SANDUKU LA AGANO LINA UWEZO NA SIFA ZIFUATAZO:
Sanduku la Agano lina nguvu, hata ya kusababisha radi na ngurumo. UFUNUO 11:19…. [Kisha Hekalu la Mungu lililoko mbinguni likafunguliwa, na sanduku la agano lake likaonekana ndani ya hekalu lake. Kukawa na umeme, na sauti, na radi, na tetemeko la nchi, na mvua ya mawe nyingi sana.]….. Shida au kitu kilichokaa ndani mwako kwa maana kuwa kimefika na hakiwezi kutoka, Sanduku la Agano litasababisha tetemeko la radi na ngurumo na uwezo na mambo mapya yanakuja kwa Jina la Yesu. Pale ambapo madaktari wamesema hawawezi, tunalileta Sanduku la Agano liende kuangamiza vyote vinavokusibu kwa Jina la Yesu. Yeyote atakayemtumaini Yesu Kristo mchana wa leo ataona maisha mapya kwa Jina la Yesu.
Sanduku la Agano lina uwezo wa kuleta wokovu. Lina uwezo wa kutoa watu kwenye mikono ya maadui zao. Ndiyo maana wana wa Israeli waliweza kutoka mikononi mwa Wafilisti. Wana wa Israeli zaidi ya 400 waliuawa, lakini wazee wa Israeli wakakaa kikao kuitisha Sanduku la Agano liletwe mara moja. 1 SAMWELI 4:2-3…[2 Nao Wafilisti wakajipanga juu ya Israeli; na walipopigana, Israeli wakapigwa mbele ya Wafilisti; wakauawa watu wa jeshi lao lililokuwa uwandani wapata watu elfu nne. 3 Hata watu walipofika kambini, wazee wa Israeli wakasema, Mbona Bwana ametupiga leo mbele ya Wafilisti? Twende tukalilete sanduku la agano la Bwana toka Shilo hata huku, lije kati yetu, na kutuokoa katika mikono ya adui zetu.]… Ninakutangazia wewe ambaye umevamiwa na maadui wenye nguvu katika biashara/kazi yako/ndoa yako/masomo yako n.k kwamba, ninakuletea Sanduku la Agano katikati yako katika Jina la Yesu likuokoe na mikono ya maadui zako hao.
Linakausha maji ya mto uaendayo kasi katika maisha yako. Kuna mafuriko katika maisha ya mtu. YOSHUA 3:1-3…. [ Yoshua akaondoka asubuhi na mapema, nao wakatoka Shitimu, wakafika mto wa Yordani, yeye na wana wa Israeli wote, wakakaa hapo kabla ya kuvuka. 2 Ikawa baada ya siku tatu, maakida wakapita katikati ya marago, 3 wakawaamuru watu wote wakisema, Mtakapoliona sanduku la agano la Bwana, Mungu wenu, na makuhani Walawi wakilichukua, ndipo mtakapoondoka hapa mlipo na kulifuata.]… YOSHUA 3:14-17 … [Hata ikawa, hao watu walipotoka katika hema zao, ili kuvuka Yordani, makuhani waliolichukua sanduku la agano wakatangulia mbele ya watu, 15 basi hao waliolichukua hilo sanduku walipofika Yordani, na nyayo za makuhani waliolichukua sanduku zilipotiwa katika maji ya ukingoni, (maana Yordani hujaa hata kingo zake na kufurika wakati wote wa mavuno), 16 ndipo hayo maji yaliyoshuka kutoka juu yakasimama, yakainuka, yakawa chuguu, mbali sana, huko Adamu, mji ule ulio karibu na Sarethani, na maji yale yaliyotelemkia bahari ya Araba, yaani Bahari ya Chumvi, yakatindika kabisa; watu wakavuka kukabili Yeriko. 17 Na hao makuhani waliolichukua sanduku la agano la Bwana wakasimama imara mahali pakavu katikati ya Yordani; Israeli wote wakavuka katika nchi kavu, hata taifa lile lote likaisha kuvuka Yordani.]… Ile shida yako iloyokaa kama mto Yordani maishani mwako tunaitangazia kukauka kwa Jina la Yesu. Sanduku la Agano lilete ukombozi na kunyausha mafuriko yote ya taabu, shida, magonjwa, dhiki n.k kwa Jina la Yesu. Mtu yeyote anayezuia kama mto ufurikao, na anyauke kwa Jina la Yesu. Ni wakati wako leo kulibeba Sanduku la Agano na kusonga mbele kwa Jina la Yesu.
Sanduku la Agano lina uwezo wa kuangusha ngome. Farao huwa hachoki akeshaona umevuka, bali hutafuta mbinu nyingine. Leo Bwana lazima akuvushe na kuangusha ngome ya maisha yako. Yeriko ni kama ukuta wa kuzuia au kizuizi. Kuna ukuta umepangwa mahali kuzuia maisha yako. Ni kweli umeshavuka, lakini endapo pana ukuta mbele yako, bado utapata ugumu wa kusonga mbele. YOSHUA 6:1…. [Basi Yeriko ulikuwa umefungwa kabisa kwa sababu ya wana wa Israeli; hapana mtu aliyetoka wala hapana mtu aliyeingia.]… Wachawi wanao uwezo wa kufunga maisha ya mtu. Ni kweli Umejaribu kusoma sana, lakini bado haufanikiwi. Mwingine umejaribu kwenda kwa waganga wa kienyeji lakini haujafanikiwa. Huu ni ukuta wa maisha yako. Sanduku la Agano linao uweza wa kuiangusha hiyo Yeriko. YOSHUA 6:8 na 20…. [Basi ikawa Yoshua alipokwisha kusema na watu, wale makuhani saba, wenye kuzichukua tarumbeta saba za pembe za kondoo waume mbele za Bwana, wakatangulia, wakazipiga hizo tarumbeta; nalo sanduku la agano la Bwana likawafuata….. 20 Basi watu wakapiga kelele, na makuhani wakazipiga tarumbeta; hata ikawa, hapo watu waliposikia sauti ya tarumbeta hao watu wakapiga kelele kwa sauti kuu sana, na ule ukuta wa mji ukaanguka nchi kabisa, hata watu wakapanda juu, wakaingia katika mji, kila mtu akiendelea kukabili mbele; wakautwaa huo mji.]… Ninaitamkia Yeriko ya maisha yako, kusimama kwako ee Yeriko ku wapi? Leo tunaiteka Yeriko na kukusanya nyara kwa Jina la Yesu.
Sanduku la Agano linao uwezo wa kusababisha miungu na wakuu wote waliokithiri na kutaabisha maisha yako kuinama chini, kusujudu na kupasuka vipande vipande. Miungu yeyote iliyokaa maishani mwako, ninawatangazia mchana wa leo, miungu hiyo ivunjike na kuangamia kabisa kwa Jina la Yesu. 1SAMWELI 5:1-5…[Basi Wafilisti walikuwa wamelichukua sanduku la Mungu, wakaenda nalo kutoka Ebenezeri hata Ashdodi. 2 Wafilisti wakalichukua sanduku la Mungu, wakalitia katika nyumba ya Dagoni, wakaliweka karibu na Dagoni. 3 Na watu wa Ashdodi, walipoamka alfajiri siku ya pili, kumbe! Dagoni imeanguka chini kifudifudi, mbele ya sanduku la Bwana. Wakaitwaa Dagoni, wakaisimamisha mahali pake tena. 4 Hata walipoamka kesho yake asubuhi, kumbe! Dagoni ilikuwa imeanguka chini kifudifudi, mbele ya sanduku la Bwana; na kichwa chake Dagoni na vitanga vya mikono yake vyote viwili vimekatika, vipo vimelala kizingitini; Dagoni ikasalia kiwiliwili chake tu. 5 Kwa hiyo makuhani wa Dagoni, na mtu awaye yote aingiaye nyumbani mwa Dagoni, hawakanyagi kizingiti cha nyumba ya Dagoni huko Ashdodi, hata leo.].. Kama kuna mchawi aliyekutesa, mpelekee Sanduku la Agano mchana wa leo ili aanguke chini kwa Jina la Yesu.
Sanduku la Agano lina uwezo wa kuwapiga maadui zako wote kama Wamisri katika Jina la Yesu. Kabal ya Wana wa Israeli hawajatokaMisri, walipata mateso sana. 1 SAMWELI 4:8… [Ole wetu! Ni nani atakayetuokoa na mkono wa miungu hawa walio hodari? Hawa ndio miungu waliowapiga Wamisri kwa mapigo ya kila namna jangwani.]… Wakati wewe unaposonga mbele kwa Jina la Yesu, maadui zako, waliokutesa wakawa kama /Misri, wakapigwe kwa Jina la Yesu.
Sanduku la Aganolina uwezo wa kurudisha vyote vilivyoibiwa. 1 SAMWELI 4:9-11 .. [Iweni hodari, na kufanya kiume enyi Wafilisti, msije mkawa watumwa wa Waebrania, kama wao walivyokuwa watumwa wenu; fanyeni kiume, mkapigane nao. 10 Wafilisti wakapigana nao, Israeli wakapigwa, wakakimbia kila mtu hemani kwake; wakauawa watu wengi sana; maana katika Israeli walianguka watu thelathini elfu wenye kwenda vitani kwa miguu. 11 Hilo sanduku la Mungu Likatwaliwa; na Hofni na Finehasi, wale wana wawili wa Eli, wakauawa.]…
1 SAMWELI 5:6-12…[Lakini mkono wa Bwana ulikuwa mzito juu ya watu wa Ashdodi, akawaharibu, akawapiga kwa majipu, huko Ashdodi na mipakani mwake. 7 Kisha hao watu wa Ashdodi, walipoona ilivyokuwa, walisema, Hilo sanduku la Mungu wa Israeli halitakaa kwetu; kwa maana mkono wake ni mzito juu yetu, na juu ya Dagoni, mungu wetu. 8 Basi wakatuma watu waende kuwakusanya kwao mashehe wote wa Wafilisti, wakasema, Tulifanyieje sanduku la Mungu wa Israeli? Nao wakajibu, Sanduku la Mungu wa Israeli na lihamishwe liende Gathi. Wakalihamisha sanduku la Mungu wa Israeli. 9 Ikawa, walipokwisha lihamisha, mkono wa Bwana ulikuwa juu ya mji huo, kwa kuwafadhaisha sana; akawapiga watu wa mjini, wadogo kwa wakubwa, wakapatwa na majipu. 10 Basi, wakalipeleka sanduku la Mungu mpaka Ekroni. Ikawa, sanduku la Mungu lilipofika Ekroni, watu wa Ekroni walifanya kelele, wakasema, Wamelileta hilo sanduku la Mungu wa Israeli kwetu, hata kutuua sisi na watu wetu. 11 Kwa hiyo wakatuma watu waende kuwakusanya mashehe wote wa Wafilisti, wakasema, Liondoeni hilo sanduku la Mungu wa Israeli, liende tena mahali pake, ili lisituue sisi, wala watu wetu; kwa sababu kulikuwa na fadhaa kubwa sana mjini mwote; mkono wa Mungu ulikuwa mzito mno huko. 12 Na wale wasiokufa walipigwa kwa yale majipu; na kilio cha mji kikafika mbinguni.]… Ninaagiza, vile vyote vilivyoibiwa, Ndoa yako, kazi yako, mume wako, mke wako, watoto wako, biashara yako popote ilipowekwa, naamuru vyote viletwe kwa jina la Yesu.