Mbona ninyi nanyi huihalifu amri ya Mungu kwa ajili ya mapokeo yenu? Kwa kuwa Mungu alisema, Mheshimu baba yako na mama yako, na Amtukanaye baba yake au mama yake kufa na afe. Bali ninyi husema, Atakayemwambia babaye au mamaye, Cho chote kikupasacho kusaidiwa na mimi ni wakfu, basi asimheshimu baba yake au mama yake. Mkalitangua neno la Mungu kwa ajili ya mapokeo yenu. Enyi wanafiki, ni vema alivyotabiri Isaya kwa habari zenu, akisema, Watu hawa huniheshimu kwa midomo; Ila mioyo yao iko mbali nami. Nao waniabudu bure, Wakifundisha mafundisho Yaliyo maagizo ya wanadamu.” (Mathayo 15:3; Marko 7:6-7; Isaya 29:13). Mungu alisema kupitia nabii Isaya kwamba atayakomesha mapokeo haya. Paulo hakuwa ameelewa bado madhumuni au nia ya Mungu kupitia kwa Yesu Kristo na Kanisa. Kwa ajili hii, na makosa ya kimafundisho, alilitesa na kulidhulumu kanisa kinyume kabisa na maagizo ya Torati ya Mungu huku akidhani kwamba yu sahihi kwa mujibu wa Torati ya Mungu. Usemi na dhana ya kwamba “hakuwa na hatia kwa mujibu wa totati” kumtenga mbali kunaonyesha vilevile kwamba hakuwa anaelewa alikuwa anakiuka maagizo ya torati. Yeye ni kama Wayahudi wengi wengine leo ambao wanadhania na kujiona kuwa hawana hatia kwa mujibu wa torati lakini huku wakitenda dhambi na kumkana Kristo aliyewaokoa. Wakati alipoitwa aje kwenye utumishi, ndipo alipouelewa wito wake. Alijiona kuwa hakuwa na dhambi wala hatia chini ya torati lakini hatimaye akagungua kwamba alikuwa ameihalifu torati kwa kupitia mapokeo na akayachukia. Jambo hili aliliona na kulionyesha wazi kwenye mafundisho yake kwenye Warumi 3:9,10,19,20,23 na Wagalatia 3:10-12. Hata hivyo, kila ilipombidi Paulo alitumia mkazo wake kwa kutumia mapito yake ya Kifarisayo aliyoyapitia huko nyuma. Matendo 23:6 Paulo alipotambua ya kuwa sehemu moja ni Masadukayo, na sehemu ya pili ni Mafarisayo, akapaza sauti yake katika ile baraza, Ndugu zangu, mimi ni Farisayo mwana wa Farisayo; mimi ninahukumiwa kwa ajili ya tumaini la ufufuo wa wafu. Wongofu wa Paulo Wongofu wa Paulo haukuwa wa kuongoka kunakoeleweka kwa kuigeukia Torati na kuikiri ili kuanza kuishika na uiona umuhimu wake. Yeye alikuwa ni mtu anayeishika kwa bidii na moyo wake wote, pamoja na mapokeo yote, lakini alipaswa kuonyehswa uhusiano uliopo kati ya imani na sheria nah ii ilikuewa ndiyo sababu kuu ya kuandika na ndiyo hasa ujumbe au maana kuu ya maandiko au waraka kwa Wagalatia. Wongofu wake ulikuwa ni kwa ajili ya kujua mamlaka na maagizo makuu ya kiroho kwenye imani. Kusudi kuu na la kwanza na la mwisho la Sheria yote ya Mungu ulielekezwa kwenye Amri Kuu Mbili. Mathayo 22:37-39 Akamwambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote. 38 Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza. 39 Na ya pili yafanana nayo, nayo ni hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako. Paulo anaelewa lengo hili. Kusudi la huduma hii, na kwa hiyo ndiyo yetu, ilikuwa ni kuzihubiri amri hizo mbili zote kwa kuwa kama tutazishika hizo zote, hatutaweza kutenda dhambi na sheria ndipo haitatuhusu sisi. Kama hatutamwibia jirani yetu kwa kuhofia kutiwa mbaroni na kufungwa jela, bado tunakuwa wezi, lakini ni kwamba tu hatufanyi hivyo kimatendo. Bali kama tutampenda jiraji yetu, hatutaweza kufikiria kumuibia kwa kuwa hatutapenda kuwataabisha na kuwaona wakipata mateso. Kwa hiyo kama tutampenda jirani yetu, sheria inayohusu wizi, udanganyifu au usingiziaji, kutamani na kumfanyia maovu, nk, haitatuhusu tena kwa kuwa hazijaingia mawazoni wala aikilini mwetu. Na ndiyo maana ya usemi alioutoa wa “wamekufa kutokana na sheria”. Watu wengi wanapenda kujipa haki wanapovunja sheria wakisingia kwamba Paulo aliacha kushika sheria na wanawafundisha wengine wafanye hivyo. Watu hawa wanahatia ya makosa makubwa. Paulo na Sheria Matendo 20:5-16 inasema: Ila watu hao wamekwisha kutangulia wakamngojea Troa. 6 Sisi tukatweka baada ya siku za mikate isiyotiwa chachu, tukatoka Filipi, tukawafikia Troa, safari ya siku tano, tukakaa huko siku saba. 7 Hata siku ya kwanza ya juma, tulipokuwa tumekutana ili kumega mkate, Paulo akawahutubu, akiazimu kusafiri siku ya pili yake, naye akafuliza maneno yake hata usiku wa manane. 8 Palikuwa na taa nyingi katika orofa ile tulipokuwa tumekusanyika. 9 Kijana mmoja, jina lake Eutiko, alikuwa ameketi dirishani, akalemewa na usingizi sana; hata Paulo alipoendelea sana kuhubiri, akazidiwa na usingizi wake akaanguka toka orofa ya tatu; akainuliwa amekwisha kufa. 10 Paulo akashuka, akamwangukia, akamkumbatia, akasema, Msifanye ghasia, maana uzima wake ungalimo ndani yake. 11 Akapanda juu tena, akamega mkate, akala, akazidi kuongea nao hata alfajiri, ndipo akaenda zake. 12 Wakamleta yule kijana, yu mzima, wakafarijika faraja kubwa sana. 13 Lakini sisi tukatangulia kwenda merikebuni, tukaabiri kwenda Aso, tukikusudia kumpakia Paulo huko; kwa maana ndivyo alivyoagiza, yeye mwenyewe aliazimu kwenda kwa miguu. 14 Alipotufikia huko Aso, tukampakia, kisha tukafika Mitilene.15 Tukatweka kutoka huko, na siku ya pili tukafika mahali panapokabili Kio; siku ya tatu tukawasili Samo, tukakaa Trogilio, siku ya nne tukafika Mileto. 16 Kwa sababu Paulo amekusudia kupita Efeso merikebuni, asije akakawia katika Asia; kwa maana alikuwa na haraka, akitaka kuwahi Yerusalemu siku ya Pentekoste, kama ikiwezekana. Hapa tunamuona Paulo na wenzake wakiadhimisha Sikukuu ya Mikate Isiyo na Chachu kisha akasariri akirudi Yerusalemu ili akaishike Sikukuu ya Pentekoste huko. Hii ilikuwa safari ya kupendeza kwa mtu anayenenewa kuwa amefundisha kuiondoa sheria! Wapinzani wa Paulo wanatafuta kutumia andiko hili kuonyesha kwamba Paulo alikuwa anaabudu siku ya Jumapili, lakini yana maana gani hasa maandiko haya? Tafsiri ya Biblia ya King James inasema kwene Matendo 20:7 hivi: Hata siku ya kwanza ya juma, tulipokuwa tumekutana ili kumega mkate, Paulo akawahutubu, akiazimu kusafiri siku ya pili yake, naye akafuliza maneno yake hata usiku wa manane. Toleo hili liliaandikwa ili kuonyesha kwamba hili lilikuwa na uhusiano mkutaniko wa kanisa na kwamba Paulo alikuwa anahubiri na kwamba uke umegaji wa mkate ulikuwa ni ibada ya ushirika wa komunio takatifu. Hata hivyo, neno linalotumika hapa kuelezea kuhubiri ni neno la Kiyunani mjadala au majadiliano linalomaanisha pia majadiliano yanayoendana na kujibu maswali kati ya watu wawili au zaidi katika kuwafundisha na kujibu maswali yao. Usemi uliotumika kuelezea kuwa waliumega mkate ulimaanisha tendo la kula chakula cha kawaida tu. Neno lililotumika kuelezea juma au wiki ni sabbaton ambayo inaweza kuwa siku nyingine yoyote ndani ya kipindi hiki cha siku saba. Kwa hiyo, ni kwamba Paulo alikula nao chakula siku ya Jumapili jioni akiwa pamoja na wanafunzi wake na mazungumzo yao yaliendelea hadi usiku wa manane, kwa kuwa alikuwa anaondoka asubuhi iliyfuatia. Watu wanajaribu kudai kwamba kwakuwa Paulo hakuwalazimisha waongofu wapya kutahiriwa, basi alihubiri akipinga tohara na sheria pia; lakini je, Paulo anasemaje kuhusu madai yao hayo? Matendo 21:17-26 Tulipofika Yerusalemu wale ndugu wakatukaribisha kwa furaha. 18 Hata siku ya pili yake Paulo akaingia kwa Yakobo pamoja nasi, na wazee wote walikuwako. 19 Na baada ya kuwaamkua, akawaeleza mambo yote moja moja Mungu aliyoyatenda katika Mataifa kwa huduma yake. 20 Nao waliposikia wakamtukuza Mungu, wakamwambia, Ndugu yetu, unaona jinsi Wayahudi walioamini walivyo elfu nyingi, nao wote wana wivu sana kwa ajili ya torati. 21 Nao wameambiwa habari zako, ya kwamba unawafundisha Wayahudi wote wakaao katika Mataifa kumwacha Musa, ukiwaambia wasiwatahiri watoto wao, wala wasizifuate desturi. 22 Basi, ni nini? Bila shaka watasikia kwamba umekuja. 23 Basi fanya neno hili tunalokuambia. Wako kwetu watu wanne waliofungwa na nadhiri. 24 Wachukue watu hao, ujitakase pamoja nao, na kuwagharimia ili wanyoe vichwa vyao, watu wote wapate kujua ya kuwa habari zile walizoambiwa juu yako si kitu, bali wewe mwenyewe unaenenda vizuri na kuishika torati. 25 Lakini kwa habari za watu wa Mataifa walioamini, tuliandika na kutoa hukumu yetu ya wao kujilinda nafsi zao na vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na damu, na kitu kilichosongolewa, na uasherati. 26 Ndipo Paulo akawatwaa wanaume wale, na siku ya pili yake akajitakasa nafsi yake pamoja nao, akaingia ndani ya hekalu, akitangaza habari ya kutimiza siku za utakaso, hata sadaka itolewe kwa ajili ya kila mmoja wao. Tulipofika Yerusalemu wale ndugu wakatukaribisha kwa furaha. 18 Hata siku ya pili yake Paulo akaingia kwa Yakobo pamoja nasi, na wazee wote walikuwako. 19 Na baada ya kuwaamkua, akawaeleza mambo yote moja moja Mungu aliyoyatenda katika Mataifa kwa huduma yake. 20 Nao waliposikia wakamtukuza Mungu, wakamwambia, Ndugu yetu, unaona jinsi Wayahudi walioamini walivyo elfu nyingi, nao wote wana wivu sana kwa ajili ya torati. 21 Nao wameambiwa habari zako, ya kwamba unawafundisha Wayahudi wote wakaao katika Mataifa kumwacha Musa, ukiwaambia wasiwatahiri watoto wao, wala wasizifuate desturi. 22 Basi, ni nini? Bila shaka watasikia kwamba umekuja. 23 Basi fanya neno hili tunalokuambia. Wako kwetu watu wanne waliofungwa na nadhiri. 24 Wachukue watu hao, ujitakase pamoja nao, na kuwagharimia ili wanyoe vichwa vyao, watu wote wapate kujua ya kuwa habari zile walizoambiwa juu yako si kitu, bali wewe mwenyewe unaenenda vizuri na kuishika torati. 25 Lakini kwa habari za watu wa Mataifa walioamini, tuliandika na kutoa hukumu yetu ya wao kujilinda nafsi zao na vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na damu, na kitu kilichosongolewa, na uasherati. 26 Ndipo Paulo akawatwaa wanaume wale, na siku ya pili yake akajitakasa nafsi yake pamoja nao, akaingia ndani ya hekalu, akitangaza habari ya kutimiza siku za utakaso, hata sadaka itolewe kwa ajili ya kila mmoja wao. Hapa tunamuona Yakobo, ndugu wa kuzaliwa na Kristo, pamoja na Wazee, waliomba kwamba Paulo afanye utakaso Hekaluni kwa mujibu wa Torati ili awathibitishie Wayahudi kwamba bado yungali anashika Torati. Habari na tukio hili ni mojawapo ya ushahidi mkubwa na wenye nguvu unaoonyesha mwendelezo wa ushikaji wa sheria kwenye Agano Jipya. Kanisa halikuachwa huru kutoka kwenye umuhimu wa kuzishika na kuzitii sheria kwa kifo cha Kristo, bali ni ile tu kanuni ya utoaji dhabihu za wanyama ndiyo ilitimilizwa nay eye. Ishara ya Yona ilikuwa bado inatenda kazi au inaelea kwa miaka 40 tangu Yohana Mbatizaji na kwene huduma ya Kristo na iliishia pale Hekalu lilipobomoshwa kwa ajili ya kuasi kwao Yuda na kushindwa kwao kufanya toba kwa dhambi waliyoifanya kwa kuendelea kwao kuivunja na kuitia unajisi torati kwa ajili ya kuyatukuza mapokeo yao baada ya miaka 40 ya neema waliyopewa. Utaratibu wa Hekalu katika Yuda ulikoma kwa kuangamizwa kwake Hekalu mwaka 70 BK. Kristo alisema kwenye Mathayo16:4: Kizazi kibaya na cha zinaa chataka ishara; wala hakitapewa ishara, isipokuwa ishara ya Yona. Akawaacha, akaenda zake. Tunajua kwamba kazi ya Yona huko Ninawi iligharimu safari ya siku moja (huduma ya Yohana Mbatizaji ilifanyika kwa mwaka mmoja) na siku mbili akhubiri (huduma ya Kristo ya miaka miwili) na siku 40 za kutubu (mwaka wa 30 BK hadi 70 BK) wakati utoaji wa dhabihu za wanyama ulipokoma. Unabii wa Danieli kuhusu juma la 70 la miaka na uelekeo wa Kristo na kuashiria kwake kwenye Ishara ya Yona haukukoma hadi kuhusuriwa kwa Hekalu, kwa hiyo utaratibu ule haukuhukumiwa hadi kipindi cha neema (miaka 40) kilipowasili (soma jarida la Ishara ya Yona na Historia ya Ujenzi Mpya wa Hekalu (Na. 013) [The Sign of Jonah and the History of the Reconstruction of the Temple (No. 013)]. Wayahudi walikuwa wanawahukumu watakatifu kwa alama onekevu kama vile tohara, ns Paulo mara moja anasema hivi: “Kama tohara inatosha, basi hatuna haja ya kuwa na Kristo”. Je, Paulo alikuwa anamaanisha kwamba tohara ilikiwa ni lazima au haina maana kuifanya? Hapana. Basi alisema tu kwamba watu wa mataifa walioitwa na kuongoka wakiwa watu wazima haikuwa lazima kwao kutahiriwa ila watoto wao waliozaliwa baada ya kuongoka kwao walipaswa kutahiriwa kama inavyoagiza torati, na ndivyo walivyofanya. Soma pia jarida la Utakaso na Tohara (Na. 251) [Purification and Circumcision (No. 251)]. Harakati za Yakobo Hekaluni zikukuwa sahihi na zilifuata mahudhui yote ya torati. Paulo alikuwa chini ya maelekezo ya baraza kuishika Toraati ya Mungu kwa mujibu wa sura na aya. (Matendo 21:17-40) kwenye Matendo 21:24 mitume (na hasa Yakobo) walimwambia awachukue wanaume wane kisha ajifanyie utakaso pamoja nao na awalipie gharama ili wanyoe vichwa vyao (kwa maneno mengine wakamilishe au kutimiza nadhiri zao kwa mujibu wa torati, kama Paulo alivyotakiwa kukamilisha nadhiri zake alizoziweka alipokuwa Senkrae (sawa na inavyosema Matendo 18:18)). Kwa nini ilikuwa hivi? “Watu wote wapate kujua ya kuwa habari zile walizoambiwa juu yako si kitu, bali wewe mwenyewe unaenenda vizuri na kuishika Torati.” (RSV) (pia tazama KJV: neno Shika Sheria au Torati). Mchakato wote huu ulihesabiwa kuwa anahaki na kustahili na Kristo kutoka Matendo 23:11 ambapo inasema: Usiku ule Bwana akasimama karibu naye, akasema, Uwe na moyo mkuu; kwa sababu, kama ulivyonishuhudia habari zangu Yerusalemu, imekupasa kunishuhudia vivyo hivyo Rumi nako. Kwa mtu anayenenwa na kutolewa hoja ya kwamba ameiondoa sheria, anaonekana kwa kina sana mwenyewe akiishika.
KUREJEZWA KATIKA IMANI " Ndugu zangu, mtu akighafilika katika kosa lolote, ninyi mlio wa Roho mrejezeni upya mtu kama huyo kwa roho ya upole, ukijiangalia nafsi yako usije ukajaribiwa wewe mwenyewe."Wagalati 6:1 (1) Kosa lolote Kosa lolote maana yake kosa lolote! Mtu akighafilika njia ya kufanya kwa wale walio wa Roho tu tunatakiwa kumrejeza upya katika imani, upya katika kosa husika na hatuambiwi sasa tuanze kusema na kuanza kumtangaza ovyo, "tulijua tu, yule kwa mwendo ule asingeweza kufika mbali..." Hayo hayatarajiwi kufanywa na kuzungumzwa kwa "Walio wa Roho" hayo yatafanywa kwa wasio wa Roho maana ndio kinyume cha andiko hilo! Wasio/Walio wa Roho sio watu wa dhehebu fulani, ni mtu yeyote yule. Katika andiko hilo haitajwi mtu ambaye hajawahi kukutana na Yesu! Hapo anatajwa mtu ambaye alikuwa katika imani na sasa amekengeuka ndio maana maandiko yanasema "Tunatakiwa kumrejeza upya.." Anayerejezwa ni mtu ambaye alikuwa katika mstari na sasa ametoka nje ya mstari, anatakiwa kurejezwa! Wako watu wanaweza wakawepo makanisani lakini hawajawahi kukutana na Yesu, hawajahi kuokoka, wapo kwa sababu zao au kwa kufuata wazazi n.k. Hao andiko hili si la kwao! Andiko hili ni la mtu aliyekuwa katika njia salama na sasa hayupo amekengeuka huyo ndiye tunaagizwa kwa ajili yake, kumrejeza. Ni vema tufanye hivyo! Tuache habari ya kukaa kaa na kuanza kumsengenya mtu, kama unajua mtu ameghafirika katika hilo unalolijua, tunatakiwa kumrejeza tena kwa roho ya upole na sio kujifanya sisi kama sasa ndio tumepatia pakusemea mambo yetu ya moyoni ya muda mrefu! Unamwambia mtu ambaye hata kuomba haombi, atasaidia nini huyo zaidi ya kusengenya tu. Aliyeghafilika muombee na huku ukijitahidi kumrejeza tena kwa roho ya upole kwa sababu kauli nazo zinaweza kumfanya mtu kuwa mbali zaidi! Lazima tuwe na kauli nzuri tunapotaka kumrejeza mtu! (2) Ukijiangalia nafsi yako Hapa tunaona katika maneno ya mwisho inasema "ukijiangalia nafsi yako usije ukajaribiwa wewe mwenyewe.." Pamoja na maagizo ya upendo ya kuwarejeza watu walioghafilika! Kuna tahadhari tunapewa! Tukiziangalia nafsi zetu tusije tukajaribiwa wenyewe; ako baadhi ya watu wanaruka la kwanza wanalifuata la pili! Hiyo haipo! Yaani wanadai wanaziangalia nafafsi zao kabla ya kujaribu kufanya la kwanza la kuwarejeza. Tunayakiwa kujiangalia nafsi zetu wakati tunafanya kazi ya kumrejeza aliyeghafilika! Hayo ni mapacha! Tunajiangalia nafsi zetu kwa maombi na umakini wa hali ya juu! Ili usije kujikuta unamvuta mtu kutoka shimoni kwa kamba, badala ya wewe kumvuta unavutwa wewe na kujikuta tumedumbukia shimoni sisi na kamba zetu! Hapo inakuwa hatari maana wote mkiwa shimoni huko mtatiana moyo chini kwa chini! Ndugu zangu nawasihi sana! Ikiwa unajua mtu yeyote ameghafilika! Tusimuache kwa kusema "kila mmoja atalibeba furushi lake mwenye". Tuseme hayo baada ya kushindwa kumrejeza kwa jitihada zetu zote, ni kama tunahitimisha kazi yetu lakini tusiseme hayo tukiwa hatujafanya chochote kumhusu aliyeghafilika! Tuko hivi wakati mwingine ni kwa neema ya Mungu tu, pamoja na jitihada zetu, lakini ni kwa neema ya Mungu pia! Angalia maisha yako! Maombi binafsi ni shida, lakini kinachotuufanya tusitetereke ni nini basi wakati maombi ni silaha yetu lakini hatuombi inavyotupasa? Tunaomba mpaka tukiwa kanisani tu au jumapili? Wako watu walikuwa waombaji lakini wamerudi nyuma, wako watu walikuwa na misimamo ya hatari lakini wamerudi nyuma! Uwokovu ni safari ndefu sana! Ikitokea mwenzetu ameshambuliwa tumsaidie kadiri inavyowezekana, na kama tukishindwa basi tushindwe pia na kumzungumzia ovyo yaani tushindwe yote! " BWANA nikumbuke mimi Marco Bashiri katika Ufalme wako, na kama unajua nitarudi nyuma! BWANA naomba ombi hili lipate kibali mbele zako! Uitoe roho yangu nisiendelee kuishi maana nitalitukanisha jina lako sana BWANA! Ni heri uniingize katika ufalme wako kabla ya wakati wangu" " Ndugu zangu, mtu akighafilika katika kosa lolote, ninyi mlio wa Roho mrejezeni upya mtu kama huyo kwa roho ya upole, ukijiangalia nafsi yako usije ukajaribiwa wewe mwenyewe."Wagalati 6:1 #MTUWAVITA