IMANI YA MTU NDIPO ITAKAPOINEKANA
Wakristo Wanaokufa kwa ajili ya Imani Mpinga Kristo atawatesa
wakati huu wa dhiki kuu.
Wakristo ambao watakuwa hawafuati mambo yake.
Hawatatii amri zake ila watendelea kuomba Mungu wa kweli wa taifa la Israeli
kupitia Masihi Yesu kristo.
Kwa ajili hii, wakristo watakuwa na uhusiano wa karibu na mwanamke Israeli
Ufu. 12:17.
Katika
Warumi 11:15-20.
Paulo anasema wakristo kutoka mataifa yasiyo ya kiyahudi wamefanywa kuwa sehemu ya mti wa mzeituni kwa hivyo,
wana uhusiano wa karibu sana nao.
Uhusiano huu ndio msingi wa mapenzi tuliyonayo
kwa watu wa taifa la Israeli.
Ombi letu ni kwamba wayahudi kutoka taifa la Israeli nao pia watamtambua Kristo kuwa mwokozi na kuingia katika mapatano naye
Heb. 8: 8-13.
Wakristo wa kweli watatambua mara moja
kwamba mpinga Kristo ni kiongozi wa uwongo.
Wao watamkataa,
pia watakataa kanisa lile la dunia atakaloanzisha.
Kwao, katika milki hii ya mnyama (the beast),
kuna njia moja tuu, nayo ni ile ya mateso na kufa kwa ajili ya Imani.
Kuhusu hawa watakaokufa kwa ajili ya imani yao,
Yohana anasema hivi:
"Na alipoifungua muhuri ya tano, nikaona chini ya madhabahu roho zao waliochinjwa kwa ajili ya neno la Mungu,
na kwa ajili ya ushuhuda waliokuwa nao.
Wakalia kwa sauti kuu,
wakisema, Ee Mola, Mtakatifu, Mwenye kweli, hata lini kutohukumu, wala kuipatia haki damu yetu kwa hao wakaao juu ya nchi?"
Ufu. 6:9-10.
Kati ya hawa watakaokufa kwa ajili ya imani,
watakuwa wale ambao wamekubali wokovu baada ya huduma kanisani kupitia kazi ya wayahudi 144,000, kutakuwa na wakristo kama hawa wengi.
Wao watajitoa kumpinga Kristo, na kuichua uongo wake.
Ikiwa wakati huu utakupata, jua kwamba wokovu wako hautahusika na kumpinga muovu,
na kukataa chapa yake, lakii haya yote yatategemea sana kumkubali Kristo.
Lazima utubu dhambi zako, mkubali Kristo awe Bwana wa maisha yako, na usafishwe na damu yake.
Ni kupitia haya utakuwa umejiandaa vyema
kumpinga huyu muovu, hata kama msimamo wako huu wa upinzani waweza kukufanya upoteze maisha yako.
Lazima uwe tayari kufa kwa ajili ya imani yako. Sababu ni kwamba waKristo hawatapona dhiki kuu:
"Nao wakapewa kila mmoja nguo ndefu, nyeupe,
wakaambiwa wastarehe bado mda mchache, hata itakapotimia hesabu ya wajoli wao na ndugu zao, watakaouawa vile vile kama wao"
(Ufu. 6:11).
Watakapofika mbinguni, hawa waliokufa kwa ajili ya imani yao watapewa mwili wa kufufuka,
nao watakuwa na furaha kuu pamoja na Mungu.
Hawatakumbuka shida na machozi ya mateso, njaa, na vifo kwa ajili ya imani. Kuhusu watakaofufuka,
Yohana anasema:
"Baada ya hayo nikaona, na tazama, mkutano mkubwa sana ambao hapana mtu awezaye kuuhesabu,
watu wa kila taifa, na kabila na jamaa, na
lugha wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi, na mbele ya mwana kondoo wamevikwa mavazi meupe, wana matawi ya mitende
mikononi mwao…
Nikamwambia, Bwana wangu, wajua wewe.
Akaniambia, hao ndio wanatoka katika dhiki ile iliyo kuu, nao wamefua mavazi yao,
na kuyafanya meupe katika damu ya mwanakondoo…
Kwa maana huyo Mwana kondoo,
aliye katikati ya kiti cha enzi, atawachunga,
naye atawaongoza kwenye chemi chemi za maji yenye uhai,
na Mungu atayafuta machozi yote katika macho yao"
Ufu. 7: 9, 14, 17.
Mkutano katika Mlima wa Mizeituni Kristo ataonekana mara ya pili hapa duniani
jinsi vile imeelezwa katika Ufu 19, na hii itakuwa pale katika mlima wa mizeituni.
Twasoma:
"Na siku hiyo miguu yake itasimama juu ya mlima wa mizeituni, unaoelekea Yerusalemu upande wa mashariki, nao mlima wa mizeituni,
unaoelekea Yerusalemu upande wa mashariki,
nao mlima wa mizeituni utapasuka katikati yake, upande wa mashariki na upande wa magharibi;
litakuwako huko bonde kubwa sana; nusu ya mlima ule utaondoka kwenda upande wa kaskazini,
na nusu yake itaondoka kwenda upande wa kusini.
Nanyi mtakimbia kwa njia ya bonde la milima yangu;
kwa maana bonde lile la milima litaenea hata Aseli;
naam, mtakimbia, kama vile mlivyokimbia mbele ya tetemeko la nchi, siku za Uzia,
mfalme wa Yuda; na Bwana, Mungu wangu, atakuja, na watakatifu wote pamoja naye"
Zek. 14:4-5.
Mwokozi wetu Kristo atakuja tena pamoja na watakatifu ambao walikuwa wameungana naye kwa muda wa miaka saba iliotangulia.
Sasa anakuja kuleta makubaliano (reconciled) na wale waliobaki taifa la Israeli
ambao wakati wa vita vya Har-Magedoni,
walikimbilia usalama katika sehemu zilizo na mawe kwenye mlima wa mizeituni.
Mkutano huu utakuwa kwa ajili ya kuwapa wokovu.
"Katika siku hiyo watu wa nyumba ya Daudi,
na wenyeji wa Yerusalemu, watafunguliwa chemchemi kwa dhambi na kwa unajisi"
(Zek. 13:1).
Pale wayahudi ambao wamepona wanapotaja alama za misumari mkononi na kuuliza:
"Na mtu atamwambia, J
e! jeraha hizi uizo nazo kati ya mkono yako ni nini?
naye atajibu,
Ni jeraha nilizotiwa katika nyumba ya rafiki zangu"
Zek. 13:6.
Huu utakuwa wakati mgumu kwani wayahudi
watajuta kwa ajli ya kutenda dhambi, na pia kwa ajili mababu zao walimkataa masihi wakati yeye alipokuja mara ya kwanza.
Katika Zekaria:
"Nami nitawamwagia watu wa nyumba ya Daudi,
na wenyeji wa Yerusalemu, roho ya neema na kuomba;
nao watamtazama yeye ambaye walimchoma;
nao watamuombolezea, kama vile mtu amuombolezeaye mwanawe wa pekee;
nao wataona uchungu kwa ajili yake, kama vile mtu aonavyo uchungu kwa ajili ya mzaliwa wake wa kwanza.
Siku hiyo kutakuwa na maombolezo makuu huko Yerusalemu,
kama maombolezo ya Haddarimoni katika bonde la Megido"
(Zek. 12:10-11).
Kristo ataunganishwa na wale aliosafishwa,
wanaokimbia na wenye huzuni, naye atawatia moyo na maneno haya:
"Nami nitaleta fungu lile la tatu na kulipitisha
kati ya moto, nami nitawasafisha kama fedha isafishwayo,
nami nitawajaribu kama dhahabu ijaribiwavyo;
wataliita jina langu,nami nitawasikia; mimi nitasema,
watu hawa ndio wangu; nao watasema, Bwana
ndiye Mungu wangu"
(Zek. 13:9).
MUNGU WANGU WA MBINGUNI AKUBARIKI MSOMAJI WANGU,
Nakupenda sana ndo maana najitahidi kukushirikisha hiki kidogo.
Lakini pia, nikuombe, nitie moyo na unishike kwa mkono wako, ukiwa na chochote
kama sadaka kwa Bwana, ukiguswa nibariki pia.
Ndimi ndugu yako
Ev. Elimeleck S Ndashikiwe
Tel: +255767445846
+255715445846