Pages

Subscribe:

Friday, 1 December 2017

THE HEAVENLY KINGDOM "GOD".

By
Ev. Elimeleck S Ndashikiwe

         Ufalme waMbinguni una wakili mkuu ambaye ni Yesu Kristo.

           1 Yohana 2:1
       Watoto wangu wapendwa, nawaandikieni haya ili msitende dhambi. Lakini kama mtu ye yote akitenda dhambi,
tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo Mwenye haki.

        Ufalme wa Mbinguni una hakimu Mkuu (Mungu).
          Na mbingu zitatangaza haki yake,
kwa maana Mungu ndiye aliye hakimu
(Zaburi 50:6).

UBARIKIWE SANA TENA SANA.

Ufalme wa Mbinguni ni urithi wetu watoto wa MUNGU tupendwao sana.

UFALME WA MBINGUNI Sehemu II..

Tunaendelea na Sehemu hii ya Pili.

BWANA YESU ASIFIWE SANA MTU WA MUNGU, Karibu sana,

UFALME WA MBINGUNI UNA KATIBA NA SHERIA.
            Katiba inatoa kanuni na taratibu ambazo raia wanazitumia ili waweze kuishi na kutawaliwa.

         Katika ufalme wa Mungu katiba inaitwa Biblia.

  Pia hujulikana kama neno la Mungu au sheria ya Mungu.
Mathayo 5:18
“18 Kwa maana, amin, nawaambia, mpaka Mbingu na Dunia zitakapopita, hakuna hata herufi moja ndogo wala nukta itakayopotea kwa namna yo yote kutoka kwenye Torati mpaka kila kitu kiwe kimetimia.”

  UFALME WA MBINGUNI UNA LUGHA YA TAIFA.
      Kunena kwa lugha ndiyo lugha ya taifa katika ufalme wa Mungu,
     Matendo 2:1-4
Ilipowadia siku ya Pentekoste, walikuwa wote mahali pamoja.
       2 Ghafula sauti kama mvumo mkubwa wa upepo uliotoka mbinguni, ukaijaza nyumba yote walimokuwa wameketi.
      3. Zikatokea ndimi kama za moto zilizogawanyika na kukaa juu ya kila mmoja wao.
       4 Wote wakajazwa na Roho Mtakatifu, wakaanza kunena kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia”.

Ufalme wa Mbinguni una utamaduni (Tunda la Roho pamoja na kusifu na kuabudu).
     Kusifu na kuabudu ni utamaduni katika ufalme wa Mbinguni
      Ufunuo 4:8
“Kila mmoja wa hawa viumbe wenye uhai wanne, alikuwa na mabawa sita na kujawa na macho pande zote, hadi chini ya mabawa.
         Usiku na mchana hawakuacha kusema‘‘Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu,
        ni Bwana Mungu Mwenyezi, aliyekuwako, aliyeko na atakayekuja.’’

Tunda la Roho pia ni utamaduni wa Mbinguni ambao ni upendo,
furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,
upole, kiasi.
          Wagalatia 5:22-23

 
UFALME WA MBINGUNI UNA SERIKALI.
         Kanisa siyo chombo cha kidini,
bali kanisa ni muundo wa serikali iliyopewa mamlaka ambayo Mfalme (Yesu Kristo) hutumia ili kuutawala ufalme wake.
           Mathayo 16: 18-19
‘‘Nami nakuambia, wewe ndiwe Petro na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu, hata malango ya kuzimu hayataweza kulishinda.
        19 Nitakupa funguo za Ufalme wa Mbinguni na lo lote utakalolifunga duniani litakuwa limefungwa Mbinguni, lo lote
utakalofungua duniani litakuwa limefunguliwa mbinguni.’’

UFALME WA MBINGUNI PIA UNA JESHI.
      Jeshi la Mbinguni ni malaika,
raia walioko katika ufalme wa Mungu wanalindwa na malaika.
     Zaburi 34:7
“Malaika wa BWANA hufanya kituo akiwazunguka wale wamchao, naye huwaokoa.”

         Ufalme wa Mbinguni una ulipaji wa kodi
(Fungu la Kumi).
Sisi kama raia wa ufalme wa Mungu, tunatakiwa kulipa kodi (zaka/ fungu la kumi).
      Malaki 3:8-10 “8
‘‘Je, mwanadamu atamwibia Mungu? Hata hivyo mnaniibia.
‘‘Lakini mnauliza, ‘Tunakuibia kwa namna gani?’ ‘‘Mnaniibia zaka(mnaniibia kodi) na dhabihu.
         9.Mko chini ya laana, ninyi taifa lote, kwa sababu mnaniibia mimi. 10Leteni zaka kamili
(leteni kodi kamili) ghalani , ili kiwemo chakula katika nyumba yangu.

Nijaribuni katika hili,’’
asema BWANA Mwenye Nguvu,
‘‘nanyi mwone kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni na kuwamwagieni
baraka nyingi mpaka mkose nafasi ya kutosha au la.”

        Ufalme wa Mbinguni una Mabalozi.
       Tumechaguliwa na Mungu na kuteuliwa kama mabalozi ili kuwakilisha matakwa na mawazo ya ufalme wa Mungu.
           Mkakati wa Mungu wa kueneza habari njema ya ufalme ulikuwa ni kutumia mabalozi.
           2 Korintho 5:20
“Kwa hiyo sisi ni mabalozi wa Kristo, kana kwamba Mungu anawasihi kwa kupitia vinywa vyetu,
nasi twawaomba sana ninyi kwa niaba ya Kristo, mpatanishwe na Mungu.”

Ufalme wa Mbinguni una Mwanasheria mkuu ambaye ni Roho mtakatifu.
           Roho mtakatifu ni mwanasheria mkuu wa Mbinguni, yeye ndiye aliyehusika katika uandikaji wa katiba (Biblia)
          2:Petro 1:20-21.
     Roho mtakatifu kama mwana sheria mkuu katika ufalme wa Mungu, yeye ndiye anayehusika katika kuwaongoza na
kuwafundisha raia wa ufalme wa Mungu jinsi ya kusema wanapopelekwa mbele ya mabalaza na mahakama au masinagogi,

      Unaposoma kitabu cha
   Luka 12:11-12
Neno la Mungu linasema hivi:-
       ‘‘Watakapowapeleka katika masinagogi mbele ya watawala na wenye mamlaka, msiwe na wasiwasi kuhusu namna mtakavyojitetea au mtakavyosema:
          12 Kwa maana Roho Mtakatifu atawafundisha wakati uo huo mnachopaswa kusema.”

Ufalme wa Mbinguni una fedha (currency) ambayo ni IMANI.
             Ufalme wa Mungu ni nchi ambayo fedha yake ni Imani.
        Huwezi ukafanya biashara yoyote katatika ufalme wa Mungu bila ya kuwa na Imani.

          Kama vile ambavyo huwezi kuishi katika nchi yoyote duniani bila fedha, vilevile huwezi kuishi katika
Ufalme wa Mungu bila ya kuwa na Imani
(Warumi 1:17, Marko 5:34).

BARIKIWA SANA MTUMISHI KWA KUENDELEA KUFUATANA NAMI.

            Ni Mimi ndugu yako
Ev. Elimeleck S Ndashikiwe.

Wednesday, 15 November 2017

MCHUMBA SAHIHI KWAKO

JINSI YA KUPATA MCHUMBA SAHIHI
May 11, 2017
Moja ya mambo ya msingi ambayo kila kijana anahitaji ni Ndoa ya Kudumu ukiacha ongezeko la kufeli kwa ndoa nyingi.
Wakati huohuo moja ya uamuzi (wa maana sana katika maisha ya binadamu ni kuamua nani atakuwa mume wako au mke wako na huu uamuzi ndiyo utakufanya uweze kuishi maisha ya namna gani katika ndoa yako na pia kuathiri kabisa mfumo wa maisha yako kuwa raha au kuwa karaha
Watu wengi katika maisha wamekuwa wakilaumu upande mwingine iwe mke wake au mume wake kwamba ndiye sababu ya kuvunjika kwa uhusiano au ndoa yao.
Huu ni ujinga muhusika mara nyingi ni wewe kwani asilimia 99 ni jinsi ulivyompata huyo mtu ambaye amesababisha ndoa yako au uhusiano kuvunjika.
Mtu anayestahili kupewa lawama zote ni wewe.
Kama hujaolewa au ndio upo kwenye process za kuolewa au kuoa,Fahamu kwamba hakuna jambo muhimu maishani mwako kama huo uamuzi unaotaka kufanya, unaweza kukupa furaha ya maisha au uchungu wa maisha hapa duniani.
Unahitaji kutumia
akili zako zote,
maombi yako yote,
uwezo wako wote na
kila resource ulizonazo
kwani hapa makosa hayana nafasi kabisa
Wala usikubali kumuoa huyo binti au kuolewa na huyo kaka eti kwa sababu:
Watu wanasema Mbona hujaolewa au kuoa!
Au ndugu zako, au mchungaji, au wazazi wako au rafiki zako wamekwambia!
Au kwa sababu umeona muda unakwenda!
Amua mwenyewe na jichunguze kama upo tayari na kama mtu unayetaka kuwa naye anakupa uhakika unaoridhika nao wewe mwenyewe.
Kumbuka it is easy to reshape the mountain siyo mtu, kwa hiyo kama kuna tabia fulani ambayo unaiona kwa mtu unayetaka kuoana naye na hujaridhika nayo Please fikiri zaidi ya mara mbili.
Na kama unaweza give time au fikiri mara nyingi zaidi.
Mara nyingi wanaosema watawabadilisha matokeo yake wao ndo wamebadishwa
Hapa huhitaji kuwa blind kwa sababu ya fall in loves, bado unahitaji kuwa na akili timamu kumfahamu zaidi huyo unataka kuoana naye kabla love haijawafanya kuwa blind au otherwise muwe blind maisha yenu yote.
Kuna maswali matano (5) ya msingi sana kujiuliza kabla hujajikamatisha vizuri kwenye hii kamba ya ndoa.

Haijalishi mtu unayetaka kuoana mmekutana wapi;
hata kama ni kanisani, shuleni, kwenye mkesha wa maombi, kijijini, mjini, hotelini, sokoni, kwenye daladala, barabarani, ofisini, kazini, safarini, kwenye semina au hata kama ni kwenye internet au njia yoyote ile ambayo Mungu anaweza kuitumia maana Mungu hafungwi na njia za kukutanisha watu.
Au Haijalishi ni mzungu, mwarabu, mchina, mwafrika, au awe mnene, mwembamba, mrefu kama Ngongoti, mfupi kama Zakayo,
Awe amesoma au hajasoma, awe mbena au mchaga au mhaya au mgogo au mzigua, au awe anatoka Canada, Kenya, Uganda, Nigeria au Tanzania. Pia haijalisha ktk kukutana naye umeunganishiwa na rafiki yako, au mchungaji wako, au wazazi wako au mtu wako wa karibu.
Kitu cha msingi ni wewe kuwa makini kujiuliza haya maswali matano muhimu.
1. JE, TUNAFANANA?
Ndoa ni kama jengo la nyumba na nyumba ni sharti iwe na msingi. Msingi imara huwezesha nyumba kuhimili kila aina ya janga linalotokea kama vile mvua, upepo, mafuriko, dhoruba, tetemeko la ardhi nk. Na kuna aina ya material zinazotumika kujengea msingi na hizi aina za material ndizo huelezea aina ya msingi na uimara wake.
Unaweza kujenga ndoa kwa kuvutiwa na umbo la mtu (mvuto wa nje) au urembo tu. Pia sasa hivi kuna uzuri mwingi tu na unauzwa dukani (body shops)
Unavutiwa na kipande kimoja tu cha mwili wake kama vile shingo, matiti, matako, unene, au wembamba, nywele, smile, anavyotembea, miguu, au kifua nk.
this is just physical attraction kuna siku anaweza kubadilika kuna kuugua, kuna ajali, kuna kubadilika mwili nk kwa hiyo ku-base kwenye mwonekano wa nje peke yake lisiwe jibu kwako kuona huyu mtu ananifaa.
Hapo utakuwa umejenga msingi wa nyumba kwa kutumia mabua au miti hakika nyumba ikishika moto hata majivu tunaweza tusipate.
Ndoa hujengwa ktk misingi 3 muhimu ambayo lazima mfanane au kuwa kitu kimoja. Ni muhimu kusiwe na gap kubwa sana katika mambo haya matatu,
Nayo ni Kimwili,
Kiakili na
Kiroho
(Mind, Body and Soul).
Mara ya kwanza mnapokutana wote mmoja anapata kuvutwa na mwingine kwa njia ya tofauti na huko kuvutwa kuna base kwenye mwonekano wa tabia kama vile anavyoongea, anavyotabasamu, anavyopenda na kwa hayo tu huwezi kusema biashara imeisha ananipenda au nimempenda na kukubaliana kuoana.
Unapotumia muda zaidi kuwa naye na kumjua zaidi, uhusiano unakua na unamfahamu zaidi ya ile physical attraction ambayo uliipata kwa mara ya kwanza sasa unaweza kutambua mambo anayopenda,
mawazo yake katika mambo mbalimbali ya kiroho,
kimwili na kiakili,
unaweza kujua talents zake na hobbies zake
hapa ndo inabidi uwe makini kufanya assessment kwani hapo ndo biashara yenyewe kwani ukimpenda na ku fall in love unakuwa blind halafu utaona kila kitu shwari hata watu wakikwambia kuna tatizo utakataa na kuwambia yupo sawa kabisa na bila yeye wewe maisha hayana maana, kumbuka huyo ni mchumba si mke/mume.
Unahitaji kuwa mchunguzi zaidi kuliko kupendwa. Kumbuka hapa unatafuta mchumba hajawa mke so ukiona kuna dalili au tabia ambayo ni hatari inabidi uwe makini.
Upendo wa kweli hauwezi kuwepo bila bonding ya kiroho.
Kutofautiana kiroho na kiimani ni moja ya sababu ya ndoa kuvurugika na hatimaye kuvunjika. Hivyo ni vizuri kupata data kamili kwa kuthibitisha imani yako na yake.
2. JE, UNAKUBALIANA NAYE KTK MAMBO YAKE?
Mtu ambaye kwake pesa na kazi ni namba moja yaani ni kitu cha kwanza, kwake bila hivyo hakuna maisha, yaani muda wake na akili yake ni pesa na kazi kwanza,
Then mambo ya michezo kama soka, au kushabikia tu michezo ni kitu cha pili, familia (mke au mume na watoto) ni kitu cha tatu kwake,
Na mwisho Mungu, yaani Mungu ni kitu cha ziada kwake, akiwa hana cha kufanya ndo anakumbuka mambo ya Mungu, Kama wewe ni dada ukapata kijana wa kiume wa aina hii kuendelea naye fikiria mara mbili.
Au mwanamke ambaye kwake kujiremba, kujisifia au kusifiwa na kuhudhuria sherehe (mama wa shughuli) kwake namba moja, then familia na Mungu baadae.
Kama ni kijana wa kiume binti wa aina hii fikiria mara mbili kabla hujaamua.
Kama ninyi ni Christians kitu cha kwanza ni kila mmoja kuwa na uhusiano na Mungu wake kwanza then familia yaani mke/mume na mtoto then kazi hii ni pamoja na kazi ya Mungu.
Hivi unaweza kwenda kuimba kwaya wakati mke au mume yupo kitandani anaumwa na hakuna mtu mwingine? Mlio kwenye ndoa tusaidie hapo!....