MAMBO KUMI YANAYOWEZA KUWACHELEWESHA WACHUMBA KUFUNGA NDOA. Bwana YESU
KRISTO
-
Na Peter & Jemimah Mabula Watendakazi katika Shamba la MUNGU wa
Mbinguni Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu zangu wote.Karibu upate maarifa
ya kukusaidia kat...
Thursday, 3 November 2016
MAISHA YA WOKOVU, MTUME PAULO
Pasaka/Mikate Isiyo na Chachu
Kristo aliishika Idi au Sikukuu ya Mikate Isiyo na Chachu, sawa na Paulo na wengine, kwa hiyo na sisi tunapaswa kuishika.
Matendo 12:3
Na akiona ya kuwa imewapendeza Wayahudi akaendelea akamshika na Petro. Siku hizo zilikuwa siku za mikate isiyochachwa.
Matendo 20:6
Sisi tukatweka baada ya siku za mikate isiyotiwa chachu, tukatoka Filipi, tukawafikia Troa, safari ya siku tano, tukakaa huko siku saba.
1Wakorintho 5:8
basi na tuifanye karamu, si kwa chachu ya kale, wala kwa chachu ya uovu na ubaya, bali kwa yasiyochachika, ndio weupe wa moyo na kweli.
Miandamo ya Mwezi
Wakolosai 2:16
Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato;
Kwa suala la Mwandamo wa Mwezi, hapa tunamuona Paulo akiwaambia wamataifa wasione haya kushika na kuadhimisha zile zilizokuwa zinajulikana kama Sikukuu za Wayahudi ambazo sasa ni zao pia. Kristo alitilia maanani Miandamo ya Mwezi na kuichukulia kama jambo muhimu, kwa kuwa kama Paulo angeenda kinyue na kupingana na Kristo na Paulo akaishika Miandamo ya Mwezi inaonyesha kuwa Kristo alifanya hivyo pia. Aliziishika sheria na Sikukuu, na Miandamo ya Mwezi na ziliadhimishwa kwa uaminifu mkubwa kwenye imani au dini ya Kiyahudi hadi kuangamizwa kwa Hekalu, na Kristo alikuwa ni Mfalme na ni Kuhani Mkuu aliyewekwa asiye na dhambi. Kuidai na kuamini kuwa andiko hili limeondoa umuhimu wa kuziadhimisha Sabato, Miandamo ya Mwezi na Sikukuu zilizoamriwa ni kutumia vibaya kabisa matumizi ya lugha zote mbili, yaani Kyunani ya Kiingereza.
Sikukuu ya Vibanda
Yohana 7:2
Na sikukuu ya Wayahudi, Sikukuu ya Vibanda, ilikuwa karibu.
Kama Kristo alivyoishika Sikuuu ya Vibanda, ndivyo pia Paulo alivyofanya na ndivyo hata sisi tunavyotakiwa kufanya.
Matendo 18:18-21
Baada ya hayo Paulo akazidi kukaa huko siku nyingi, kisha akaagana na ndugu akaabiri kwenda Shamu; na Prisila na Akila wakaenda pamoja naye, alipokwisha kunyoa kichwa chake huko Kenkrea; maana alikuwa ana nadhiri. 19 Wakafika Efeso, akawaacha huko. Yeye mwenyewe akaingia katika sinagogi, akahojiana na Wayahudi. 20 Walipomtaka akae wakati mwingi zaidi, hakukubali; 21 bali aliagana nao, akisema, Nitarejea kwenu tena, Mungu akinijalia. Akatweka, akatoka Efeso,
Hii ni nadhiri ambayo inapaswa ikamilike huko Yerusalemu wakati alipokwenda huko kama tunavyoona hapo juu.
Kwa kuwa wasomaji wengi wa Injili ya Yohana walikuwa sio Wayahudi, ilikuwa muhimu kutumia neno “Wayahudi” katika kuitja sikukuu hii kama Sikukuu ya Vibanda ya Wayahudi (Yohana 7:2). Matendo na mwenendo wa Kristo unaonyesha kutilia kwake umuhimu utunzaji wa Sikukuu, kama alivyo waambia na kuwasisitiza watu wa familia yake waende kuishika kwenye Yohana 7:8, na aya ya 10 tunaona kwamba yeye mwenyewe pia alikwenda kuishika Sikukuu hii. Ingawaje viongozi wa dini wa wakati ule walitafuta kumuua, hii haikumzuia Kristo kwenda kuishika na kuingia hadi ndani ya Hekalu ambako alikuwa anafundisha pia (Yohana 7:14). Ukweli huu unatuacha sisi tukwa hatuna udhuru wowote wa kutoishika au kuadhimisha siku hizi za muhimu.
Sikukuu ambayo Paulo alikuwa anaitaja inaweza kuwa ilikuwa ni Sikukuu ya Vibanda tu. Kupangilia upya kwa ratiba ya safari ya Paulo unaonyesha kuwa alikuwa makini kuiadhimisha. Alifika huko Korintho (Matendo 18:1) na akakaa nyumbani kwa Yusto kwa miezi 18 (Matendo 18:11). Ksha akasafiri hadi Yerusalemu, ambako aliwasili majira ya kipupwe ya mwaka 52-53 BK. Paulo kwa wazi anaona hitaji na umuhimu wa kuitunza Sikukuu ya Vibanda mjini Yerusalemu, ambako ndiko yalikuwa makao makuu ya Kanisa kwa wakati ule.
Upatanisho
Matendo 27:9
Na wakati mwingi ulipokwisha kupita, na safari ikiwa ina hatari sasa, kwa sababu siku za kufunga zilikuwa zimekwisha kupita, Paulo akawaonya,
Bullinger anasema kwenye ufafanuzi wake kuhusu aya ya 9 juu ya mfungu huu wa saumu kuwa ulifanyika siku ya kumi ya mwezi wa saba, ambayo ni Siku ya Upatanisho. Anadhani kuwa ilikuwa ni tarehe 1 Oktoba ya mwaka ule (Companion Bible).
I wazi kabisa kwamba Paulo alishika sheria ama torati kama alivyofanya Kristo. Tunajua kwamba Torati haikutanguliwa na yeyote kwa kuwa Kristo anasema kwenye Mathayo 5:17-18 kwamba:
Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza. 18 Kwa maana, amin, nawaambia ,Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka,yodi moja wala nukta moja ya torati haitaoondoka ,hata yote yatimie.
Ufunuo 22:6
Kisha akaniambia, Maneno haya ni amini na kweli. Naye Bwana, Mungu wa roho za manabii, alimtuma malaika wake kuwaonyesha watumwa wake mambo ambayo hayana budi kuwako upesi.
Hadi matukio haya yalipokuwa yanatimilika yote yalikuwa hayajatimilika
Dhambi ni uasi na uvunjaji wa sheria (1Yohana 3:4). Kama Paulo hakushika sheria, basi alikuwa akitenda dhambi. Na iwapo kama alizivunja sheria kwa kiufanya mambo aliyokuwa anayafanya Kristo, basi tutasema kuwa Kristo alikuwa anafanya dhambi pia. Lawama atakayopewa Paulo kwa kuishika kwake sheria ni lawama ya kumshambulia Kristo pia.
Ni nani hawa watakatifu wa Mungu? Hawa ni wale wanaoishika sheria au Amri za Mungu na ushuhuda wa Yesu Kristo (Ufunuo 12:17; 14:12).
Na ni lini ilitimilika? Utimilifu wa Ufufuo wa wafu na Hukumu na kushuka kwa Mji wa Mungu ndiko kukamilika kwa mpango au mchakato huu na kufanya mwisho na hitimisho kuukomesha uasi na kuwaleta viumbe wote kwa Mungu, mbingu na dunia havitapita na sheria itasimama. Tuna kazi nginyine mbele yetu ambayo itagharimu maisha yetu na imani kuendelea katika sheria au Torati ya Mungu kama zilivyotolewa kutoka asili yake ambayo tutairithi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment