Pages

Subscribe:

Thursday, 11 August 2016

UCHAWI UPO Acha Ubishi

MASHAMBULIZI KATIKA NDOTO  Lengo Kuu:
Kujua Jinsi gani wachawi hupambana na wanadamu kwenye ndoto

Lengo Mahususi:
Tunawezaje kuwashinda Mashambulio haya katika ndoto.
Tafiti zinaonesha kuwa,
Karibu kila aliyeuawa na nguvu ya wachawi aliota kwa namna moja au nyingine.

Ndoto hizo ni pamoja na kuota unapigwa risasi,
unagombana na mtu unayemjua au usiyemjua
anaweza akawa,
jirani,
mme,
mke,
mtoto n.k.

Ndoto nyingine ni pamoja na zile za kufukuzwa na vichaa,
kukimbizwa na wanyama wakali na hatimaye kukupa hofu sana.
Hizo ni roho ambazo wachawi huzitumia kujaribu imani yako na kupitia ndoto hizo hukushambulia sana.

Aidha,
inakupasa ujue kuwa endapo utakamatwa na vichaa hao wanaokukimbiza,
au kama ukianguka wakati unakimbizwa,
hiyo ni dalili ya kushindwa kwako.

Unapaswa kuomba Mungu sana na Kujifunika kwa damu ya YESU.
Pia,
kama unaota unaongea na watu waliokufa huku wakisema kuwa ni rafiki zako,
kutokewa na sauti za watu waliokufa hususani unapokuwa peke yako hata kama ni mchana,
jua hiyo ni mbinu ya kipepo kwa kuwa unatumiwa mizimu ili ije kukuita na kukutambulisha kuzimuni.

Ita jina la Yesu kwa kumaanisha ili ujiepushe na nguvu hizo zinazokufuatilia.

Ndoto nyingine zinazotumiwa ni sawa na zile za kuota uko porini peke yako,
kuota uko kwenye giza nene linalokupa hofu.

Pia,
kuota umeumwa na wadudu wakali kama siafu,
nge,
tandu,
nyuki,
manyigu,
nyoka na
mbwa
ni dalili mbaya hasa kwa wajawazito kwani huashiria kuchukuliwa kwa mtoto aliyeko tumboni,
hii husababisha mimba kuharibika zaidi karibu na kujifungua.

Pia ndoto zinazokuja zikikuonesha kuwa unajifungua alafu anaepokea mtoto humfaham,
au pengine unaona mikono tu ikipokea mtoto,
ni ndoto za kipepo ambazo zinachukua mtoto wako;
ndoto hizi zinaweza kupelekea mtoto kufia tumboni,
na hata wakati mwingine mama kupata kifafa cha uzazi ambacho kinaweza kusababisha kifo chake.

Jambo la msingi hapa,
ni kukemea nguvu zote za giza zilizokuzunguka,
huku ukiukabidhi ujauzito wako kwa Yesu ili aulinde wala adui asiweze kuuharibu.

Kwa kufanya maombi haya, unaweza kuzuwia kifo hiki,
unaweza kuzuwia upasuaji wakati wa kujifungua na unaweza kunusulu maisha ya mama na mtoto,
japo mara nyingi mtoto.

Kufanya hivi kunakupa usalama kutoka na ahadi ya neno la Mungu ya kuwa

“...kila atakayeliita jina la BWANA ataokoka” (Warumi 10:13).

Kuoka hapa maana yake ni Kunusurika, kuponea chupu chupu.
Unapaswa kujua kuwa jina la Yesu lina nguvu sana na lina mamlaka kamili juu ya vitu vyote duniani na mbinguni,

vinavyoonekana na visivyoonekana, hivyo kwa kufanya hivyo utakuwa umeahirisha msiba wako.

“Kwa kuwa katika yeye,
vitu vyote viliumbwa,
vilivyo mbinguni, na vilivyo juu ya nchi vinavyoonekana na visivyoonekana ikiwa ni vitu vya enzi au malaika, vyote viliumbwa kwa njia yake na kwaajili yake.” (Wakolosai 1:16,)”

...Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia jina lipitalo kila jina, ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni na vya nchi kavu....”
(Wafilipi 2:9-11)

Hatahivyo, pamoja na nguvu iliyoko kwenye jina la Yesu na mamlaka yote,
unapaswa kujua kuwa,
unapaswa kuishika haki yote ili kuweza kupata msaada huu yaani kuwa na imani na kusihi katika hali ya kumpendeza Mungu.

Pepo wanamjua Yesu,
na wanamwogopa,
ila hawashituliwi na anayetumia jina hilo kama hajashika haki kamili ya jina la Yesu.(Matendo 19:13-16)

“baadhi ya wayahudi wenye kutanga-tanga, nao ni wapunga mapepo, wakajaribu kutaja jina la Bwana Yesu juu yao waliopagawa na mapepo....
yule pepo mchafu akawajibu,
akawambia,

Yesu tunamjua na Paulo tunamfahamu, lakini ninyi ni nani?
Na yule mtu mwenye pepo mchafu akawarukia wawili,
akawaweza, akawashinda hata wakatoka mbio ili hali wa uchi na kujeruhiwa.”

Ninachotaka kukwambia hapa ni kuwa, unapaswa utambulike katika ulimwengu wa roho kwanza na hapo ndipo Jina la Yesu litakupa ushindi,
na ukisomeka kwa kuwa na jina la Yesu,

kila utakacho kiamuru kitakutii,
kutokana na mamlaka unayotumia ambalo ni jina la Yesu ambalo kila kilichoumbwa kinatii na kutetemeka mbele yake.

Unapaswa kujua kuwa,
kulitaja jina la Yesu bila kutambulika katika ulimwengu wa roho ni sawa na kuwa na simu isiyo na chaji japo kweli salio linatosha,
ila huwezi kupiga simu wala kutuma ujumbe wowote,
kwasababu hauko hewani;

hivyo basi unapaswa kuwa kwenye mtandao na malaika wa mbinguni ili kuambatana na jina la Yesu Kristo.

Na hii ndiyo maana Yesu mwenyewe anasema
“ninyi mkikaa ndani yangu,
na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote,
nanyi mtapewa” (Yohana 15:7).

Ndugu yangu,
naomba ni kwambie kuwa maombi yako daima,
yapeleke mbele za Yesu mwenyewe,
hapo ndipo utakapojibiwa,

naomba nikwambie kitu kimoja,
epuka mafundisho ya uongo ambayo maombi
yanapitia watu waliokufa eti kwa kuwa ni watatifu,

mitume au manabii wa zamani,
bibilia inasema
hayo ni machukizo mbele za Mungu, wala Mungu hawezi kuyajibu,
kwa kuwa anasema hayuko radhi na wapumbavu,
ebu omba kupitia Jina la Yesu kwa kuwa ndiyo anuani tuliyopewa.

Kuomba kupitia wafu au watu wengine kama
Paulo,
Isaya,
Bikra Maria
na Watakatifu wengine,
siyo njia sahihi,

ni sawa na mtu unampigia simu halafu, unakosea namba,
kimsingi hutampata,
nawaomba mbadilike,

liangalie neno la Mungu linavyosema, yapuuze mafundisho ya upotovu. Hayatakusaidia lolote.

Kwa upande mwingine,
unapoota unaumwa na mbwa au nyoka, au
kukimbizwa na wanyama hata wakakuangusha,
humaanisha kuwa uko dhaifu kiroho.

Pia,
unaweza kuota majitu yenye sura zisizo tambulika sahihi na pengine kuona vivuli vinakukaribia
au vinyago,
hii ni hatari sana kwani ni ishara ya kuwa adui yuko karibu yako,
anaweza akawa rafiki au hata ndugu na amekushinda kumtambua,
hivyo amekudhoofisha kiimani na karibu atakuangamiza.

Ndoto hizo pamoja na zile zakuota unaliwa na wanyama mwitu kama vile simba,
chui na
mbwa mwitu,
au kuota unachukuliwa hewani,
huweza kusababisha mtu kuvurugika akili na hata kuehuka.

Hii ni hatari sana,
kwani zinatumika sana kuangamiza watu kupitia njia hii.

Pia,
mara nyingi huweza kuota umetoka huko unatembea na watu ambao huwajui, aghalabu huongea vitu/lugha ambavyo huijui,
na wakati mwingine hujisikia unagandamizwa chini,

ukijaribu kupiga kelele au kuamka unashindwa,

zote hizi ni dalili za kulegea kiroho na huweza kukupelekea mashambulizi makubwa ambayo hukuotesha ndoto chafu huku ukiwa unalishwa vitu mara nyingi nyama,

ukifanya tendo la ndoa na watu usiowajua.

Hii huufanya mwili kuwa najisi na kuibomoa madhabahu ya roho mtakatifu anayekaa ndani yako,
hivyo mapepo kupata nafasi.

La msingi,
chukua hatua ya kufanya maombi ya muda mrefu usiku huo,
na anza maombi makavu yaani kufunga bila kula wala kunywa walau masaa kumi na mawili.

Fanya hivyo mara nyingi zaidi,
na tenga muda wa kusoma neno la Mungu,
huku ukilitafakari kwa kina.

Aidha,
jenga mazoea ya kuamka usiku na kuomba na kukemea nguvu zote za giza, huku ukiita ulinzi wa malaika wa Mungu. Kumbuka,

“....kushinda kwetu sisi si juu ya damu na nyama;
bali ni juu ya falme na mamlaka juu ya wakuu wa giza hili,
juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho” Efeso 6:12.

Pia,
Yesu mwenyewe anasema,
“Tazama nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge,
na nguvu zote za adui wala hakuna kitu cha kuwadhuru” Luka 10:19.

Mungu awabariki na kuwapa Ulinzi daima.
Akupeni uwezo wa kuzishinda njia zote za adui,
na mipango yote ya kipepo iwe chini ya nyayo zako.

Ameeeeeeen

Ni mimi ndugu yako
Ev. Elimeleck S. Ndashikiwe

UTANGULIZI HALI YA KANISA LA KWANZA Ahadi ya Yesu kwa Mitume Kitabu cha Matendo ya Mitume moja kwa moja kinaanza kutambulisha kusudi la kufufuka na kupaa kwa Bwana Yesu Kristo. Tukio linalosimuliwa ni namna ya kuzaliwa kwa kanisa (Mdo. 1.8). Kwamba kuzaliwa kwa kanisa na utume ni kazi ya Mungu kupitia Roho Mtakatifu ambaye anakuja kuendeleza kazi aliyoianzisha Yesu. Tukio la kupaa na ahadi ya Yesu kwa wanafunzi wake, inafuatiwa na tukio muhimu sana kwa Kanisa (Mdo. 2:1-10). Wanafunzi wanavuviwa na Roho Mtakatifu na kupata nguvu kama ahadi ya Yesu ilivyosema. Kuanza kwa Kanisa la Kwanza Kwa tukio hili, kasi ya kuineza injili kwa ujasiri mkubwa wakiongozwa na Roho Mtakatifu. Kwa njia ya Roho Mtakatifu, Mitume walitambua na kuelewa hasa maana ya huduma ya Yesu Kristo kwa ulimwengu na kuanza kuihubiri injili kwa watu wote. Kituo kikuu cha umisheni kilikuwa Yerusalem kama walivyoagizwa na Yesu. Lakini kutokana na upinzani mkubwa ulioongozwa na makundi ya dini ya kiyahudi ilipelekea Injili kwenda nje ya Yerusalem na kupokelewa zaidi. Kanisa matesoni Kasi ya kukuwa kwa kanisa, kama nilivyokwisha sema hapo juu, inaletea kanisa kukutana na uadui na kusababisha kuuwawa kwa baadhi ya mitume. Kifo cha Stephano ni mfano mkuu dhidi ya vifo vingi ambavyo vilitokea wakati huo. Ikumbukwe kuwa wakati huu utawala wa dola ya kirumi ulichangia pia kudhoofu nguvu ya ukuaji wa neno la Mungu kupitia mitume (Mdo. 4-7). HISTORI YA MAISHA YA PAULO Sauli kama Falsayo Historia ya Paulo, inatambulishwa mara ya kwanza kama kijana mtesaji wa kanisa, wakati wa kifo cha Stefano alikuwepo. Lakini kimsingi Paulo alikuwa mmoja wapo katika kundi la mafarisayo. Kundi ambalo lilikuwa kinyume na mafundisho yake Yesu Kristo na Mitume ambao walitumika kuendeleza kazi au utume huo. Paulo ambaye ni Sauli aliamini kwamba Mungu ni mmoja, na muumbaji wa vitu vyote. Imani aliyoikiri kama myahudi, mwebrania na falisayo. Kwamba Mungu katika kuhusiana: watu na ulimwengu alijitenga mbali zaidi, ili aweze kutawala kila kitu na kwa kupita malaika wake. Na baadhi ya malaika wake hawakuwa waaminifu hata kutenda dhambi ‘uasi’ (Kol. 2.15). Na uovu uliingia kwa mwanadamu wa kwanza Adam (Rum. 5.12). Mambo mengine kama sabato, torati, familia, na mifumo mbalimbali ya maisha katika jamii ya kiyahudi alijifunza na kuyashika sawa sawa. Sauli kama Mtesi wa Kanisa Kwa kutekeleza sera ya dini yake, Sauli aliongoza makundi ya kuwakamata, kuwafunga, kuwatesa na kuwauwa mitume kwa lengo la kuteketeza utume uliasisiwa na Yesu (8.1-3). Kutokana na adha hiyo, wanafunzi walikimbia Yerusalem na kwenda mbali huko na huko walifuatwa na kukamatwa na hata kuuwawa. Mateso hayo yalisaidia sana kukuwa kwa kanisa, kwani kutokana na hofu, mitume walitawanyika sehemu mbalimbali bila kuacha kuitangaza injili (8.1). Kwa ujumla Sauli alizaliwa Tarso, mji ulikuwa nje ya Palestina chini ya utawala wa Kirumi, Lugha iliyotumika ni kiyunani na kirumi (Greceo Romana). Lakini kwa asili alikuwa myahudi wa kabila la Benjamini (Fil. 3.3-5). Kuongolewa kwa Sauli Katika mpango wake wa kwenda Dameska kuwaangamiza mitume, njiani alikutana na muujiza ulio badili maisha yake. Sauli anakutana na ufahamu tofauti juu ya Yesu Kristo ambaye alitambua kuwa alikufa na hakufufuka (9.1-19; 22.1-22 na 26.9-23). Uzoefu huu unafanya mapinduzi makubwa katika maisha yake. Anaongolewa katika imani ya Kikristo, anabatizwa, na kupokelewa katika kanisa la Dameska (9.10-31). Yesu alimtuma kuifanyakazi ya injili kama chombo kwa mataifa (9.15). Kumbuka kuwa Sauli alizaliwa na kukulia Tarso ambako wenyeji wake ni wayunani na kwa uchache sana wayahudi waishio Tarso. Majina yote hayo mawili yana maana sawa kwa ujumla wa utofauti wa matumizi kwa makabila haya. Sauli ni jina la Kiyahuidi lenye maana ‘kijana nadhifu wa akili’ kwa kiyunani ‘saulos’ lilikuwa tusi – ujinga. Paulo ni jina la asili ya Kiyunani lenye maana sawa na Sauli kwa kiebrania ‘mjuvi wa mambo’. Hivyo Sauli aliamua kutumia jina la kiyunani ili isiwe kwazo kwao na bado ikawa sawa kwa kabila lake mwenyewe. HUDUMA NA UTUMISHI WA PAULO Mwanzo wa huduma ya Paulo Paulo alikutana na upinzani mkubwa kutoka kwa mitume, kwani hawakuamini kabisa juu ya kuongolewa kwake, ilimpelekea Paulo kuondoka Yerusalem si tu kwa kuwaepuka wanafunzi wa Yesu ila pia kuwatoroka mafarisayo wenzake. Aliondoka na kurudi nyumbani kabla ya kuanza huduma kamili. Pamoja na kuwa katika hali ya upinzani wa ndani, Paulo hakuacha kumshuhudia Kristo. Baada ya kuokolewa 32 BK, Paulo aliishi na kuhubiri Damaska kwa muda wa miaka mitatu 32 – 35 BK (Gal. 1.15-19 na Mdo. 9.20-25). Paulo alifanya ziara ndogo kwenda Yerusalem 35 BK, na ilifuata baraza la mitume, na kurudi tena mjini alikozaliwa (Mdo. 9.26-31). Paulo alibakia Tarso kwa muda wa miaka nane 35-44 BK. Hakuna shaka kuwa alifanyakazi ya Injili kwa wayahudi wa uhamishoni na wayunani pia. Kwa kipindi hiki, idadi ya wakristo na makanisa iliongezeka mara dufu. Hata Mitume kule Yerusalem walimtuma Barnaba kwenda Antiokia kukutana na Paulo kwa ajili ya kazi ya injili kati ya mwaka 45 na 46 (Mdo. 11.19-30). Waliondoka Antiokia na kuelekea mbali zaidi kuihubiri injili katika maeneo yote ya utawala wa kirumi hasa waliozungumza kirumi na kiyunani (Mdo. 13.1-3). Siku za Paulo kama mchungaji zilikamilika. Paulo alikuwa akihudumu kama msafiri mmisionari katika ulimwengu wa wakati wake. Safari za Paulo za Kimitume Paulo kama mtume wa mataifa alifanya safari kubwa tatu; safari ya kwanza ilifanyika mwaka 47 – 49 BK, alipeleka ujumbe wa neno la Mungu pande za Syria na Asia ndogo (Mdo. 13-14). Safari ya Pili na ya tatu zilifanyika 49 -52 BK na 52-57 BK. Ambako alisafiri kuelekea maeneo ya Asia ndogo, Makedonia na uyunani yote (Mdo. 15.38-18.21 na 18.22 – 21.16. Kama matokeo ya juhudi za Paulo katika kuhubiri na kufundisha; wayunani wengi walimgeukia Kristo na kuanzishwa kwa makanisa mengi madogo madogo. Kutumika kwa Paulo kama mtume kwa mataifa, kulileta sintofahamu kati ya wayahudi juu ya kuwatambua wayunani kama wamoja katika imani yake Kristo. Wakristo ambao walikuwa bado katika kifungo cha kanuni za kiyahudi, ndio walioleta shida katika kuwajumuisha wayunani kushiriki Baraka za neema ya Mungu ya wokovu. Paulo alishambuliwa hata kuuwawa na kundi hilo (Mdo. 21-22). Masingizio mengi yalimkabili Paulo ili mradi akatishwe tamaa ya kuupeleka ujumbe wa Mungu kwa mataifa. Alikamatwa na kuwekwa gerezani huko Yerusalem na kisha akahamishiwa Kaisaria kwa miaka miwili 59-59 BK (Mdo. 23-24). Paulo alitumia nafasi ya uraia wake na sifa ya kuzaliwa kwake kujitetea panapotokea utatanishi wa uamuzi wa mashitaka yake (Mdo. 25.1-12). Paulo alifungwa Rumi kwa miaka miwili 59-61 BK. (Mdo. 28.17). hadi mashitaka dhidi yake yalipofutwa na kuachwa huru. Mara akatoka kifungoni, Paulo aliendelea kuihubiri injili pembezoni mwa viuga vya Spaini na mji wa Rumi. Lakini mwaka 54-68, Mfalme Nero wa Rumi alikuwa na mpango wa mauji na mateso makali kwa wakristo na kufanikiwa kumuuwa Paulo mnamo mwaka 68 BK. Nyaraka za Paulo Kimsingi, Paulo aliwezeshwa sana kuandika Nyaraka mbali mbali si kwa lengo la vitabu, bali kufundisha, kukumea na kusahihisha makosa ya uelewa wa mafundisho yake kwa njia ya barua. Nyaraka alizoziandika hazikuwa zenye mtazamo ya kitheologia kama hivi leo, bali ulikuwa ni ujumbe wa moja kwa moja kwa makundi husika na eneo husika ikiambatana na ujumbe tarajiwa. Paulo aliweza kuandika nyaraka nyingi zaidi ya nyaraka tuzisomazo katika Biblia. Nyaraka hizo zilipitishwa na kanuni za maandiko ili zitumike kama sehemu ya nyaraka zilizobeba ujumbe wa wokovu wetu. Vyaraka zipatazo 13 ziliandikwa na Paulo mwenyewe, ya mkini waraka kwa Waebrania, Paulo aliuandika pia. Wapo wanazuoni wanasisitiza kuwa si Paulo aliyeandika ila chanzo kikuu ni makuhani kwa vile kina mazingira ya kikuhani zaidi. Lakini watheoligia wa sasa wanapendekeza uandishi wa waraka huo ni kazi ya Paulo iliyokusanywa na kuhaririwa na ama Luka, Apollo, au Barnaba, kwa lengo la kuwaabarisha wayahudi wa uhamishoni juu ya msingi wa imani yao juu ya Wazee wa imani, Kristo Yesu, Hekalu ufalme wa Mungu na kanisa Nyaraka zilizoandikwa kwenye makundi maalum ya wakristo; Warumi, 1 na 2 Wakorinto, Wagalatia, Wafilipi, Wakolosai, 1 na 2 Wathesalonike.

Thursday, 30 June 2016

MGOGORO WA WAISREL na WAPALESTINA

Mgogoro uliopo kati ya Wayahudi(Waisraeli) na Wapalestina

umeigawanya dunia,
ambapo wapo wanaoamini kuwa Wayahudi ndio wanaopaswa kuwa wamiliki halali wa
Nchi ya Israeli

na wapo wanaoamini kwamba Wapalestina ndio wanaopaswa kuikalia Nchi hiyo kama Nchi yao .

Kwa watu wengine Wayahudi wanaonekana ni watu wakatili wanaoikalia Nchi hiyo kimabavu huku wakiwanyanyasa Wapalestina.

Wakati baadhi ya watu wanadai Wayahudi ndio wenye Nchi hiyo na Wapalestina wanaonekana ni Magaidi na watu wakorofi wanaowanyanayasa Wapalestina.Baadhi ya Wasomi na wachambuzi wa mambo ya kisiasa wanaona kwamba Wapalestina wanatendewa visivyo.

Baadhi ya Waislamu wao wanalichukulia suala la kunyanyaswa Wapalestina kuwa ni la mgogoro wa kidini na kwamba Wapalestina wananyanyaswa kwasababu ya Uislamu wao.

Kimsingi mgogoro wa Wayahudi na Wapalestina umegawanyika kidini na kisiasa.

Waisraeli ndio wenye Nchi kidini lakini kisiasa Wayahudi au Waisraeli ni wakoloni wanaoikalia Nchi ya Wapalestina kimabavu.
Imeshindwa kueleweka kwamba mgogoro wa Waisraeli na Wapalestina utatatuliwa kwa njia gani kwani Mataifa haya mawili yote yanaonekana kufanya harakati kwa njia zinazotafsiriwa kuwa za kigaidi.

Wengine wamekuwa wakiilaumu Marekani kwamba inawapendelea Waisraeli kitu ambacho mimi naona si kweli kulingana na mgogoro wenyewe, ila ninachokiamini hapa ni ugumu wa mgogoro wenyewe.

Yameandikwa mengi kuhusiana na mgogoro huo na kila mmoja ametoa maoni yake namna ya kutatua mgogoro huo.
Imeundwa mikataba mingi ili kuleta amani katika Nchi hiyo na eneo la Mashariki ya Kati.

Wapalestina wamekuwa wakidai kunyanyaswa na Waisraeli kwa kupigwa na kutemewa mate usoni mbele ya watoto wao kitu kinachowafanya wakate tama na kujitoa muhanga kwa kujiua wenyewe ili mradi wameuwa Wayahudi kadhaa. Mbinu hiyo ya Wapalestina sijui walifundishwa na nani kwani inaonekana ni ya kujidhalilisha zaidi kuliko kutetea maslahi yao .

Pengine tuyaangalie madai ya Wapalestina yanayowafanya wapambane na Waisraeli kufa na kupona.
Kimsingi Wapalestina wanapigania haki ya kuwepo Taifa kamili la Kipalestina,
Mji wa Jerusalemu ambao ndio wanadai Mji Mkuu wa Nchi yao na kurudi kwa Wapalestina zaidi ya Milioni 5 ambao ni wakimbizi katika Nchi mbalimbali Duniani ambapo kwa sheria za Israeli hawaruhusiwi kurudi Palestina bila kibali maalumu. Watu wengi wamekuwa wakijiuliza nini hatma ya mgogoro wa Waisraeli na Wapalestina.

Kila mmoja anatoa majibu yake jinsi anavyoufahamu mgogoro huo. Hata hivyo majibu ya msingi ya namna ya kutatua mgogoro huo yanakosekana. Kufuatia mgogoro huo maswali ya msingi yamekuwa yakijitokeza na watu wengi wamekuwa wakijiuliza maswali mengi bila majibu,baadhi ya maswali hayo ni kwa nini Waisraeli na Wapalestina wanashindwa kuelewana, nani atamaliza mgogoro wa Mataifa hayo na Je mgogoro baina ya Mataifa hayo utakwisha na je Wapalestina wataweza kujikwamua kwenye makucha ya Waisraeli?.

Mgogoro wa Waisraeli na Wapalestina una mlolongo mrefu sana uliochanganyika na udini ndani yake na ambao unawachanganya watu wengi na kuwaachia maswali mengi.
Kama nilivyosema awali kwamba kuna Mikataba mingi iliundwa ili kujaribu kuleta amani katika Nchi hiyo ya Palestina huko Mashariki ya Kati.

Moja ya mikataba iliyoundwa na inayokumbukwa ni Mkataba wa Oslo ambao ulisainiwa katika Hoteli ya Plaza Mjini Oslo Norway Septemba 13, 1993.

Mkataba huo ulipingwa na baadhi ya wasomi wa kiarabu wakidai una kasoro nyingi na baadhi ya wasomi hao walidai kuwa mkataba huo uliokuwa na vifungu 17 na kurasa 14 za ufafanuzi ulikuwa na mapungufu mengi.

Wasomi hao walisema upungufu wa kwanza katika mkataba huo ni kuwaondolea Wapalestina hadhi ya kuwa Taifa kamili na kuishia kuwapa uwezo wa kuwa na mamlaka ya ndani (Internal Palestinian Authority ).

Upungufu wa pili wasomi hao walisema mazungumzo ya mkataba huo hayakugusia lolote kuhusu hatma ya Mji wa Jerualem ambapo Wapalestina wamekuwa wakiupigania sambamba na Taifa lao.

Wapalestina wanadai Jerusalem ndio makao yao makuu na kwamba utakuwa Mji Mkuu pindi watakapounda Taifa lao. Wasomi hao walisema mkataba utakaokwepa kuzungumzia hatma ya Jerusalem watakwepa kuuzungumzia. Kimsingi mkataba huo wa Oslo haukuweza kutatua matatizo baina ya Waisraeli na Wapalestina zaidi ya kuongezea matatizo na lawama nyingi kumwangukia aliyekuwa kiongozi wa Wapalestina wa wakati huo Marehemu Yasser Arafat kwa kuukubali mkataba huo.

Manyanyaso ya Waisraeli dhidi ya Wapalestina yalipelekea kuundwa kwa chama cha Ukombozi wa wapalestina PLO, kilichoongozwa na Marehemu Ysser Arafat.
Karibu Nchi zote zilizokuwa zikitawaliwa hapa duniani zimejikomboa kutoka kwenye makucha ya wakoloni na kujitawala,
swali ni kwamba ni lini Wapalestina watapata Uhuru wao?.

Je watumie njia gani kuwatimua Waisraeli kwenye Nchi wanayodai ni ya kwao, je watumie mtutu wa Bunduki ambao ulishindwa kwenye vita ya Mwaka 1967 iliyojulikana kama vita ya siku saba, pale Waarabu walipoungana ili kuwaondoa Waisraeli katika Nchi hiyo ya Mashariki ya Kati.

Je watumie mdomo kuwabembeleza Waisraeli kuondoka Nchini humo na kama wakiondoka watakwenda kuishi wapi? Hayo ni maswali magumu kujibiwa. Kisiasa Waisraeli wanaonekana ni walowezi na wakoloni ambao wanaikalia Nchi isiyo yao kimabavu na wanaonekana ni watu wakatili na wasio na huruma kwa wenyeji wao Wapalestina.

Wanaonekana kama wakaburu wa Afrika ya Kusini katika miaka ya nyuma au Wareno katika Nchi ya Msumbiji katika enzi za ukoloni.
Lakini la kujiuliza ni kwamba hawa ni wakoloni wa aina gani wanaotaka kukaa kwenye Nchi ya wenzao milele licha ya kelele zinazoambatana na machozi ya mamba za baadhi ya Mataifa makubwa ya Ulaya.

Baadhi ya wasomi na wachunguzi wa mambo ya kisiasa wanasema Wapalestina ndio wanaopaswa kuikalia kihalali Nchi hiyo ya Palestina na kwamba Wayahudi walifika tu hapo na kuikalia Nchi hiyo.

Hebu tuangalie kidini Taifa hili la Israeli kwa kuangalia Kitabu Kitakatifu cha Biblia na baadhi ya vitabu vya dini. Kimsingi Taifa hili lenye nguvu za kijeshi linaanzia kwa mtu mmoja anayeitwa Abramu ambaye baadaye alibarikiwa na Mungu na kuitwa Ibrahimu.

Baadhi ya maandiko toka kwenye Biblia yanasema mimi agano langu nimelifanya nawe, nawe utakuwa Baba wa Mataifa mengi wala jina lako hutaitwa tena Abramu, lakini jina lako litakuwa Ibrahimu kwani nimekuweka uwe Baba wa Mataifa mengi.

Nitakufanya uwe na uzao mwingi sana , nami nitakufanya kuwa Mataifa, na wafalme watatoka kwako. Agano langu nitalifanya imara kati ya mimi na wewe na uzao wako baada yako, na vizazi vyao, kuwa Agano la milele, kwamba nitakuwa Mungu kwako na kwa uzao wako baba yako. Nami nitakupa wewe uzao wako baada yako Nchi hii unayoikaa ugeni, nchi yote ya Kaanani kuwa milki yako ya milele. (Mwanzo 17:4-7).

Mungu alimtokea Ibrahimu wakati akiwa na miaka 100 na mkewe Sarai akiwa na miaka 90 na kusema,
Sarai mkeo hutamwita jina lake Sarai, kwa kuwa jina lake ataitwa Sara.

Nami nitambariki na tena nitakupa mwana kwake, naam nitambariki, naye atakuwa mama wa mataifa na wafalme wa kabila watatoka kwake. (Mwanzo 17:15-16).

Baada ya kuambiwa maneno hayo na Mungu Ibrahimu na Sara hawakuamini kwani walikuwa wazee na miaka yote waliishi bila kupata mtoto ambapo Sara alikuwa tasa.
Licha ya mashaka hayo waliyokuwa nayo Ibrahimu na Sara lakini Mungu aliwasisitiza kwamba watapata mtoto ambaye watamwita Isaka.

Kwa Mungu hakuna linaloshindikana baada ya muda ule uliotamkwa na Mungu kwamba Sara angepata mimba akapata mimba na kumzalia Ibrahimu mtoto wa kiume katika uzee wake. Ibrahimu akamwita mtoto huyo Isaka kama Mungu alivyosema (Mwanzo 21:1-3).

Kimsingi Ibrahimu ambaye Baba yake aliitwa Tera ndio Msingi mkubwa wa Taifa hili. Isaka alizaa watoto wawili mapacha, akawaita Esau ambaye alikuwa mkubwa yaani Kulwa na mdogo aliitwa Yakobo, yaani Doto.

Kama ilivyo kwa mama yake pia mke wa Isaka aliyeitwa Rebeka alikuwa Tasa, watoto hao aliwapata baada ya kumwomba Mungu (Mwanzo 25:21,24:26).

Esau alikuwa mwindaji hodari wakati Yakobo alitulia nyumbani. Isaka alimpenda Esau lakini Rebeka mkewe alimpenda Yakobo.
Wakati Isaka alipokuwa Mzee akikaribia kufa akataka kumbariki mwanaye mkubwa Esau kutokana na uzee Isaka alikuwa amepofuka macho.

Ilikuwa desturi za wakati ule Baba kumbariki mwanaye wa kwanza kabla ya kufa. Isaka akamwita mwanaye wa kwanza,
Esau na kumweleza kwamba yeye ameshakuwa mzee hivyo anataka kumbariki kabla hajafa,
akamwambia amfanyie chakula kitamu kabla hajambariki kama ilivyokuwa desturi ya wakati huo.

Esau alipoambiwa hayo akaenda nyikani kuwinda ili amtengenezee Baba yake nyama kama alivyomuagiza.
Wakati Isaka akizungumza na Esau ndani Rebeka alisikia na akamwita Yakobo na kumwambia nimemsikia baba yako akimwambia Esau akatafute mawindo amfanyie chakula ili apate kumbariki. Rebeka akamwambia Yakobo akamletee mbuzi wawili ili akamtengenezee na akampe baba yake ili apate kumbariki.

Kulikuwa na mabishano kati ya Yakobo na Mama yake ambapo Yakobo akamwambia Mama yake kwamba Esau ni mtu mwenye malaika (Vinyoleo) kifuani na mikononi hivyo baba yake atakapompapasa na kugundua yeye si Esau atamlaani hivyo laana haiwezi kuwa mbaraka, lakini mama yake akamwambia laana hiyo iwe juu yake.

Yakobo akafanya kama mama yake alivyomuagiza akamletea mbuzi wawili. Mama yake akawatengeneza Mbuzi hao na kuchukua mavazi ya Esau mwanawe mkubwa na kumpa Yakobo ayavae, wakati hayo yote yakifanyika Esau alienda porini kuwinda.

Mama yake Yakobo akachukua ngozi ya Mbuzi na kumvika Yakobo mikononi na kumpa nyama ya Mbuzi iliyotengenezwa vizuri na mikate akampe Baba yake. Yakobo alipofika mbele ya Baba yake akasema nimefika Baba na nimefanya kama ulivyoniagiza.

Yakobo akamwambia baba yake inuka ule ili unibariki. Baba yake alipomuuliza wewe ni nani Yakobo akasema mimi ni Esau mzaliwa wako wa kwanza. Isaka Baba yake akamuuliza imekuwaje umefanya haraka namna hii, Yakobo akajibu Bwana Mungu wako amenifanikisha. Yakobo akamwambia Baba yake inuka unipapase, naye alipompapasa mikononi akasema mikono ni ya Esau lakini Sauti ni ya Yakobo maana hakumtambua.

Baada ya kula Isaka akambariki mwanaye. Yakobo alipotoka tu Esau naye akawa anaingia kutoka katika mawindo yake. Esau akamwambia Baba yake ondoka ule mawindo yangu ili unibariki. Isaya akamuuliza U’ nani wewe, akamjibu mimi ni Esau mzaliwa wako wa kwanza. Isaka akatetemeka na kushangaa na kuhoji ni nani aliyekuja na mawindo akaniletea, nami nimeshakula kabla hujaja wewe, nikambariki, naam naye atabarikiwa.

Baada ya kuambiwa maneno hayo Esau akalia kilio kikuu akisema nibariki na mimi, Isaka akamjibu ndugu yako amekuja kwa hila na kuchukua mbaraka wako. Baada ya hayo Esau akamchukia sana Yakobo na akapanga kumuua. Rebeka Mama yao Esau na Yakobo aliposikia kwamba Esau anapanga kumuua Yakobo alimwambia Yakobo mwanae akimbilie Harani kwa Lutu ndugu yake. Akamwambia akae huko hadi hasira ya ndugu yake itakapopungua na atakaposahau aliyotendewa. (Mwanzo 27:1-46)

Kimsingi alikokimbilia Yakobo ni sehemu za Mashariki ya Kati ya leo. Yakobo akiwa huko katika Nchi ya ugeni malaika wa Mungu alimtokea na kuongea naye na kumuuliza jina lake anaitwa nani.
Akamjibu kuwa anaitwa Yakobo.

Malaika akamwambia hutaitwa tena Yakobo bali utaitwa Israeli (Mwanzo 32:27-28). Kimsingi Taifa la Israeli ambalo linasuguana na Wapalestina huko Mashariki ya Kati linaanzia hapo.

Ni habari za uhakika kwamba Mungu alilibariki Taifa hilo katika msingi wa kidini na si wa kisiasa na asili ya dini ya kikristo ni kutoka Taifa hilo ambalo Biblia imelitaja kama Taifa teule la Mungu. Mungu aliliteua Taifa hilo kama chanzo cha kufikisha Injili yake kwa mataifa mengine,
ndio maana Wayahudi walikuwa hawachangamani na Mataifa mengine hadi alipokuja Yesu kuondoa utengano huo na kuwaambia Wayahudi wasiwaite Najisi wale walioumbwa na Mungu.

Uteule wa Wayahudi kidini kama Taifa teule la Mungu ulikoma baada ya kumkataa Yesu na kumsulubisha msalabani na kumuua Mtume wake aliyeitwa Stephano.

Kuanzia hapo sasa Injili iliwageukia Mataifa, yaani watu wengine wasio Wakristo na katika Dunia yote na ndio maana Wakristo wengine wanajiita Waisraeli wa Kiroho.

Lakini licha ya Wayahudi kumkataa Yesu hawakunyang`anywa mibaraka waliyopewa pamoja na nguvu za kijeshi walizopewa. Istoria ya awali inaonyesha kwamba mapigano kati ya waisraeli na Waarabu ni ya muda mrefu, pengine tunaweza kuyaita mapigano yao kuwa ya Jadi.

Kwa mujibu wa Kitabu Kitakatifu cha Biblia,
mapambano hayo yamekuwa yakitegemeana ambapo mara nyingine Waisraeli walikuwa wakipigwa na mara nyingine Wapalestina walikuwa wakipigwa.
Taifa hilo Teule limepitia katika mlolongo mrefu sana wa kutekwa na Mataifa mengine kama adhabu iliyotolewa na Mungu kuliadhibu Taifa hilo .

Waisraeli walikuwa watu wa kuhama hama wakitafuta mahali panapowafaa kwa kuishi.
Katika kulielezea Taifa la Israeli hatuwezi kuacha kuelezea habari za mtu mmoja aitwae Yusufu. Huyu alikuwa mtoto wa mwisho wa Yakobo. Alikuwa kijana mwenye miaka 17 kwa wakati huo, pia alikuwa mzuri wa sura (Handsome).

Katika hatua za awali alionekana kwamba angekuwa mtu mkubwa kwa nyadhifa baadaye kwani alikuwa akiota ndoto za ajabu ajabu ambazo ziliashiria hilo . Baba yake alimpenda kuliko watoto wake wote.
Alimshonea vazi zuri. Baada ya kushonewa vazi hilo wivu uliibuka toka kwa ndugu zake.

Siku moja Baba yake alimtuma Yusufu kuwapelekea chakula ndugu zake machungani walikokuwa wakichunga. Walipomwona kwa mbali akija wakasemezana tazama mwota ndoto yule anakuja, tumuue. Kaka yake aliyeitwa Reuben akasema tusimuue bali tumtupe humu kwenye shimo.

Wakachukua chakula wakamvua kanzu yake na kumtupa kwenye shimo. Wakati wakila chakula waarabu wakapita wakielekea Misri ndipo ndugu zake wakashauriana na kumuuza kwa Waarabu. Ndugu za Yusufu wakamuuza Yusufu kwa vipande 20 vya fedha.

Waarabu wakamchukua Yusufu hadi Misri. Ndugu hao wa Yusufu wakachinja Kondoo na kuirarua kanzu ya Yusufu na kumwagia damu ya Kondoo. Waliporudi wakamwambia Baba yao kwamba mnyama mkali amemla Yusufu. (Mwanzo 37:5-36).

Yusufu alipopelekwa Misri alipandishwa cheo na kuwa Waziri Mkuu kutokana na kipaji alichokuwanacho cha kutafsiri ndoto ambapo alitafsiri ndoto aliyoota Farao juu ya miaka 7 ya mavuno na miaka 7 ya njaa. (Mwanzo 40:1-57).

Kwa mujibu wa Kitabu Kitakatifu cha Biblia ni kwamba baada ya miaka 7 ya mavuno kupita kulikuwa na njaa katika Dunia yote isipokuwa Nchi ya Misri ambako walihifadhi chakula wakati ule wa miaka 7 ya Neema(mavuno).

Huo ndio ulikuwa mwanzo wa Taifa la Israeli kwenda utumwani Misri kwani kulipokuwa na njaa katika Nchi ya Israeli Yakobo na wanawe walihamia Misri ambako waliishi kwa raha mustarehe hadi alipokuja Farao asiyemtambua Yusufu (Mwanzo 46:8-27).

Waisraeli wakaanza kuzaana kwa kasi kuwashinda Wamisri wakati wana wa Israeli wakiendelea kuzaana akainuka Farao mpya asiyemfahamu Yusufu na kuwaambia Wamisri angalieni Waisraeli wengi tena wana nguvu kuliko sisi.

Farao akasema tunapaswa kutumia akili kwani ikitokea vita wanaweza kuungana na maadui zetu na kutupiga,
Basi Wamisri wakakubaliana kuwawekea Waisraeli wasimamizi ili wawatese. Kadri walivyowatesa ndivyo Waisraeli walizidi kuongezeka.
Waisraeli wakafanyishwa kazi kama watumwa ambapo walifanya kazi za mashambani, walijenga mapiramidi ambamo wafalme wa Misri walizikwa.

Alipoona Waisraeli wanazidi kuongezeka Mfalme alipitisha Amri kwamba akizaliwa mtoto Muizraeli wa kiume auawe na kama wa kike asiuawe.
Amri hii walipewa wakunga.
Wakati Waisraeli wakiteseka mikononi mwa Wamisri Mungu akamuandaa mkombozi wa kuwakomboa Waisraeli katika makucha ya Farao.

Mkombozi huyo si mwingine bali ni Musa aliyezaliwa katika Nchi ya Misri.Musa alipozaliwa alifichwa kando ya mto ili asiuawe na binti wa Farao wakati kienda kuoga alimuokota na akatatafuta msichana wa kiyahudi kwa ajili ya kumlea. (Kutoka 1:1-22, 2:1-25).

Mungu alimwandaa Musa kwa ajili ya kuwakomboa Waisraeli utumwani Misri, Musa aliandaliwa kukabiliana na Farao Mfalme wa Misri ili aweze kuwaachia Waisraeli. Musa alienda kuzungumza na Farao ili awaruhusu Waisraeli waweze kuondoka Misri kuelekea kwenye Nchi ya ahadi ambayo Mungu aliwaahidi.

Farao alikuwa mgumu kuwaruhusu Waisraeli waondoke Misri hadi pale Musa alipofanya miujiza mingi ili Farao aweze kuamini kwamba Musa ametumwa na Mungu. Muujiza wa mwisho uliomfanya Farao aamini kwamba Musa ametumwa na Mungu ni ule wa kuuawa kwa mzaliwa wa kwanza wa Misri ambapo waliuawa wanyama hadi wanadamu. (Kutoka 12:29-31).

Baada ya kuruhusiwa na Farao kutoka Misri Musa akaanza kuwaongoza Waisraeli kuelekea Nchi ya Kaanani ambayo aliwaahidi Waisraeli. Waisraeli waliishi Misri miaka 430.
Waisraeli walisafiri miaka 40 Jangwani wakielekea Nchi ya Kaanani.

Mungu aliwaongoza Waisraeli kupitia Musa. Awali Waisraeli waliambiwa watakapofika katika Nchi ya Kaanani

na Miji yake waue watu wote wasimuache hata mmoja, bali wabakize wanyama tu. Musa hakuendelea kuliongoza Taifa la Israeli kwa kuwa alikuwa mzee na hivyo hakufika katika Nchi ya ahadi.
Alikufa akiwa miaka 120 na kuzikwa katika Nchi ya Moabu na Yoshua mwana wa Nuni akashika usukani wa kuliongoza taifa la Israeli kuelekea Nchi ya hadi.

Walipofika katika Nchi hiyo kwanza wakatuma wapelelezi waende kupeleleza Nchi hiyo ambapo walifikia kwa mwanamke mmoja aliyeitwa Rahabu.

Upelelezi ulipokamilika kazi ya kuupiga mji huo ikaanza. Waisraeli wakiongozwa na Yoshua wakiipiga miji ya Nchi hiyo kwa makali ya upanga.

Waliteka miji ya Hai, Yeriko na Yordani. Awali kabla ya mapambano Yoshua aliwaambia Waisraeli kama watayasikiliza maneno ya Mungu basi Mungu atawatia Wakaanani mikononi mwao (Yoshua 3:9-10).

Yoshua akaipiga Nchi yote na kuiteka sawasawa na neno la Mungu, baada ya kuitwaa akawagawia Waisraeli urithi wao kama walivyoambiwa na Mungu (Yoshua 12:6-23).

Lakini kitu kikubwa walichokosea Waisraeli ni kuwabakiza Wakaanani, yaani Wapalestina wa leo ambao wanasuguana nao leo.
Katika vita hiyo mji mgumu kuuteka ulikuwa Yerusalemu ambao leo ndio unaopiganiwa sana na Wapalestina na Waisraeli kila mmoja akidai ni wa kwake.

Ukiondoa Misaafu ya dini,
hata vitabu vya kihistoria vinalizungumzia suala la vita hii jinsi ilivyokuwa ngumu katika kuishinda Mji wa Yerusalemu kwani kwa uwezo wa Mungu Yoshua aliamuru Jua lisimame na likasimama bila kuzama hadi Waisraeli waliposhinda.

Mfalme wa Yerusalemu aliyeitwa Adoni-Sedeki aliposikia Yoshua ameishinda Miji mingine akaungana na Wafalme watano wa Wapalestina kupambana na waisraeli ili wasije wakauteka Mji wa Yerusalemu. Kufuatia kuungana huku vita ikawa kali sana kati ya Waisraeli na Wakaanani (Wapalestina).

Wakati vita ikiendelea kupiganwa jua lilikuwa likikaribia kuzama na desturi ya enzi zile ni kwamba vita inapopiganwa linapozama jua, basi vita hutulia kwa kitambo hadi kesho yake hivyo Yoshua akachukua jukumu la kumuomba Mungu asimamishe jua hadi wao washinde. Jua lilizama baada ya Waisraeli kuushinda mji wa Yerusalemu. (Yoshua 11:1-23).

Katika miji mingine Waisraeli waliwauwa Wapalesttina wote isipokuwa katika miji ya Gath , Ashdodi na Gaza ambako kuna makazi ya Wapalestina hata hivi leo. (Yoshua 11;22).

Licha ya kuwaacha Wapalestina lakini Waisraeli walifanya mapatano na Wapalestina suala ambalo lilikatazwa na Mungu. Mungu aliwaambia Waisraeli kwa sababu wamefanya mapatano na Wapalestina basi Wapalestina watakuwa miiba mbavuni mwao na hatawafukuza watoke mbele zao (Waamuzi 2:1-3).

Lakini hata hivyo Misaafu ya dini inajichanganya yenyewe kwa mfano katika Biblia Kitabu cha Waamuzi 3:1, kinasema
“Basi hayo ndiyo Mataifa ambao Bwana aliwaacha ili awajaribu Israeli kwa hao yaani awajaribu hao wote ambao hawakuvijua vita vyote vya Kaanani, ili kwamba vizazi vya Israeli wapate kujua, ili kuwafundisha vita,
hasa wao ambao hawakuvijua vita kabla ya wakati ule, aliwaacha wakuu watano wa Wafilisti (Wapalestina) Wakaanani wote na Wasidoni na Wahivi waliokaa katika kilima cha Lebanoni toka mlima wa Baal-Hermoni mpaka kuingia Hamathi.

Awali kabisa Waisraeli waliishi Kaanani (Palestina) na kisha walienda Misri baada ya Kaanani kukumbwa na njaa. Baada ya kuibuka Farao mpya Nchini Misri, asiyemtambua Yusufu Waisraeli walianza kuteswa na kisha kurejea katika Nchi waliyodai ya kwao yaani Nchi ya Kaanani ambayo ndiyo Izraeli ya leo.

Mgogoro wa Wapalestina na Waisraeli unakuwa mgumu kwa sababu Waisraeli wanaamini Palestina ni Nchi yao waliyoahidiwa na Mungu na Wapalestina kwa upande wao wanaona wamevamiwa katika Nchi yao kama Biblia inavyosema kwamba Wapalestina watakuwa miiba kwa Waisraeli na ndivyo ilivyo hivi sasa.

Barikiwa sana mtu wa Mungu
Ni mimi ndugu yako
Ev. Elimeleck Ndashikiwe
  
   +255767445846
   +255715445846