Friday, 23 October 2015
UTAWALA WA KIKUHANI
Thursday, 22 October 2015
NGAO YA IMANI
Wednesday, 21 October 2015
RAI YANGU KWAKO MPIGA KURA
KURA KURA KURA
Hii ni haki mojawapo ya kufikia tamayi ya mashindano ya aina yoyote yale.
Ni wajibu wa kila mtu unapokuwa ktk mashindano ya aina yoyote yale
kimaisha
na kifikra lazima ufikie pahala ufanye uamuzi.
UAMUZI BORA ndio utakaotoa mstakabali mzima wa kile ulichokiamua
kutegemeana unataka au unahitaji nini
na kwa wakati gani.
KILA CHAGUO NA THAWABU YAKE
Kanisa la Kristo likaamua vema kumchagua Mungu kuliko mapokeo ya dini zao.
Sisi kama kanisa tunayo nafasi ya pekee
ktkt ya jamii hata kubatilisha mashauri
yaliyo potofu.
Ni tar. 25/10/2015
macho na masikio ya watanzania wote yatakuwa ktk msitu mnene totoro kufanya maamuzi
juu ya nani atayekuwa mbele yao kwa miaka mitano ijayo
kama Rais wa nchi yao.
Ni ushauri wangu tu kwako mwana wa MUNGU kuwa
usiyumbishwe na misisimko ya maneno ya
ushabiki bali
kaa utafakari kama mtu uliye mahali palipobomoka
uone utafanya nini.
Lakini pia ukimaliza kupiga kura ondoka kituoni nenda kamshukuru Mungu
na umsihi asimamie kusudi lake
na
ailinde kura yako dhidi ya waharamia wa kuiba haji za watu (kura).
NIKUTAKIE UCHAGUZI MWEMA NA AMANI YA KRISTO IPITAYO FAHAMU ZOTE IKUFUNIKE MPENDWA WANGU.
BY Ev. Elimeleck S Ndashikiwe
0767445846
Saturday, 17 October 2015
NGUVU YA IMANI ILIYO THABITI
IMANI THABITI tunazungumzia viwango vya kuwa na uhakika juu ya kile unachokijua kuhusu MUNGU na kazi zake.
EBRANIA 11:1 Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo,
ni hayana ya mambo yasiyoonekana.
Hiyo ndiyo maana halisi ya neno imani kwa mujibu wa maandiko.
Au twaweza kusema kuwa imani ni kuwa na uhakika wa yale mambo tusiyoyaona kwa macho ya nyama
bali ktk macho ya roho tunayaona na kuamini kuwa yapo.
Macho haya ya nyama huwa hayaamini hadi yaone kitu halisi (physically).
WAKO MASHUJAA WA IMANI
Kwa nini tunawaita mashujaa wa imani?
Ni kwa sababu waliiishi imani.
Hawakuyapenda maisha yao hata kufa kwa kule kuwa naimani.
EBRANIA 11:32-40 "Nami niseme nini tena? Maana wakati usingenitosha kuleta habari za Gideoni na Baraka na Samsoni na Yeftha na Daudi na Samweli na manabii;
33 ambao kwa imani walishinda milki za wafalme, walitenda haki, walifunga vinywa vya simba…………".
Hawa walistahili kabisa kuitwa hivyo kuwa
"Mashujaa wa Imani"
maana kwa kuijua imani
walifanya mambo makuu na ya ajabu.
Kumbe siri ya ushindi wao ni kwa sababu
walikuwa na imani iliyo thabiti.
Iko siri na nguvu ktk imani.
1YOH 5:4-5 "Kwa maana kila kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu,
huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu
hiyo imani yetu.
Siri ya ushindi ni imani iliyoko ndani yangu Elimeleck na wewe unayelitafakari NENO hili.
-Imani ina uwezo wa kushinda mateso
-Imani pia ni nguvu ya uumbaji EBR 11:3"Kwa imani twafahamu kuwa ulimwengu uliumbwa kwa NENO".
-Imani ni mlango wa sita wa fahamu alioongezewa mwana wa Mungu (macho, pua, sikio, ulimi na ngozi).
1KORINT 2:6-10 "Mambo ambayo jicho halikuyaona wala sikio kuyasikia
Mungu ametufunulia sisi kwa Roho".
Si kila mwanadamu ana imani
bali ni wale tu wanaomkiri Kristo kuwa ni mwana wa Mungu.
EBRANIA 11:2 Kwa imani thabiti waliyokuwa nayo wazee wetu,
walishuhudiwa kuwa wenye haki mbele za Mungu.
EBR 11:4 "UTOAJI"
Kumbe utoaji ni ibada kamili mbele za BABAyetu wa Mbinguni.
Kornelio ingawa alikuwa mshika dini lkn alipata kibali kwa Mungu kupitia utoaji.
IMANI ndiyo iliyomsukuma kumtolea Mungu
maana alijua kuwa Mungu ndiye mtoaji
MDO 10:1 Palikuwa na mtu mmoja Kaisaria, jina lake aliitwa Kornelio
, akida wa kikosi kilichoitwa Kiitalia, ……………!
Imani ni ushuhuda wa matendo makuu ya Mungu ktk maisha yetu ya kila siku.
Kutoa ni uthibitisho wa mtu kupenda kutoka moyoni
hatuwezi kumzuilia Mungu vile alivyotukirimia.
RBRANIA 11:5-6 "Kwa imani Henoko alihamishwa, asije akaona mauti , wala hakuonekana……………!"
6Pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu.
Henoki akampendeza sana Mungu kwa ile imani aliyokuwa nayo akaonekana kuwa shujaa na kuhesbiwa haki
kwa imani.
Mungu akamhamisha, akamnyakua (Henoko hakufa bali alitwaliwa).
Musa na Ibrahimu wakampendeza Mungu kwa vile walivyokuwa na imani
hata wakaitwa marafiki wa Mungu.
EBRANIA 11:32 Hawa mashujaa waliyashinda mateso kwa ile imani waliyokuwa nayo
wakimpendeza Mungu na wanadamu.
NB: USIFIE DHAMBINI
wako wazazi wako wa kiroho wanaweza kukusaidia ktk maisha yako kiroho.
Samsonianashindwa kuwasikiliza wazazi wake na kwenda kumuona mwanamke Delilla
aliyekuwa kahaba
ktk nchi yake mwenyewe.
Samsoni anaingia kwenye mtego wa kunaswa na Wafilisti wasiotahiriwa anakamatwa,
anatobolewa macho baada ya kuitoa siri na kunyolewa nywele zake zote.
Anapopata nguvu na kuziangusha zile nguzo
hasara inatokea na yeye mwenyewe anakufa.
soma WAAMUZI 14:1-3 Samsoni akaukataa ushauri wa wazazi wake.
MUNGU WANGU WA MBINGUNI AKUBARIKI MPENDWA WANGU
Somo hili limeandaliwa na Pastor GAYO MSAMATI
E.A.G (T) MBUYUNI DSM
Na kuletwa kwako nami
Ev. Elimeleck S Ndashikiwe
0767445846
0715445846.
B A R I K I W A.
Tuesday, 13 October 2015
KUSIFU NA KUABUDU
JINSI YA KUSIFU AU KUONGOZA SIFA NA KUABUDU VIZURI. A. SEHEMU YA KWANZA • Anza na nyimbo za kukutana na watu au akili yako pale ilipo au kukutana na mahitaji yako au ya watu pale walipo. • Mara nyingi watu huanzia katika hali ya kusongwa na shughuli za kila siku za maisha (masumbufu) • Hivyo anza na nyimbo au pambio zinazohusiana na kuwatia watu moyo pale walipo. • Imba nyimbo zenye kuamsha kiu na hamu ya watu juu ya kukutana na Mungu kwa msaada wa yale yanayowatatiza. • Ni kukutana na watu Misri (nje ya kambi au hekalu) walipo na kuwatia moyo kama Musa ili waanze safari ya kwenda kuelekea Kaanani (ndani ya hekalu) ambako ni nchi yenye asali na maziwa (wema na uzuri wa Mungu kwa msaada) kwenye faraja na amani ya kweli. • Imba nyimbo za kujipa au za kuwapa watu tumaini, furaha, na utayari wa kumwendea Mungu – kuiamsha kiu na hamu ya msaada wa Mungu. • Imba nyimbo za kujialika au kuwaalika watu ili kuanza safari ya kuuendea kiimani wema na uzuri wa Mungu. • Imba nyimbo za kuelezea Jinsi Mungu anavyoweza kukutendea au kuwatendea mema kama ukimwamini au wakimwamini na kumwendeayeye anayewapenda sana! • Nyimbo zinazoelezea au zinazokumbusha matendo makuu ya Mungu alivyokutendea, alivyowatendea, anavyoweza kukutendea au kuwatendea. • Katika nyimbo za injili; ni nyimbo za maisha ya Kikristo, Uinjilisti, na Kualikwa. • Zaweza kuwa ni nyimbo za haraka au taratibu. B. SEHEMU YA PILI • Nyimbo za kumfurahia, kumshangilia, na kumualika Mungu. • Ni kufanya watu waliokwishaingia Kanani /hemani / hekaluni – washangilie na kufurahia, na tena wakimshukuru Mungu kwa kuwafikisha salama (katika mji wa BWANA au nyumbani mwa BWANA. • Ni nyimbo zinazoufanya mioyo watu kujiachilia kwa Mungu waliyemwendea ili aonekane. • Ni kuyafanya mawazo yasiwe ya kujiangalia mwenyewe tena ila Mungu tu. • Ni kuyaelekeza mawazo kwa Mungu na kumshukuru kwa yale aliyoyatenda, anayoyatenda, na atakayoyatenda kwa ajili yetu. • Ni nyimbo zinazoelekeza zaidi kwa Mungu na vipawa vyake atoavyo kwa wanadamu. • Ni nyimbo kuelezea jinsi unavyomjua na jinsi anavyotenda, jinsi ulivyo ndani yake, raha na faida toka kwa Mungu, ili kwueafikisha na kuwaweka watu katika hali ya kuwa tayari kuingia rahani na kumuona Mungu. • Sehemu hii inabidi ichukue muda mrefu na wa kutosha sana, pamoja na uhamasishaji mwingi: ili watu waingie kikwelikweli katika raha na imani kwa Mungu; yaani, wautambue kikweli kweli ukuu, wema, ukarimu, na uzuri wa utukufu wa Mungu katika Kristo Yesu! C. SEHEMU YA TATU • Ni sehemu ya kumuinua Mungu, kumuabudu Mungu, na kujiachilia mbele zake. • Inahusu kuingia na kuwaongoza watu kuingia katika kumuinua Mungu na kisha kufikia katika kumuabudu Mungu Mkuu! • Ni hatua ambayo kusifu kwetu sasa husogea jirani na upendo wa Mungu, heshima, na hali ya kujiweka wakfu kitakatifu kwa Mungu. • Kasi ya mwendo wa nyimbo na vitendo hupungua hatua kwa hatua na kuwa wa taratibu na sauti ya kutulia sana. • Ni hatua ambayo umakini wako unatakiwa uwe kwa jinsi Mungu alivyokuwa, alivyo sasa, na atakavyokuwa kwa uzuri wake, ikuu wa Mungu, na upendo mkuu; na wa tabia zake za uungu ambazo ametushirikisha nasi pia. • Mara nyingine, ukimya na utulivu mtakatifu hulifunika kusanyiko la Mungu. Katika hali hii, inamaanisha kuwa kusifu kunahamia hatua nyingine, yaani, kutoka kumuinua Mungu na kuingia katika kuabudu. • Roho Mtakatifu huwaongoza watu sasa kuingia Patakatifu pa patakatifu. Kusifu sasa kunakuwa ni laini na kuingia katika uzuri wa kuabudu kwa kweli katika utakatifu. • Katika hatua hii unatakiwa (mwongozaji wa sifa) kuwa makini sana kuangalia utembeaji wa Roho Mtakatifu na kusikiliza vile atakavyo au atoavyo maelekezo. • Ni vizuri kuwaongoza watu kwa upole na pia kuwaelimisha kwa maneno ya uangalifu sana ya kuwa sasa wanahamia hatua nyingine. Chagua maneno ya busara na kiasi, usiseme maneno mengi au yale ya kuwahamisha watu mbali na utulivu wa kuabudu, bali yenye kuwasaidia na kuwahamasisha kububujika zaidi. a. Kumbuka: Usimzimishe Roho Mtakatifu; Watu wanapobubujika, nyamaza na uwaache watu wabubujike katika Roho, umakini wako na wa watu unatakiwa uelekezwe kwa Mungu pekee, na si kwa kiongozi wa kuabudu au muziki tena! RUHUSU WINGU LA UTUKUFU WA MUNGU KUSHUKA. • Kadiri tuisogeleavyo sehemu takatifu sana, ndivyo uimbaji wetu unatakiwa kuwa ni wa kuhusu sana Mungu mwenyewe (Wewe ni Mungu … ) • Unakuwa upo mbele za Mungu na uwepo wake. • Kumbuka uimbaji ulianzia nje ya kuta kwa kuimba kuhusu sisi wenyewe na mahitaji yetu na hisia zetu au hau yetu juu ya Mungu; sasa safari ya uimbaji mwishowe tunaimalizia ndani, patakatifu pa patakatifu, kwa kumuabudu Mungu. • Ni sehemu ya uwepo mtakatifu wa Mungu. • Katika hatua hii, Mungu na malaika zake watakatifu huwahudumia watu. JINSI YA KUPANGILIA PAMBIO KATIKA KIPINDI CHA SIFA 1. PAMBIO ZA KUFARIJI a. KUONYA b. KUTIA MOYO c. KUKEMEA d. KUHUBIRI 2. PAMBIO ZA KUSIFU / ZINAZOELEZEA JINSI : a. ALIYOTATENDA / ALIVYOTENDA / ALIVYOKUTENDEA/ ALIVYOWATENDEA b. ANAYOTATENDA / ANAVYOTENDA / ANAVYOKUTENDEA / ANAVYOWATENDEA c. ATAKAYOTENDA / ATAKAVYOTENDA / ATAKAVYOKUTENDEA / ATAKAVYOWATENDEA 3. PAMBIO ZA KUMUINUA MUNGU a. KUMUELEZA MUNGU MWENYEWE UNAVYOMFAHAMU b. KUMUELEZA MUNGU TABIA NA SIFA ZAKE c. SI KUELEZA ALIYOYATENDA, BALI JINSI MUNGU ALIVYO 4. PAMBIO ZA KUMUABUDU MUNGU a. KUMUELEZA MUNGU JINSI UNAVYOJISIKIA KUWA NAYE b. KUMUALIKA MUNGU AHUSIKE NAWE c. ELEZA HISIA ZAKO SI ZA WENGINE d. UTAKAVYOJISIKIA KAMA UKIENDELEA KUWA NAYE MILELE i. UPENDO WAKO KWAKE, Sifa zake na kazi zake. ii. FURAHA YAKO KWAKE Sifa zake na kazi zake. iii. AMANI YAKO KWAKE Sifa zake na kazi zake. iv. UZIMA WAKO KWAKE Sifa zake na kazi zake. v. NGUVU WAKO KWAKE Sifa zake na kazi zake. vi. RAHA YAKO KWAKE Sifa zake na kazi zake. vii. UJASIRI WAKO KWAKE Sifa zake na kazi zake. BADHI YA MFANO WA NYIMBO / PAMBIO NA JINSI YA KUPANGILIA (LABDA ROHO ASEME VINGINEVYO NA WEWE!) (I) NYIMBO / PAMBIO ZA KUFARIJI 1. TWENDE JUU SAYUNI X 3 MJI WAKE BWANA 2. TEMBEA NAYESU 3. WPTE WALIOMPOKEA 4. AMINI YESU ANALEA 5. MCHAKA MCHAKA MKIMBILIE YESU 6. MWAMINI X 3 MWOKOZI X 2 7. KIMBILIA KWAKE YESU UTAPONA. 8. NIPE MAJI NINYWE, MAJI YA UZIMA. 9. ONJENI KUONE, MUNGU YU MWEMA 10. SIMAMA TUKAIMBE PARADISO 11. NIMPELELEZE NANI FURAHA YA MBINGUNI 12. JINA LANGU LIKO KULE X 3 MBINGUNI 13. SAYUNI X 4 NINAIMANI YA KWAMBA NITAFIKA 14. (MIKONONI, MIKONONI) X 2 TUKIWA SAFARINI, YESU NDIYE KIONGOZI 15. NJIA YEMBAMBA X 2 NITAIFUATA, NIWEZE KUFIKA MBINGUNI 16. WAAMBIENI WATEULE WAJIPE MOYO, BWANA AMEKUSUDIA KUWAPA MEMA 17. JINA LAYESU, NI NGOME YANGU. 18. MWAMBIE YESU X 2 ANAWEZA YOTE 19. YUKO MUNGU MMOJA MBINGUNI YEYE NI MWAMBA 20. AINULIWE MUNGU WETU LEO, AINULIWE, BWANA WA MABWANA 21. SIMAMA USICHELEWE 22. SIMAMA IMARA UMTETEE BWANA 23. NATAMANI NIENDE PARADISO KWA BWANA 24. MSALBA MBELE DUNIANYUMA 25. NINAMJUA ALIYE MWAMBA. 26. NYIMBO ZA KITABUNI - NYIMBO ZA INILI UKURASA WA 91-11 (II) NYIMBO / PAMBIO ZA KUMSIFU MUNGU 1. JINA LAKE IMANUELI HOSANA 2. YU MWEMA BWANA WANGU YESU, YU MWEMA! 3. NIMWUONA MWOKOZI, NIMEMWONA AHA! 4. MSHUKURUNI BWANA KWA KUWA NI MWEMA 5. NISEME NINI BWANA X 3 YOTE NINASHUKURU 6. YESU NI WANGU WA UZIMA WA MILELE 7. WATU WOTE WAMTUKUZE BWANA 8. TUIMBE HALELUYA HOSANA NA YAHWE 9. EE BABA X 3 POKEA SIFA 10. LEO NI SIKU NGEMA TUTAMUONA BWANA 11. MUNGU YU MWEMA X3 KWANGU 12. NINAMJUA ALIYE MWAMBA, ALIYENIOKOA 13. MWIMBIENI BWANA WIMBO MPYA, KWA MAANA AMETENDA MAMBO YA AJABU 14. SIJAMPAT RAFIKI WAKUFANANA NA YESU 15. SIJAONA KAMA YESU 16. MWAMBA NI YESU… 17. (AIME, AIME, AIME!) X 2 18. JINA LA YESU, LIBARIKIWE X 3 NI JINA LA NGUVU ZOTE! 19. NI BWANA WA WATU WOTE 20. NI YEYE YULE X 3 ALIYENIOKOA 21. MSALABA WA YESU, NI MSALABA UMENIOKOA DHAMBI, HALELUYA 22. ALIUBEBA MSALABA KUELEKEA GOLIGOTA 23. POPOTE ALIENDA ALITENDA MEMA 24. NAMPENDA YESU WA GALILAYA AMETENDA MAKUU MOYONI MWANGU 25. AMEJAA NEEMA YESU AMEJAA NEEMA 26. NI WA NEEMA X 3 BABA! 27. HAKUNA WA KUFANANA NAYE! 28. MAHALI NIKEFIKA NIMEONA MKONO WAKO, 29. YESU ANAWEZA YOTE 30. HOSANA MWANA WA DAUDI 31. BABA YETU WA MBINGUNI, MAPENZI YAKO YATIMIZWE! 32. PALE KALIVARI YOTE YALIKWISA 33. NIMEUONA MKONO WA BWANA NIMEUONA! 34. KAMA SI WEWE BWANA NINGEKUWAJE LEO 35. NANA MWANAUME KAMA YESU HALELUYA 36. SIFUNI – OH IMBA IMBA SIFUNI 37. SIFU MUNGU HALELUYA, SIFU MUNGU AME! 38. HAKUNA KAMA YEHOVA X 3 HAKUNA KAMA YEHOVA YIRE! 39. ALIPO YESU YOTE YANAWEZEKANA (III) NYIMBO ZA KUMUINUA MUNGU NA KUABUDU. 1. WEWE NI MUNGU MKUU, WAWEZA YOTE, … 2. HAKUNA MUNGU KAMA WEWE … 3. BWANA WA MABWANA, MUNGU WA MIUNGU, ALFA NA OMEGA …. 4. UMEINULIWA X 3 JUU … 5. HAKUNA, MUNGU KAMA WEWE, HAKUNA POPOTE… 6. BWANA UMETAMALAKI, HAKUNA ALIYE KAMA WEWE. 7. UNASTAHILI KUABUDIWA … 8. NASEMA ASANTE X 3 EWE MUNGU WANGU. 9. NISEME NINI BWANA X 3 YOTE NINASHUKURU. 10. BABA WA MBINGUNI HAKUNA KAMA WEWE. 11. NAFSI YANGU YAKUTAMANI, ROHO YANGU YAONA KIU, KAMA AYALA… 12. MUNGU WETU, TUNAKUABUDU. 13. BABA WA MBINGUNI, MUNGU MTAKATIFU, TUNAUNGANA NA MASERAFI MAKERUBI KUKUABUDU. 14. HAKUNA X 3 KAMA WEWE! HAKUNA, HAKUNA, ALIYE KAMA WEWE! 15. BWANA, UMETAMALAKI, HAKUNA ALIYE KAMA WEWE. 16. ZA KITABUNI - NYIMBO ZA INILI UKURASA WA 19-42.
UTUMWA WA KIPEPO
Shalom mwana wa MUNGU upendwaye sana!
Natumai ya kuwa uko mzima wa afya kabisa
ukiwa unautafakari ujumbe huu.
Si ujumbe rahisi kabisa kama unavyoweza kuudhania.
KOLOSAI 1:13 "Naye alituokoa ktk nguvu za giza
akatuhamisha na kutuingiza ktk ufalme wa mwana wa pendo lake...."
Ni dhahiri kwamba kuokolewa kwetu tumeondolewa ndani ya ufalme wa shetani
tukaingizwa ktk ifalme wa MUNGU BABA.
Hivyo shetani hakufurahia kuona sisi tunakuwa waasi ktk ufalme wake,
anajitahidi kadri awezavyo kutufuatilia
na kuoigana nasi ktk ulimwengu wa roho.
Hivyo basi silaha mara zote anazozitumia ni kuhakikisha anauvunja uhusiano wetu na Mungu wetu
kwa kuyatumia
mapepo (wafuasi wake), kuja kuwatesa watu wa MUNGU.
Maandiko yanasema "mpingeni shetani naye atawakimbia ninyi"
lkn wakati mwingine huwa inaachiliwa roho ya hofu ndani ya mtu
na kujikuta
unajiona kuwa huwezi.
Lakini kumbe tunayaweza yote ktk yeye aliyetupenda na atutiaye nguvu.
MDO 1:8 "Lakini mtapokea nguvu akiwajilia juu yenu Roho Mtakatifu......."
Kunbe Roho Mtakatifu anatutia nguvu ya kuweza kupambana na kila roho inayojiinua juu ya elimu ya MUNGU.
Kwa nini watu wanaendelea kuteswa na mapepo?
unaweza ukajiuliza kuwa inakuwaje mtu yuko kanisani lkn bado anasumbuliwa na nguvu za giza.
Hii mara nyingi huwa inatokana na mtu binafsi kushindwa
kujitambua na
kutojitoa dhabihu kama chombo cha BWANA
anajikuta yeye kila kitu kwake ni kawaida tu.
Mtu mwenye mapepo sio lazima umkute anapiga kelele,
analia,
anagombana au
anaombewa ndipo uone anaanguka!
HAPANA.
HAPA ZIKO ISHARA ZA KUMTAMBUA MTU MWENYE MAPEPO
1.Hasira zisizo za kawaida
Unakutana na mtu yeyote unayemfahamu au hata usiyemfahamu
anakuwa na
hasira zisizo za kawaida lama ulivyomzoea.
hapo lazima direct
utambue kuwa huyu mtu kapatwa na pepo la hasira
MATH 8:28-29
tunaona mapepo yaliyotokea makaburini
yakawa ndani ya wale watu wawili wakashikwa na hasira wakawa wakali mno.
MHUB 7:9 & YAK 1:19-20
"Hasira ya mwanadamu hairwndi haki ya MUNGU"
3.Kuwa na uchungu usio wa kawaida
Uchungu wa kipepo unaamvatana na roho ya kutokuwa tayr kusamehe wala kuachilia,
pepo hao huchochea uxhungu moyoni
EFES 4:26-27 "Usiwe na hasira shina la uchungu lisije likachipuka".
Shetani anaitumia mbinu hii ili apate kukushambulia nyuma ya uchungu kwa magonjwa, chuki, kiburi n.k.
EBR 12:14-15 "Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote......"
kuwa na amani na watu wote si kazi rahisi kabisa.,
wengine wanashindwa kuwa na amani na mtu kwa sababu uchungu unatia unajisi.
3. Kuwaza mawazo mabaya
Hapa huja mawazo ya kujisikia na kutamani kufanya mapenzi ya mwili tu
kama ngono, kujiua,
wizi, ushirikina, visasi na mengineyo lama hayo
hii ni kwa sababu nyuma kuna pepo la mauti!
Pepo huyu hukuumbia tabia ya kusahau unaweza ukapanda gari bila kujua linaelekea wapi
au unaweza kuona maono ya kipepo
unamwona mtu yuko uchi wa nguo kumbe amevaa nguo.
AYUB 31:1 Hapa Ayubu si kwamba hakuwa anamwangalia huyu mwanamke kwa macho bali alikataa kumtazama kwa mawazo.
MATH 5:27-29 "Dhambi ya zinaa huanzia ktk mawazo ya mtu,
tendo la ndoa au zinaa ni utimilifu wa mawazo.
4. Kuwaza matusi
Hii ni dalili ya pepo!
Kila mtu huwaza na kujikuta anatukana moyoni hata kama yuko peke yake
na
wakati mwingine humtukana hata MUNGU.
mfano wakati wengine wanaimba na kuabudu wew unawaza tu kutukana.
UFU 16:10-11 "Wakamtukana Mungu wala hawakuyatubia matendo yao......".
Kusema maneno yasiyofaa kwa Mungu ni sawa na kumtukana Mungu (pepo aliyemo ndani yako ndiye anayetukana).
UFU 16:13-14 "Kwa sababu ya uchungu uliokuwamo ndani yao, wakamtukana MUNGU......".
(21) Wanadamu wakamtukana Mungu kwa sababu ya ile mvua ya mawe.
5. Kutamani kula udongo au mchele mkavu
Kwa asili udongo ni chakula cha laana
kwa kuwa ni chakula alichoamriwa kula shetani maisha yote MWA 3:14.
Pepo huwapelekea wanadamu kula udongo au mavumbi
mfn wanawake.
Baada ya anguko la mwanadamu pale Edeni,
aliyeamriwa kula udongo ni nyoka (shetani),
si ADAMU wala EVA.
NB:Hususani akna mama msishabikie kubugia bugia udongo wa aina yoyote ile ni laana.
NADHANI UTAKUWA UMEJIFUNZA KITU HAPA
MPENDWA WANGU.
NAKUPENDA SANA SANA SANA
Ni mimi rafiki yako mpendwa
Ev. Elimeleck S Ndashikiwe
elimelck@gmail.com
0767445846
0715445846.
Monday, 12 October 2015
NENO LA MUNGU
UWEZA ULIO KATIKA NENO LA MUNGU Uwezo wa kukuongoza katika njia sahihi. “neno lako ni taa ya miguu yangu, na mwanga wa njia yangu” Zaburi 119:105 ,
neno linatuonyesha tunapoelekea, linatuongoza kutenda kwa usahihi kama vile nchi bila katiba inapotea, ndivyo mtu anayemwamini Yesu kutokuwa na neno la Mungu moyoni mwake! lazima atapotea! Mungu akamwambia Joshua “kitabu hiki cha torati kisitoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku…ndipo utakapoifanikisha njia yako…” Joshua 1:8.
Ni kwa kufuata Neno la Mungu ndipo mtu anaweza ifanikisha njia yake! Uwezo wa kutufanya hai. “maana mtu hatoishi kwa mkate tu bali kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu” Mathayo 4:4,
neno limejaa uwezo wa kutufanya hai, kama vile mwili bila chakula unakufa ndipo mtu aliye na Yesu bila neno lake lazima atakufa kiroho. Neno la Mungu linatupatia nguvu ya kuishi bila neno la Mungu maisha yetu ya kiroho yamo hatarini,
Petro akamwambia Yesu “basi twende kwa nani wewe unayo maneno ya uzima” maneno ni uzima! Uwezo wa ushindi dhidi ya shetani. “tweni upanga wa roho ambao ni neno la Mungu” Waefeso 6:17b ,.
Mkristo asiye na neno la Mungu ni sawa na mwanajeshi asiye na silaha alafu yuko vitani, neno la Mungu ni salaha kuu dhidi ya shetani “je, neno langu si kama moto, asema Bwana, na kama upanga ukatao kuwili?” neno la Mungu ni ushindi mkamilifu dhidi ya shetani! Tukijua kulitumia ni ushindi mkamilifu! Uwezo wa kupokea kutoka kwa BWANA. “…….na maneno yangu yakikaa ndani yenu , ombeni lolote mtalipata” Yohana 15:17.
Neno likijaa ndani yetu tutajua jinsi ya kuomwomba Mungu sawa sawa. Ni muhimu kuishi kwa kusoma neno la mungu ili tuombe sawa na mapenzi yake . Uwezo wa kuumba. “kwa imani twafahamuya kuwa ulimwengu uliumbwa kwa NENO LA MUNGU….” Waebrania 11:3.
“maana yeye alisema ikawa,NA YEYE ALIAMURU IKASIMAMA” Zaburi 33:9 neno lina nguvu ya kuumba inategemea unaamuru nini na kwa uweza gani! Hivyo hata ukipita katika ugonjwa unaweza ukasimama mwenyewe ukaamuru kwa uweza wa kuumba na ugonjwa ukaondoka. Yesu alikuwa anatumia maneno kama haya kuponya watu “nataka takasika” uwe mzima” “mtoke mtu huyu” haya ni maneno ya kuumba kama Mungu alivyo tamka “iwe nuru ikawa n.k.” mwanzo 1:1-.. . Ni Mungu mwenyewe. “hapo mwanzo kulikuwa na neno , naye neno alikuwako kwa Mungu naye neno alikuwa Mungu” Yohana 1:1 ,.
Nine la Mungu ni Mungu mwenyewe, kwasababu huwezi kumtofautisha mtu na neno lake , Mungu ni neno na ndio maana sisi tukilishika neno lake tunakuwa washiriki wa tabia ya kiungu “…tupate kuwa washiriki wa tabia ya kiMungu…” 2Petro 1:4,. The Amplified Bible says that “ sharer (per-takers) of divine nature” na kwa namna hiyo tunaitwa miungu “mimi nimesema ndinyi miungu,na wana waa aliye juu wote pia..” Zaburi 82:6. Kumbe tunapata uwezo wa kuumba kwasababu na sisi ni mi ungu kwa kulishika neno lake! Tunapataje uwezo wa Neno la Mungu! “hapo mwanzo kulikuwa na neno, naye neno alikuwako kwa Mungu naye neno alikuwa Mungu,
Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu. Vyote vilifanyika kwa yeye; wala pasipo yeye hakikufanyika chochote kilichofanyika. Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima , nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu. Nayo yang’aa gizani wala giza halikuiweza!” Yohana 1:1-5 ,. Mambo ya kujifunza kutoka kwenye hilo andiko!
1.) Neno la Mungu ni Mungu mwenyewe hivyo si la kulifanyia mzaha, kamwe huwezi kumtenganisha mtu na neno lake , ndiyo maana hata Mafalisayo walimtega Yesu kwenye maneno yake ili wamkamate “wakamviziavizia …ili wamnase kwenye maneno yake, wapate kumtia kwenye enzi ya mamlaka ya liwali” Luka 20:20. Neno la Mungu ni Mungu mwenyewe.
2.) Tunajifunza jinsi ya kulitumia neno la Mungu , biblia inasema “ ndani yake ndimo ulimokuwa uzima” ni muhimu kujua kusikia neno tu haitoshi bali kujua kilichoko ndani ya neno hilo, Neno la Mungu lina uzima ndani yake ambao huwezi kuupata kwa kusikia peke yake! Ni kweli kusikia neno la Mungu kunaleta imani(warumi 10:17) lakini imani inatakiwa kuwekwa kimatendo hapo inamaanisha udhihirisho wa neno ulilolipokea na hapa ndipo wakristo wengi wanashindwa kujua na kubaki kumlaumu MUNGU!
3.) Tunaweza kuupokea ule uzima ulio katika neno , kwa kutafakari neno, kivipi basi? Tuchukue mfano wa tundo kama chungwa huwezi kula pamoja na maganda yake ni lazima kumenya maganda kwanza ndipo ule , sasa chungwa ni kama neno la Mungu na maganda ni tafsiri za kibinadamu, Kutafakari neno ni kumruhusu Roho mtakatifu akufundishe kama tulivyoona hapo juu kuwa NENO NI MUNGU, na hakuna anayejua mafumbo ya Mungu isipokuwa Roho mtakatifu, (1wakorintho2:10-11) hivyo Roho hutufunulia kwa kutafakari neno la Mungu Daud akasema “na sheri huitafakari mchana na usiku”
4.) Je wajua kuto kutafakari neno la Mungu ni kumzimisha Roho wa Bwana? Biblia inasema “ tusimzimishe Roho wa Bwana” 1Thesalonike 5:19 ,. Kuto kutafakari neno la Mungu ni kumzimisha Roho wa Bwana, kwa sababu haumruhusu yeye kukufundisha na huku biblia inasema “Roho atatufundisha kuyashika yote” sasa ni Muhimu kutafakari neno la Mungu kwa kufanya hivyo tunaruhusu uwezo wa Neno la Mungu kutenda kazi katika maisha yetu!
5.) Sasa kwa kutafakari ndipo unapo ingiza uzima kwenye maisha yako, kwenye kazi yako , mafanikio yako (Joshua 1:8) n.k. iyo ndiyo Nuru inayo ng’aa gizani hata giza na wakuu wake hawataiweza kabisa! Jifunze kujiwekea Ratiba ya kusoma neno la Mungu kila siku na kutafakari(meditation) unahusianisha na maisha na kumwomba Roho mtakatifu akufundishe ! MAY GOD BLESS YOU
EV. ELIMELECK NDASHIKIWE
NGAO YA IMANI
IMANI YA UKRISTO
"Katika nyakati hizi za Agano Jipya, imani ya UKRISTO imejengeka kutoka kwa Yesu Kristo ambaye wafuasi Wake wote amewafanya kuwa WATEULE Wake kwa kuwajaza Roho Mtakatifu ambaye ni mfano wa mafuta waliyokuwa wanapakwa wateule
wa Mungu enzi za nyakati za Agano la Kale."
Waswahili husema kwamba: "Ukweli usioujua hauwezi kukusaidia." Nami pia nasema kwamba: "Uongo usioujua ni vigumu kuuepuka." - na: Mwinjilisti Masanja Sabbi.
Hebu soma kwa makini mafundisho haya ili upate kuifahamu iliyo kweli. Mpenzi msomaji,
bila shaka unayo shauku kubwa sana ya kujua ukweli uliojificha katika imani ya Ukristo kwani ni watu wengi tunawasikia wakijiita na kuitwa wao ni "Wakristo" lakini yawezekana wewe haujui nini hasa maana ya neno "WAKRISTO"; na pia chimbuko na asili ya imani hii.
Bila shaka hapa umefungua ukurasa sahihi kabisa na utarajie kujifunza mengi na kweli tupu. Kabla hatujafika mbali katika kujifunza napenda kukupa taadhali / angalizo hili: Mara nyingi katika kujifunza unaweza ukapokea kitu kilicho kipya kwako na wakati mwingine ujumbe huu ukakuudhi kwa sababu umefichua machukizo yaliyojificha katika imani yako au dhehebu lako. Elewa kwamba; Huduma hii haipo kwa lengo la kuitukana dini au dhehebu fulani, bali dhumuni kuu la huduma hii ni kufundisha jinsi kweli ilivyo pasipo kificho. Napenda nikushauri hivi: Lengo la kujifunza ni kutaka kujua / kuelewa kweli yote. Lakini zingatia kwamba: "Hauta elewa mpaka pale utakapo funguka akili; na hautafunguka akili mpaka pale utakapoikubali kweli." Na sasa unaweza ukachukua kalamu na karatasi, au daftari ili uandike point za muhimu unazojifunza ambazo utakuwa ukijikumbushia yale uliyojifunza pindi upatapo nafasi. Baada ya utangulizi huo; napenda tujifunze kwa kina somo letu linalohusu IMANI YA UKRISTO. Hebu tuanze ifuatavyo: IMANI YA UKRISTO CHIMBUKO NA ASILI YA UKRISTO. UKRISTO unatokana na neno KRISTO. Ni sawa sawa na kusema UTANZANIA unatokana na neno TANZANIA kwa sababu UTANZANIA maana yake ni utamaduni wa ki-Tanzania. Unapotamka neno KRISTO unakuwa umetamka kwa kutumia lugha ya Kiyunani (Kigiriki) lakini chimbuko na asili ya neno hilo ni neno MASIHI ambalo ni la lugha ya Kiebrania. Maneno yote hayo mawili; "KRISTO" na "MASIHI" yote yana maana moja ambayo kwa Kiswahili chepesi tafsiri yake ni Mteule wa Mungu au Mpakwa mafuta wa BWANA Mungu. Imani hii ya UPAKWA MAFUTA (UKRISTO au UMASIHI) inatokana na desturi ya Wayahudi katika nyakati za Agano la Kale hususani pindi miongoni mwao walipokuwa wanateuliwa watu kufanya kazi zifuatazo: i/: KUHANI. Kuhani ni mtu aliyeteuliwa na Mungu kwa ajili ya kufanya huduma ya upatanisho kati ya Mungu na wanadamu. Makuhani walikuwa ni wakuu wa dini ambao kazi yao ni kuwapa watu maagizo ya Mungu au miungu yao (hata wapagani walikuwa na makuhani kwa ajili ya miungu wao. Soma Mwanzo 41:45; 47:22 hao walikuwa makuhani wa Misri) na pia makuhani walikuwa watoaji wa sadaka / kafara ambazo zimeletwa na watu kwa lengo la shukrari, au upatanisho wa dhambi zao kwa Mungu, au miungu wao. UFAFANUZI - ZINGATIA HILI: Utofauti kati ya "Mungu", na "mungu" - unapoandika kwa kuanza na herufi kubwa "M" yaani "Mungu" unakuwa umemtaja Mungu muumba wa vitu vyote; lakini endapo ukiandika kwa kuanza na herufi ndogo "m" yaani "mungu" hapo unakuwa umetaja "miungu" kwa maana ya watu, mizimu, pepo wachafu, au Shetani. Uwe makini sana utumiapo majina hayo. Pia uonapo katika Biblia Takatifu pameandikwa kwa herufi zote kubwa neno "BWANA" unatakiwa ujue hapo limetumiwa badala ya jina YEHOVA ambalo ndilo jina Mungu alijitambulisha kwa Musa (Kutoka 6:2,6). Hivyo basi; Mungu aliamuru makuhani wawekwe wakfu kwa kupakwa mafuta kichwani. Tunaona Mungu anamwagiza Musa kwamba: "Nawe umlete Haruni ndugu yako karibu nami, na wanawe pamoja naye, miongoni mwa wana wa Israeli, ili anitumikie katika kazi ya ukuhani... nawe watie mafuta, na kuwaweka kwa kazi takatifu, na kuwatakasa, ili wapate kunitumikia Mimi katika kazi ya ukuhani." - (Kutoka 28:1, 41) Hapo tunaona Mungu anamwambia Musa kwamba: "...watie mafuta..." Musa alichukua mafuta na kuyatia kichwani mwao kwa ishara ya kuwa watu hao wamepewa kibali na Mungu cha kumtumikia kwa huduma ya ukuhani. Watu wengine waliopakwa mafuta kwa ishara ya kupewa kibali na Mungu kwa kazi husika ni hawa: ii/: WAFALME WA ISRAELI. Tunaposoma Biblia Takatifu tunaona pia wafalme wa Israeli nao waliteuliwa kwa kupakwa mafuta matakatifu kichwani mwao. Tukimtazama mfalme Sauli tunaona Biblia inatuambia kuwa yeye ni mpakwa mafuta wa Mungu, yaani: "...masihi wa BWANA..." - (1 Sam 24:10). Wakati mfalme Sauli anawekwa wakfu, Biblia Takatifu inatuambia: "Ndipo Swamweli akatwaa kichupa cha mafuta, akayamimina kichwani pake, akambusu, akasema,.. Nawe utawamiliki watu wa BWANA... hii itakuwa ishara kwako ya kuwa BWANA amekutia mafuta..." - (1 Sam 10:1) Pia tukija kwa mfalme Daudi tunaona naye pia alipakwa mafuta. Hapa tunaona Mungu anamwambia Samweli mtumishi Wake kwamba Samweli aende akampake Daudi mafuta ili awe mfalme wa Israeli. Tunaona Mungu anamwambia Samweli: "...Ondoka, umtie mafuta; maana huyu ndiye. Ndipo Samweli akaitwaa pembe yenye mafuta, akamtia mafuta... na Roho ya BWANA ikamjilia Daudi kwa nguvu tangu siku ile..." - (1 Sam 16:12-13) Vile vile mfalme Sulemani naye alipakwa mafuta kwa ishara ya kuteuliwa na Mungu kuwa mfalme wa Israeli. Biblia Takatifu inasema kwamba: "Na Sadoki, kuhani, akaitwaa ile pembe ya mafuta... akamtia Sulemani mafuta... Na watu wote wakasema, Mfalme Sulemani na aishi!" - (1 Wafalme 1:39) Pia tunamwona Mungu anamwambia nabii Eliya kumpaka mafuta Yehu awe mfalme wa Israeli - (1 Wafalme 19:16). Watu wengine waliokuwa wanapakwa mafuta kwa ishara ya kuteuliwa na kupata kibali kwa Mungu kwa ajili ya kazi maalumu, ni hawa wafuatao: iii/: MANABII. Upo wakati pia manabii nao waliteuliwa na Mungu kwa ishara ya kupakwa mafuta. Biblia Takatifu inatueleza jinsi Mungu alivyomwambia nabii Eliya kwamba: "...Elisha mwana wa Shafati wa Abel-Mehola mtie mafuta awe nabii mahali pako." - 1 Wafalme 19:16. Watu hao, yaani makuhani, wafalme wa Israeli, pamoja na manabii walikuwa wanateuliwa kwa kupakwa mafuta ambayo ni ishara ya kupata kibali mbele za Mungu kwa ajili ya kufanya kazi waliyopewa. Vile vile haikuwa tu mtu ye yote anaweza kuwapaka mafuta wateule hao, la hasha! Kazi hiyo ilifanywa na watumishi wa Mungu; nao hao watumishi hawakupaka watu ovyo ovyo bali waliongozwa na Mungu mwenyewe kwa agizo Lake. Mungu ndiye aliyechagua wateule Wake. Hiyo ndiyo chimbuko la imani ya UKRISTO, au UMASIHI, au UPAKWA MAFUTA, au UTEULE. Hadi hapo tunakuwa tumefahamu kwamba UKRISTO haukuanzia katika huduma ya Bwana Yesu kama mtu hapa duniani, bali UKRISTO ulikuwepo hata kabla ya Yesu kuja duniani kama mwanadamu. Katika nyakati za Agano la Kale huo UKRISTO au UMASIHI au UPAKWA MAFUTA au UTEULE ulikuwa wa mtu mmoja mmoja katika jamii ya Waisraeli; lakini, bado tunaona wana wa Israeli walikuwa wanatazamia kuja kwa MASIHI Mkuu yaani KRISTO Mkuu ambaye atawatawala watu wa Mungu, atakuwa kuhani kwa kufanya upatanisho, atakuwa nabii kwa kuyasema yale ayaonayo kwa YEHOVA, na pia MASIHI (yaani MTEULE) huyo atatawala milele - (Zaburi 89:3-4; Isaya 9:2-7; 11:1-5; Yeremia 23:5; Ezekieli 34:23-26; Mika 5:2) na unabii wote huo ulikuja kutimia katika Agono Jipya ambalo linamtaja wazi wazi kuwa Yesu ndiye Masihi Mkuu ambaye Yule walimtazamia atakuja - (Yohana 1:41-42). Yesu ndiye "...Mchungaji mmoja..." - (Ezekieli 34:23), ambaye ni Kuhani Mkuu - (Waebrania 7:26), na pia ndiye Masihi Mkuu - (Dan 9: 25-27). Tukisoma Biblia ya King James hapo andiko la Danieli 9:25 inamtaja Yesu kuwa ni Masihi Mwana wa Mfalme ("...Messiah the Prince...") Sasa basi; katika nyakati hizi za Agano Jipya, imani ya UKRISTO imejengeka kutoka kwa Yesu Kristo ambaye wafuasi Wake wote amewafanya kuwa WATEULE Wake kwa kuwajaza Roho Mtakatifu ambaye ni mfano wa mafuta waliyokuwa wanapakwa wateule wa Mungu enzi za nyakati za Agano la Kale. Watu wote wamwaminio na kumtii Yesu wanaitwa WATEULE (ingekuwa ni nyakati za Agano la Kale basi nao wangemiminiwa mafuta kama ilivyokuwa desturi ya wana wa Israeli; lakini kwa sasa wanajazwa Roho Mtakatifu. Biblia inasema: "Nanyi, mafuta yale yanakaa ndani yenu... mafuta Yake yanavyowafundisha habari za mambo yote, tena ni kweli wala si uongo..." - (1 Yohana 2:27) Pia Yesu amesema: "...Yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote... na mambo yajayo atawapasha habari yake." - (Yohana 16:13) na pia Bwana Yesu amesema: "...Roho wa Kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, na Yeye atakuwa ndani yenu." - (Yohana 14:17). Hapo tunaona Biblia inasema: "...mafuta yale yanakaa ndani yenu..." - (1 Yohana 2:27); na pia tunaona imeandikwa: "...Roho wa Kweli... anakaa kwenu, na Yeye atakuwa ndani yenu." - (Yohana 14:17) Mafuta yale katika enzi za Agano la Kale yalitumika kama ishara tu ya kuteuliwa kwao, kwa maana imeandikwa: "...hii itakuwa ishara kwako ya kuwa BWANA amekutia mafuta..." - (1 Sam 10:1), bali kwa sasa Roho Mtakatifu Ndiye mafuta yakaayo ndani ya Wafuasi wote wa Yesu na kuwaongoza; na ndiyo ishara yetu ya kuteuliwa na Mungu, kwa maana imeandikwa: "...mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si Wake... Kwa maana wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu." - (Warumi 8:9, 14). Sasa je! Ni uthibitisho upi unaotubainishia kuwa Yesu ni Masihi / Kristo? Je! YEHOVA alithibitisha hilo? Biblia Takatifu inasema kwamba: "Alipokuwa akisema hayo, lilitokea wingu likawatia uvuli... Sauti ikatoka katika wingu, ikisema, Huyu ni Mwanangu, Mteule Wangu, msikieni Yeye." - (Luka 9:34,35) Sauti hiyo ilikuwa ni ya YEHOVA aliyenena mbele ya Petro, Yohana na Yakobo kwa wazi kabisa kwamba YESU NDIYE MTEULE WAKE. Kumbuka kwamba; enzi za Agano la Kale, kwa wana wa Izraeli ukisema neno "Mungu" unakuwa umemtaja "YEHOVA". Hivyo ndivyo wao walivyomtambua Mwenyezi Mungu kwa jina YEHOVA - (Mwanzo 6:2; Zaburi 83:18; Isaya 26:4; Yeremia 16:21; Habakuki 3:19) Hivyo sauti hiyo ilikuwa ya YEHOVA ikimthibitisha Yesu: "...ikisema, Huyu ni Mwanangu, Mteule Wangu, msikieni Yeye." - (Luka 9:35) Imani hii ya WAKRISTO wa sasa imejengwa kutoka kwa Yesu mwenyewe ndiyo maana tunaona wafuasi Wake wanaitwa WA-KRISTO kwa maana ya kwamba "Wateule wa Yesu." Wafuasi hao wa Yesu walikuwa WATEULE tangu kabla ya watu wa mataifa kuwaita kwa jina la Wakristo - (Matendo 11:26) Bwana Yesu Mwenyewe anasema kwamba: "Si ninyi mlionichagua Mimi, bali ni Mimi niliyewachagua ninyi..." - (Yohana 15:16) Wanafunzi wa Yesu waliteuliwa na Yesu, walijazwa Roho Mtakatifu na Yesu; hivyo walikuwa WATEULE hata kabla ya hao watu wa Antiokia kuwaita hivyo. Kwa hiyo neno MKRISTO lina maanisha "Mfuasi / Mteule wa Yesu." Ndiyo maana Biblia Takatifu inasema: "Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili Zake Yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru Yake ya ajabu." - (1 Petro 2:9) Kila aliye mfuasi wa Yesu ameteuliwa na Mungu. Anayeteua ni Mungu wala si mwanadamu; ndiyo maana hapo tumeona pameandikwa: "...ninyi ni mzao mteule,.. taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu..." Katika nyakati za Agano la Kale kule kupakwa mafuta kichwani kulikuwa ni ishara tu - (1 Sam 10:1) ya kuteuliwa na Mungu; bali, katika nyakati hizi za Agano Jipya, kumpokea Yesu, kutii kila aliloamuru, na kujazwa Roho Mtakatifu ndiko kunakufanya uwe mteule wa Mungu - (Yohana 1:12-13). UKRISTO ni zaidi ya kupakwa mafuta, bali UKRISTO ni UTEULE. Kama jinsi ilivyokuwa katika enzi za Agano la Kale kwamba Masihi (Makristo / Wapakwa Mafuta) walikuwa ni wale tu ambao waliteuliwa na Mungu bali jamii nyingine yote walibaki kuwa ni watu wa kawaida tu; vivyo hiyo hata sasa Wakristo / Wateule ni wale tu waliompokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yao na kujazwa Roho Mtakatifu, hao tu peke yao ndio wateule wa Mungu - (1 Petro 2:9). Hiyo ndiyo asili ya UKRISTO na maana halisi ya imani ya UKRISTO sawa sawa na jinsi neno la Mungu lifundishavyo. Lakini, tukizidi kutazama kwa kina imani ya Ukristo wa sasa tunaona imani hii imegawanyika katika sehemu kuu mbili, ambazo ni: (a) Wakristo wanaosali siku ya saba ya juma (yaani Jumamosi au Saturday ya leo). (b) Wakristo wanaosali siku ya kwanza ya juma (yaani Jumapili au Sunday ya leo). Matabaka hayo mawili pia wanapishana katika mafundisho na mapokeo fulani fulani. Japokuwa wote wanajiita Wakristo lakini cha ajabu hawaelewani katika mafundisho yao. Waswahili husema kwamba: "Ukweli usioujua hauwezi kukusaidia." Nami pia nakwambia kwamba: "Uongo usioujua ni vigumu kuuepuka." Je, kati ya makundi hayo mawili ya imani ya Ukristo wa sasa, ni kundi lipi linalofundisha mafundisho ya kweli sawa sawa na jinsi Yesu alivyoamuru? Yesu amesema: "...enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi... na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi..." - (Mathayo 28:18-20) Sasa, je! Ni kundi lipi kati ya hayo mawili linafundisha mafundisho ya uongo? Kabla ya kufufika mbali katika uchambuzi huo wa kuibainisha kweli, napenda nikuulize maswali haya: Je! Unapenda kujifunza? Je! Unapenda kuifahamu kweli? Kama jibu lako ni "NDIYO" sasa basi weka kando ushabiki wa dini au dhehebu. Pia zingatia kwamba: "Hauta elewa mpaka pale utakapo funguka akili; na hautafunguka akili mpaka pale utakapoikubali kweli." Katika utafiti wangu na kujifunza kwangu neno la Mungu nikiwa na watu mbalimbali, nimegundua watu wengi wanachanganywa na majina SIKU (DAYS) zilizopo kwenye juma (wiki). Ninapenda kwanza kuliweka sawa jambo hili ndipo tuendelee kujifunza kuhusu imani ya Ukristo wa sasa. Hebu kuwa makini zaidi ili uweze kuelewa vizuri. Tunapozungumza kuhusu “siku”, katika “juma moja” (wiki moja) kuna idadi ya “siku saba”. Siku hizo zimegawanyika katika matabaka makuu “mitatu”. Naomba uwe makini ili uelewe vizuri. Matabaka hayo ndiyo yafuatavyo: i/: KIBIBLIA. ii/: KIPAGANI, na iii/: KIISLAMU. Inawezekana hapa ukajiuliza: Hapo unamaanisha nini? Usihofu, fatilia kwa makini nawe utanielewa vizuri. Tukianza na siku ya JUMATATU: Kwa mujibu wa dini ya Kiislamu, kwao siku ya “Jumatatu” ya leo kwao ndiyo “siku ya tatu ya juma”. Tukilivunja vunja neno “JUMATATU” tunapata maneno mawili ambayo ni “JUMA”, na neno “TATU”. Neno “JUMA” maana yake ni “WIKI” au “muunganiko wa siku saba”, na TATU maana yake ni TATU (au THIRD - kwa Kiingereza) Kwa hiyo neno “Jumatatu” maana yake ni “siku ya tatu ya juma (wiki). Mpangilio huu umetokana na desturi ya Imani ya Kiislamu. Tukija KIBIBLIA, siku ya “Jumatatu” ya ki-sasa ni SIKU YA PILI YA JUMA. Ambayo siku hiyo kwa upande wa WAPAGANI waanaiita MONDAY. Hao WAPAGANI siku hiyo kwao ni kwaajili ya kuabudu MWEZI (moon - kwa Kiingereza). Katika nchi za Ulaya na Asia yapo mataifa yaliyokuwa yakiabudu MWEZI (MOON). Neno MONDAY ni kifupisho cha neno MOON - DAY (Siku ya Mwezi) kwa ajili ya kumuabudu mungu wao mwezi. Tukiingia siku ya JUMANNE: Kwa mujibu wa mafundisho ya Kiislamu, kwao JUMANNE ni SIKU YA NNE YA JUMA. Hiyo ni kutokana na desturi ya imani ya Kiislamu. Lakini tukija KIBIBLIA; siku ya JUMANNE ni siku ya TATU katika JUMA. Lakini kwa WAPAGANI wao siku ya JUMANNE wanaiita “TUESDAY”, ni siku maalumu waliyokuwa wakimuabudu mungu wao aliyejulikana kwa jina la “TIWI”. Siku hiyo wakaiita “Tiw's Day” ambayo baadae ikabadilishwa na kuitwa “TUE 's - DAY” (Siku ya Tue / Tiwi) sawa sawa na jinsi ijulikanavyo leo. Tukiingia kwenye siku ya JUMATANO: Kwa mujibu wa imani ya Kiislamu, wao siku ya JUMATANO ni siku ya TANO katika JUMA (week - kwa Kiingereza). Kwa mujibu wa Biblia Takatifu, siku ya JUMATANO ni siku ya NNE katika JUMA (week - kwa Kiingereza). Lakini kwa WAPAGANI, siku ya JUMATANO wanaiita WEDNESDAY. Siku hiyo kwa Wapagani ni maalumu kwa kumwabudu mungu wao ajulikanae kwa jina la “WEDNE” au “WODEN” ndiyo maana siku hiyo wakaipa jina la “WEDNE 's - DAY” au kwa English nyepesi ni “Wedne ' s Day” (Siku ya Wedne) sawa sawa na jinsi ijulikanavyo leo hata nyakati za leo. Tukiingia kwenye siku ya ALHAMISI: Kwa mujibu wa mafundisho ya Kiislamu, siku ya ALHAMISI ni siku ya SITA katika JUMA (week - kwa Kiingereza). Lakini kwa mujibu wa Biblia Takatifu, siku ya ALHAMISI ni siku ya TANO katika JUMA. Wakati huo kwa upande wa WAPAGANI, wao siku ya ALHAMISI wanaiita “THURSDAY”. Katika siku hiyo hiyo wapo WAPAGANI wanaoabudu “SAYARI YA JUPITER”, na WAPAGANI wengine ni siku maalumu kwao ya kumwabudu mungu wao aitwaye “THOR” au "THUR". Ndiyo maana siku hiyo wakaiita “THUR 's - DAY” au kwa English nyepesi ni “Thur 's Day” (Siku ya Thur). Tukiingia kwenye siku ya IJUMAA: Kwa mujibu wa imani ya Kiislamu, siku ya IJUMAA kwao ni siku ya SABA katika JUMA (week - kwa Kiingereza). Neno IJUMAA ni neno lenye asili ya lugha ya Kiarabu likiwa na maana ya KUSANYIKO (kwa lugha ya Kiswahili). Ndiyo maana katika siku hiyo waumini ya imani ya Kiislamu hukusanyika kwenda kulitaja jina la mola wao (Allah) na kisha baada ya swala (ibada) hutawanyika kwenda kutafuta riziki zao kama jinsi kitabu cha Qur'an kinavyo waamuru. Kwao si siku ya PUMZIKO bali ni siku ya KUSANYIKO. Kwa upande wa Biblia Takatifu, siku ya IJUMAA ni siku ya SITA katika JUMA (week - kwa Kiingereza) Lakini kwa WAPAGANI wao wanaiita FRIDAY. Kwao ni siku maalumu kwa kumwabudu mungu wao aitwaye “FRIGG” au “FREIA”. Ndiyo maana siku hiyo wakaiita FRI -DAY (Siku ya Fri). Tukiingia kwenye siku ya JUMAMOSI: Kwa mujibu wa mafundisho ya Kiislamu, siku ya JUMAMOSI ni siku ya KANZA katika JUMA (week - kwa Kiingereza). Neno “MOSI” maana yake ni “MOJA au KWANZA” (FIRST - kwa Kiingereza). Tumejifunza JUMA moja lina idadi ya SIKU SABA ndani yake; ndiyo maana kwa Waislamu siku ya IJUMAA tumeona ni SIKU ya SABA kwao, alafu JUMAMOSI ni SIKU ya KWANZA kwao. Hapa tunabaini kuwa hizo siku tunazozitumia Waswahili zimetokana na desturi ya mafundisho ya imani ya Kiislamu. Bila shaka hadi hapa tupo pamoja. Tukija upande wa Biblia Takatifu; siku ya JUMAMOSI ni siku ya SABA katika JUMA. Hapa ndipo tunawapata Wakristo wenye imani ya USABATO, wao siku hiyo ni SIKU YA SABATO (PUMZIKO) kwao. Wao hupumzika siku nzima bila kufanya kazi yo yote kwa kuwa ni marufuku kwao kufanya kazi katika siku hiyo. Wasabato hiyo ni siku maalumu kwa ibada tu. Bali Wakristo wasio na imani ya Kisabato wao huendelea na kazi zao kama kawaida. Tukija upande wa WAPAGANI, wao siku ya JUMAMOSI wameipa jina la SATURDAY. Kwao WAPAGANI ni siku maalumu ya kuabudu sayari ya SATURN. Wapo wapagani waliokuwa wanaabudu sayari ya “SATURN” ndiyo maana siku hiyo wakaipa jina la “SATUR - DAY” (yaani Siku ya Saturn). Tukimalizia siku ya JUMAPILI: Kwa mujibu wa mafundisho ya Kiislamu siku ya JUMAPILI kwao ni siku ya PILI katika JUMA. Lakini kwa mujibu wa Biblia Takatifu; siku ya JUMAPILI ni SIKU YA KWANZA YA JUMA. Je! Tunalitambuaje hili? Biblia Takatifu inasema: "Hata Sabato ilipokwisha, ikipambazuka siku ya kwanza ya juma... Yesu aliyesulibiwa... Amefufuka katika wafu..." - (Mathayo 28:1,5,7) Ndiyo maana wapo Wakristo wanaofanya ibada katika siku hiyo ya kwanza ya juma. Tukiingia kwenye upande wa WAPAGANI siku ya JUMAPILI wao wameipa jina la “SUNDAY” yaani ni “SIKU ya JUA” (SUN). Wapo wapagani ambao wanaabudu JUA. Ndiyo maana siku hiyo wakaiita “SUN - DAY”. Mpendwa msomaji; je! Umewahi kujiuliza kwa nini ndani ya Biblia Takatifu hakuna neno Jumatatu (Monday), Jumanne (Tuesday), Jumatano (Wednesday), Alhamisi (Thursday), Ijumaa (Friday), Jumamosi (Saturday), wala Jumapili (Sunday)? Bali utaona kwenye Biblia Takatifu pameandikwa Siku ya Kwanza, Siku ya Pili, Siku ya Tatu… Siku ya Saba? - (Mwa 1:5,8,13,19,23,31; Mathayo 28:1). Bila shaka ufafanuzi nimeshautoa hapo juu. Hadi kufikia hapo itakuwa imeeleweka vizuri kuhusu SIKU NA MAJINA YAKE. Sasa basi napenda moja kwa moja tujifunze kwa undani kuhusu mgawanyiko huu uliopo katika watu wa imani ya UKRISTO wa leo kwa kuanzia na WAKRISTO WENYE IMANI YA SABATO, kisha tutajifunza kuhusu WAKRISTO WANAOSALI SIKU YA KWANZA YA JUMA.