MAMBO KUMI YANAYOWEZA KUWACHELEWESHA WACHUMBA KUFUNGA NDOA. Bwana YESU
KRISTO
-
Na Peter & Jemimah Mabula Watendakazi katika Shamba la MUNGU wa
Mbinguni Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu zangu wote.Karibu upate maarifa
ya kukusaidia kat...
Thursday, 3 November 2016
KUREJEZWA KATIKA IMANI
" Ndugu zangu, mtu akighafilika katika kosa lolote, ninyi mlio wa Roho mrejezeni upya mtu kama huyo kwa roho ya upole, ukijiangalia nafsi yako usije ukajaribiwa wewe mwenyewe."Wagalati 6:1
(1) Kosa lolote
Kosa lolote maana yake kosa lolote! Mtu akighafilika njia ya kufanya kwa wale walio wa Roho tu tunatakiwa kumrejeza upya katika imani, upya katika kosa husika na hatuambiwi sasa tuanze kusema na kuanza kumtangaza ovyo, "tulijua tu, yule kwa mwendo ule asingeweza kufika mbali..."
Hayo hayatarajiwi kufanywa na kuzungumzwa kwa "Walio wa Roho" hayo yatafanywa kwa wasio wa Roho maana ndio kinyume cha andiko hilo! Wasio/Walio wa Roho sio watu wa dhehebu fulani, ni mtu yeyote yule.
Katika andiko hilo haitajwi mtu ambaye hajawahi kukutana na Yesu! Hapo anatajwa mtu ambaye alikuwa katika imani na sasa amekengeuka ndio maana maandiko yanasema "Tunatakiwa kumrejeza upya.." Anayerejezwa ni mtu ambaye alikuwa katika mstari na sasa ametoka nje ya mstari, anatakiwa kurejezwa!
Wako watu wanaweza wakawepo makanisani lakini hawajawahi kukutana na Yesu, hawajahi kuokoka, wapo kwa sababu zao au kwa kufuata wazazi n.k. Hao andiko hili si la kwao! Andiko hili ni la mtu aliyekuwa katika njia salama na sasa hayupo amekengeuka huyo ndiye tunaagizwa kwa ajili yake, kumrejeza.
Ni vema tufanye hivyo! Tuache habari ya kukaa kaa na kuanza kumsengenya mtu, kama unajua mtu ameghafirika katika hilo unalolijua, tunatakiwa kumrejeza tena kwa roho ya upole na sio kujifanya sisi kama sasa ndio tumepatia pakusemea mambo yetu ya moyoni ya muda mrefu! Unamwambia mtu ambaye hata kuomba haombi, atasaidia nini huyo zaidi ya kusengenya tu. Aliyeghafilika muombee na huku ukijitahidi kumrejeza tena kwa roho ya upole kwa sababu kauli nazo zinaweza kumfanya mtu kuwa mbali zaidi! Lazima tuwe na kauli nzuri tunapotaka kumrejeza mtu!
(2) Ukijiangalia nafsi yako
Hapa tunaona katika maneno ya mwisho inasema "ukijiangalia nafsi yako usije ukajaribiwa wewe mwenyewe.."
Pamoja na maagizo ya upendo ya kuwarejeza watu walioghafilika! Kuna tahadhari tunapewa! Tukiziangalia nafsi zetu tusije tukajaribiwa wenyewe; ako baadhi ya watu wanaruka la kwanza wanalifuata la pili! Hiyo haipo! Yaani wanadai wanaziangalia nafafsi zao kabla ya kujaribu kufanya la kwanza la kuwarejeza. Tunayakiwa kujiangalia nafsi zetu wakati tunafanya kazi ya kumrejeza aliyeghafilika! Hayo ni mapacha! Tunajiangalia nafsi zetu kwa maombi na umakini wa hali ya juu! Ili usije kujikuta unamvuta mtu kutoka shimoni kwa kamba, badala ya wewe kumvuta unavutwa wewe na kujikuta tumedumbukia shimoni sisi na kamba zetu! Hapo inakuwa hatari maana wote mkiwa shimoni huko mtatiana moyo chini kwa chini!
Ndugu zangu nawasihi sana! Ikiwa unajua mtu yeyote ameghafilika! Tusimuache kwa kusema "kila mmoja atalibeba furushi lake mwenye". Tuseme hayo baada ya kushindwa kumrejeza kwa jitihada zetu zote, ni kama tunahitimisha kazi yetu lakini tusiseme hayo tukiwa hatujafanya chochote kumhusu aliyeghafilika!
Tuko hivi wakati mwingine ni kwa neema ya Mungu tu, pamoja na jitihada zetu, lakini ni kwa neema ya Mungu pia! Angalia maisha yako! Maombi binafsi ni shida, lakini kinachotuufanya tusitetereke ni nini basi wakati maombi ni silaha yetu lakini hatuombi inavyotupasa? Tunaomba mpaka tukiwa kanisani tu au jumapili? Wako watu walikuwa waombaji lakini wamerudi nyuma, wako watu walikuwa na misimamo ya hatari lakini wamerudi nyuma!
Uwokovu ni safari ndefu sana! Ikitokea mwenzetu ameshambuliwa tumsaidie kadiri inavyowezekana, na kama tukishindwa basi tushindwe pia na kumzungumzia ovyo yaani tushindwe yote!
" BWANA nikumbuke mimi Marco Bashiri katika Ufalme wako, na kama unajua nitarudi nyuma! BWANA naomba ombi hili lipate kibali mbele zako! Uitoe roho yangu nisiendelee kuishi maana nitalitukanisha jina lako sana BWANA! Ni heri uniingize katika ufalme wako kabla ya wakati wangu"
" Ndugu zangu, mtu akighafilika katika kosa lolote, ninyi mlio wa Roho mrejezeni upya mtu kama huyo kwa roho ya upole, ukijiangalia nafsi yako usije ukajaribiwa wewe mwenyewe."Wagalati 6:1
#MTUWAVITA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment