Pages

Subscribe:

Sunday, 23 April 2017

MY PRAYERS TO MY HEAVENLY GOD


PRAYERS

In the nameof Jesus I return back home, I return back to my nature and attitude in thename of Jesus,

I return back from my transfer in the name of Jesus,
whoever is holding me from going back I slay you in the name of Jesus,

today I destroy all those who have planted evil thoughts and
attitude in me by the fire of God.

In the name of Jesus I pull down all mountains
that have stood in front me,

I destroy all the witches who are withholding my transfer by the fire of God, I pull you down by the blood of Jesus.

I open the passage of my freedom from captivity
and return back home in the name of Jesus,

I am shifting from where I was kept captive in the spiritual realm,
I return back tolife in the name of Jesus.

I return from death to life in the name of Jesus,
Ireturn from failure to victory in the name of Jesus.
I return from sadness, fearto my nature of confidence, power, ability, stability, wealthy and success bythe blood of Jesus.

I diminish anyone who is blocking me in the name of Jesus.

I destroye anyone who is preventing me from getting out of my captive the nameof Jesus.

I return back to my nature of multidisciplinary,
ownership andcontrol in the name of Jesus.

Amen

It is me your beloved
            Ev. Elimeleck S Ndashikiwe

Monday, 17 April 2017

THAMANI YA NENO LA MUNGU


Neno la MUNGU lina kazi nyingi sana ndani ya mwamini.

Kama vile ambavyo tunakula chakula cha kimwili ili tuishi na ili tupate afya, hivyo hivyo
tunakula chakula cha kiroho ambacho ni Neno la MUNGU ili tuishi kiroho na ili tupate
afya kiroho na ili tukue Kiroho.

Neno la MUNGU ni Muhimu sana ndani ya kila mteule wa KRISTO popote aliko. Leo tunaangalia
umuhimu wa Neno la MUNGU moyoni mwetu.

Je kwanini uliweke Neno la MUNGU moyoni mwako?
1. Ili usitende dhambi kwa kusahau maelekezo ya Neno hilo la MUNGU.

Zaburi 119:11
'' Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, Nisije nikakutenda dhambi.'' Kumbuka Neno la MUNGU li hai, lina nguvu na linajua.

Waebrania 4:12
'' Maana Neno la MUNGU li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili,
tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake;
tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo. ''

2. Ili likumulikie uone na kutenda katika mapenzi ya MUNGU.

ZaburiI 119:105
''Neno lako ni taa ya miguu yangu, Na mwanga wa njia yangu. ''

Kumbuka kabla ya kulijua Neno la MUNGU wote tulikuwa wajinga, lakini Neno ndio limetuondolea ujinga na kutupa
ufahamu mzuri wa kiMUNGU.

''Kufafanusha maneno yako kwatia nuru, Na kumfahamisha mjinga.-
Zaburi 119:130''

3. Ili likupe uhakika wa yajayo kama utalitii Neno hilo la MUNGU.

Yohana 5:24
'' Amin, amin, nawaambia, Yeye alisikiaye NENO langu na kumwamini yeye aliyenipeleka yuna uzima wa milele; wala haingii hukumuni,
bali amepita kutoka mautini kuingia uzimani. ''

4. Ili likutakase.

Yohana 17:17
'' Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli. ''

Hivyo tunakuwa safi kwa sababu ya Neno la MUNGU.

''Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya lile neno nililowaambia.''
Yohana 15:3

5. Ili likuongee Imani kwa MUNGU.

Warumi 10:17
'' Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo. ''

Ukiwa na imani utafanya yote katika Bwana YESU.

Wakolosai 3:17
''Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo,
fanyeni yote katika jina la Bwana YESU, mkimshukuru MUNGU Baba kwa yeye. ''

6. Ili likufanye umshinde shetani kirahisi.

Ufunuo 12:11
'' Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa NENO la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa. ''

Kumbuka Neno la MUNGU lina uponyaji na linaponya.

''Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu;
MANENO hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima.
Yohana 6:63''

Maneno ya YESU KRISTO(Neno la MUNGU) ni roho tena ni uzima.

7. Ili ulitumie kwa kazi ya MUNGU.

''Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na MUNGU,
mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali NENO la kweli.''
2 Timotheo 2:15

8. Ili neno la MUNGU likufundishe kuukulia Wokovu vyema.

''Kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa,
ili kwa hayo mpate kuukulia wokovu; ''
1 Petro 2:2

Asante kama umelielewa Neno la MUNGU ila nina neno moja la mwisho kwako leo.

BWANA YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?

Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na BWANA YESU?

Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?

Majibu sahihi yako moyoni mwako ila nakusihi mpokee
BWANA YESU 

kama hujampokea nakusihi Ishi Maisha Matakatifu
Ukiwa Ndani Ya Wokovu.

Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.

No Mimi ndugu yako mpendwa

                     Ev. Elimeleck S Ndashikiwe
              Tel: +255715445846
                      +255684485460

Friday, 14 April 2017

UCHAMBUZI BIBLIA KITABU CHA MALAKI


UTANGULIZI

Jina la kitabu hiki
Malaki
maana yake ni  “Mjumbe wangu”  au “Aliyetumwa na”.

Inawezekana likawa ndilo jina la unabii au kitambulisho maalumu kuwa mwandishi ni mjumbe halisi atokaye kwa Mungu
(2:7; 3:1).

Malaki hataji wakati wa kutoa ujumbe wake.

Inaelekea ujumbe huu ulitolewa wakati fulani wa
matengenezo ya
Ezra na Nehemia,

kwa sababu hali na matendo ambayo yanazungumzwa yafanana na ya nyakati hizo.

Wayahudi waliporudi kutoka utumwani Babeli wakiongozwa na Zerubabeli na Yoshua
walikuwa na hamasa ya kutengeneza upya na kutegemeza taifa lao kidini na kisiasa.

Lakini muda mfupi walilegea (tazama Utangulizi wa Hagai).
Kizazi kilichofuata hakikuwa na uongozi wenye kuenzi kazi nzuri ya viongozi waliowatangulia.

Watu wakarudi nyuma kiroho, hata wakatafsiri vibaya ahadi za Mungu.

Kurudi tena nchini mwao na kujenga hekalu upya walikutafsiri kuwa ni nyenzo ya
kupata enzi za Masihi.

Kwa kuwa waliyojiwekea wenyewe hayakutokea wakawa na mashaka juu ya ahadi za Mungu kwao,

waliacha ibada, ndoa za mseto kidini na talaka zikahalalika
2:10-12).

Walipopata matatizo walilalamika kuwa Mungu hakubali ibada zao (2:13-16), waliona kuwa Mungu hawatendei haki (2:17).

Malaki
anaweka mambo sawa kwamba Mungu ni mwaminifu kwa agano lake na hivyo basi hawana budi kujilaumu wao wenyewe.

Hii ni kwa sababu dhambi zao zimekuwa kizuizi cha upendo na baraka za Mungu. Malaki ametabiri

“Siku ya BWANA”  ambapo waovu watahukumiwa; kwa wanyenyekevu haki itatawala na wanaomcha Mungu watabarikiwa.

YALIYOMO:

1. Upendo wa Mungu kwa Israeli, Sura 1:1-5

2. Uovu wa viongozi wa taifa, Sura 1:6–2:17

3. Mjumbe wa Bwana, Sura 3 4. Siku ya Bwana, Sura 4