Saturday, 12 November 2016
Friday, 4 November 2016
KUFUNGA NA KUOMBA KWANGU MKRISTO
AINA ZA KUFUNGA.
Zipo aina tano ( 5 ) za kufunga.
1. TOTAL FAST (FUNGA KAVU).
Absolute fasting (Funga iliyo sahihi)
Hii ni funga ya kutokula chakula kabisa wala kunya maji kwa siku zisizo zidi tatu (3)
kama (Esta 4:16).
b. Supernatural Fasting (Funga ya Kiungu).
Funga ya kutokula chakula kabisa wala kunywa maji kwa siku zaidi ya tatu (3) kama Musa
(Kumb.9:9 & 9:18) kwa siku 40.
2. PARTIAL FASTING (FUNGA NUSU)
a. Yohana Mbatizaji aliamua kufunga maisha yake yote akila asali na Nzige tu. Dan. 10:2-3
Kuacha kula aina maalumu ya vyakula ambavyo ungevipenda.
b. Funga ya milo miwili au mmoja kwa siku.
c. Funga ya kawaida (Normal fasting).Kunya maji tu.
3. FUNGA YA KULAZIMISHWA (IMPOSED FAST).
Matendo 28:1
Safari ya Paulo akielekea Rumi.Kwasababu ya misukosuko ya mawimbi majini watu wanashindwa kula.
Pia kama mtu anaumwa unakosa hamu ya chakula.Mala nyingine tunapata misukosuko kama sehemu ya Maisha kiroho pia.
4. FUNGA YA WAZI/KANISA, HADHARA AU TAIFA.
(PUBLIC AND NATIONAL/CHURCH FASTS).
Hii inakuwa funga ambayo inatangazwa na inakuwa wazi kwa kila mtu.Sio za siri.
Yona 3:6. 5.
Funga ya mtu binafsi Hii hufanywa na mtu mmoja kwa siri na mungu wake hapana anayejua mtu huyo kama amefunga.
SIFA 7 ZA KUFUNGA NA KUOMBA KUNAKOONGEA
1. Huongozwa na roho wa Mungu
Marko 1:12-14,
Yesu aliongozwa na roho kufunga nyikani ndio
maana hakutenda dhambi katika kufunga na kuomba kwake.
2. Lazima iwe katika kweli ya Mungu. Kama funga na kuomba huko hakuko katika
roho hakuwezi kuwa katika kweli kwa kuwa roho wa mungu hatenganishwi na kweli ya Mungu.
2samwel12:16-17
Daudi alijaribu kufunga na kuomba ili motto aliyezaliwa katika zinaa asife hakufanikiwa
kwa kuwa Mungu tayari alisema atakufa hakika.
Hata alipokuwa ameshakufa daudi aliendelea kufunga hii inadhihirisha kuwa hakuwa rohoni kwa sababu alijua anachoomba
siyo mapenzi ya Mungu.
Angekuwa rohoni roho angemjulisha aache kuomba kwa kuwa Mungu amekataa.
3. Lazima uwe mtu wa Mungu uliyeitwa kwa jina lake 1cronicles
(2Nya 7:14a
Hapa tunaona Mungu anadhirisha kuwa si kila mtu wa Mungu ameitwa kwa jina lake. Aliyeitwa kwa jina lake ni Yule aliyezaliwa mara ya pili katika roho mtakatifu
(Yohana 1:11-13) 4.
Lazima funga ifanywe katika unyenyekevu wa hali ya juu wa rohoni.
Mtu anayefunga kwa kiburi cha uzima hawezi kupata matokeo yaliyokusudiwa. Mfano
unafunga ili ujilipizie hasira yako kwa mtu anayekudharau au kutesa, unataka kushindana na wengine,
unataka kuonesha kwamba wewe ni mwamba kanisani kwenu nk.
Isaya 58:3-4)
“Husema mbona tumefunga lakini huoni, mbona tumejitaabisha nafsi zetu lakini huangalii?
Fahamuni siku ya kufunga kwenu mnatafuta anasa zenu wenyewe, na kuwalemea wote watendao kazi kwenu, Tazama
ninyi mwafunga mpate kushindana, kugombana na kupiga ngumi ya uovu” 5.
Lazima ifanywe katika furaha ya roho mtakatifu na siyo kwa kujilazimisha na kunung’unika Ukifunga kama andiko la
Isaya 58:3
inasema (mbona tumefunga lakini huoni,
mbona tumejitaabisha nafsi zetu lakini huangalii?
Hutapata matokeo yaliyokusudiwa. Badala yake fanya funga na maombi yaliyojaa furaha ya roho mtakatifu
Mathayo 6:16-18
“tena mfungapo msiwe kama wanafiki, wenye uso wa kukunjamana, maana hujiumbua nyuso zao ili waonekane na watu kuwa wanafunga,
amini nawaambia wamekwishakupata thawabu yao.
Bali wewe ufungapio jipake mafuta kichwani,
unawe uso ili usionekane na watu kuwa unafunga, ila na baba yako aliye sirini na baba yako aonaye sirini atakujazi” linganisha andiko hilo na
Isaya 58:5 6.
Lazima kufunga kuambatane na kuomba na kuutafuta uso wa bwana 2Nya 7:14, 7.
Lazima kufunga na kuomba kufuate kanuni ya upendo na si ubinafsi. Yaani kumpenda
Mungu na jirani kama nafsi yako mwenyewe.
Matendo ya upendo kwa mungu na watu ni kama
1. hicho ambacho ungekula mpe Yesu ale. Unadhani Yesu anapatikana kanisani?
Hapana, msikie mwenyewe anapatikana wapi katika
Math 25:34-40
“Kisha mfalme akawaambia wale walioko mkono wake wa kuume, njooni mliobarikiwa
na baba yangu, urithini ufalme muliowekewa tayari tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu kwa maana nalikuwa
na njaa mkanipa chakula, nalikuwa na kiu mkaninywesha, nalikuwa mgeni mkanikaribisha, nalikuwa uchi mkanivika,
nalikuwa mgonjwa mkaja kunitazama, nalikuwa kifungoni mkanijia………………………………………amini nawaambia yoyote mliyowatendea mmojawapo ya hao ndugu zangu walio wadogo mlinitendea mimi”
NB: Linganisha andiko hilo na
Isaya 58:6a, 7
Je, Swaumu niliyoichagua mimi siyo ya namna hii?……………. je siyo kuwagawia wenye njaa chakula chako na kuwaleta maskini waliotupwa nje nyumbani mwako?
Umwonapo mtu aliye uchi umvike nguo, wala usijifiche na mtu mwenye damu moja nawe”
2. Ombea watu wengine kama familia, jamii yako, familia na taifa kwa nguvu ileile unayotumia kuombea mahitaji yako binafsi.
Isaya 58:6,
2Samweli 22: 25-26.
“ kwa mtu mwenye fadhili utakuwa mwenye fadhili, kwa mkamilifu utajionyesha
kuwa mkamilifu, kwake ajitakasaye utajionyesha kuwa mtakatifu na kwa mpotovu utajionyesha kuwa mkaidi”
Nehemia 1:1-11
jinsi Nehemia alivyolia na kutubu kwa habari ya mabaya yaliyoipata Israel na Yeusalem
hakujali kuwa alikuwa mahali salama.
Danieli 9
jinsi alivyolia kwa Mungu kwa habari ya wayahudi hata kama yeye mwenyewe alikuwa ikulu akiheshimika sana.
Au Ester ambaye alikuwa mke wa mfalme Ahusueoro angeweza kubaki alivyo lakini alifunga na kupomba kwa ajili ya
ndugu zake
SABABU /FAIDA 12 ZA KUFUNGA NA KUOMBA KATIKA KANISA
(MTU AU USHIRIKA)
1. Tunafunga kuonyesha utii kwa neno la Mungu
(Yoeli 2:12)
Biblia kuanzia agano la kale hadi agano jipya inaonyesha umuhimu wa kufunga.
Watumishi wote wa Mungu walikuwa wanafunga katika siku za maisha yao hivyo
unavyofunga unaonyesha utii katika kulifuata neno la Mungu na kuliamini.
Yesu Pia alisema kuwa siku zinakuja ambapo tutalazimika kufunga.
(Mathayo 9:15)
2. Tunafunga ili kujinyenyekeza mbele za Mungu na kupata nguvu na neema yake.
Tunahitaji neema ya Mungu siku zote ili tuweze kuishi, na ili kuipata inatubidi kujinyenyekeza chini ya mkono wake ulio hodari,
Ebrania 4:16, na Yakobo 4:10.
Ezra aliwaamuru watu wafunge ili wapate kujinyenyekeza
mbele za Mungu na kupata neema yake kwa ajili ya taifa lao,
Ezra 8:21. 3.
Tunafunga ili kuomba rehema Yesu alichukua dhambi zetu zote msalabani, inawezekana kuna jambo unaona unashindwa
kuacha na umejaribu sana. Hapo unatakiwa kufunga na kuomba rehema ili Mungu akuwezeshe kushinda. Pia unafunga kuomba rehema kwa ajili ya wengine mfano familia, jamaa na taifa pia.
Daniel alifunga na kuomba rehema kwa ajili ya dhambi za taifa la Israeli na kubeba uovu wao mbele za Mungu. Danieli 9:3-5.
Taifa la Ninawi walifunga na kuomba rehema kwa Mungu kutokana na uovu wao.
Yona 3:5-10 4.
Tunafunga ili katika udhaifu wetu Nguvu ya Mungu ionekane Unapofunga unakuwa umeikana nafsi na kumchagua Mungu,
uankuwa umedhamiria moyoni kutaka kuona nguvu ya Mungu ikionekana na sio nguvu yako.
Zaburi 109:24-28,
2Korintho 12:9-10 5.
Tunafunga kupata msaada wa Mungu katika kukamilisha kusudi lake Viongozi wa
kanisa la Antiokia walifunga na kuomba kabla ya kuwatuma Paulo na Barnabas.
Walifanya hivi ili waweze fanya uchaguzi sahihi chini ya uongozi wa Mungu.
Na Paulo na Barnabas
walikuwa wakifanya hivyo katika miji waliyotembelea kila walipokuwa wanataka
kuchagua viongozi.
Kutokana na jambo hili makanisa yale yalizidi kusonga mbele maana walimshirikisha Mungu kwa kufunga katika maamuzi yao yote.
Matendo 13:3-4, 14:23 6.
Tunafunga wakati wa taabu Mordekai na Esta walitangaza kufunga kwa wayahudi wote pale
ilipofahamika kuwa kuna mpango wa kuwateketeza wayahudi wote, na kupitia kufunga na kuomba huku wayahudi walisalimika.
Ester 4:15-16.
Wakati wa taabu ni wakati wa kufunga na kumlilia Mungu na hakika Mungu ataonekana.
Mfalme Yehoshafati pia alitangaza kufunga pale walipokuwa wamevamiwa na maadui wengi na wao hawakuwa na uwezo
wa kupigana nao
2Nyakati 20.
Tumeona kwa uchache jinsi kufunga kulivyo muhimu katika maisha yetu ya kila siku. 7.
Kufunga hunoa Imani (ili iwe kali) na huongeza ujasiri.
Esta 4:16.
Huyu mama asingefunga alikuwa hana ujasiri
wala imani ya kuingia kwa mfalme kinyume cha sheria – kwasababu adhabu yake ilikuwa ni kifo.
Ndio maana aliomba wayahudi wote walio kuwa shushani wambebe kwa maombi.
8. Kufunga huleta unyenyekevu mbele za Mungu.
Luka 14:11 & 18:14 Ezra 8:21.
Mungu huwapa wanyenye kevu neema,na kuwainua.
(1Petro5:5-6).
Ukitaka kuwa mnyenyekevu mbele za Mungu basi jifunze kuwa mfungaji. 9. Kufunga huongeza/huleta nguvu ya Maombi na kuondoa ukame wa kiroho.
Zaburi 35:13
Kufunga ni kama 4WD ya maombi.
ISAYA 40:31
na Mithali 20:13. 10.
Kufunga hufanya ulimwengu wa roho uwe wazi.
Daniel 10:14.
Baada ya Danieli kufunga siku 21 alianza kuonyeshwa na Mungu mambo ya siku za mwisho
za dunia ambako hata 11. Kukuza kanisa na huduma ya Mungu a. Hili tendo lililofanywa sana na mitume na wafuasi wao.
Mdo 14:22.
Kukua kwa Kanisa la kwanza kulitegemea Maombi ya kufunga.
b. Ushuhuda wa Paulo kuhusu maisha yake.Akafanikiwa sana kwa sababu ya maombi ya kufunga.
2Koritho 6:4-6. 12.
Kutiisha miili yetu ipate kumtii Kristo. Miili yetu siku zote hupingana na Roho Mtakatifu.
Galatia 5:16-17.
nia ya Mwilini uadui dhidi ya Mungu
Rumi 8:7-8
hivyo inabidi tuiitiishe kwa kufunga
1Kor.9:27.
Mungu akubariki mpendwa wangu!
Ni Mimi ndugu yako
Ev. Elimeleck S Ndashikiwe
+255767445846 &
+255715445846
Thursday, 3 November 2016
MAISHA YA WOKOVU, MTUME PAULO
HISTORIA YA MTUME PAULO
Sunday, 23 October 2016
Tuesday, 18 October 2016
KUOKOKA
Watu wengi wamekua wakijiuliza kuhusu kuokoka ni nini,
jamii nyingine wamekua wakipinga jambo la kuokoka hapa duniani kana kwamba wataweza kutenda jambo wakiwa marehemu ambalo litawafanya waokoke.
Lakini kuokoka wanadamu tunaokoka hapa hapa duniani maana hatuwezi kufanya chochote tukiwa wafu hivyo kwa maamuzi ya leo unaweza kuokoka, kwa matendo yako ya sasa unaweza kuokoka na sio baadae baada ya kufa.
*Kuokoka ni kumwamini YESU KRISTO.
Yohana 1:12 -13
‘’Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake;
waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa MUNGU.
‘’ Kumwamini YESU ni kumkubali YESU na pia kumtegemea kwa kila kitu, na yeye alisema kwamba sisi bila yeye hatuwezi kufanya lolote hata lile lililo dogo kabisa.
Matendo 16:30-31
Biblia inasema
‘’ kisha akawaleta nje akasema, Bwana zangu, yanipasa nifanye nini nipate kuokoka?
Wakamwambia,
Mwamini BWANA YESU, nawe utaokoka pamoja na nyumba yako. ‘’
*Tukimwamini BWANA YESU tunakuwa na ROHO MTAKATIFU ambaye hutufanya kuchukia dhambi kwani bila ROHO MTAKATIFU hakuna awezaye kuacha dhambi.
BIBLIA katika
Yohana 3:3
‘’YESU akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa MUNGU. ‘’
*Kuzaliwa mara ya pili ni
1: Kumwamini YESU.
2: Kubatizwa .
3: Kuwa na ROHO MTAKATIFU.
Yohana 3:17-18’’
Maana MUNGU hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye. Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa MUNGU.
‘’ Tunaokoka hapa hapa duniani kwa sababu ‘’
Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya KRISTO amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama!
Yamekuwa mapya. ‘’
- 2 Korintho 5:17.
*Ndugu ukiamua kuokoka usirudi nyuma maana unaweza ukapoteza wokovu wako.
Luka 9:61-62'' Mtu mwingine pia akamwambia, BWANA, nitakufuata; lakini, nipe ruhusa kwanza nikawaage watu wa nyumbani mwangu.
YESU akamwambia,
Mtu aliyetia mkono wake kulima, kisha akaangalia nyuma, hafai kwa ufalme wa MUNGU.''
*Watu wengine huogopa kuacha dhambi eti kwa sababu shetani atawatesa kwa sababu wamewahi kuingia maagano naye ya kishetani huo ni uongo.
Maana YESU akikuokoa anakuhamisha kutoka katika kila agano lako na shetani na kuanzia muda hu unakua mtoto wa MUNGU ambaye huwezi kurogwa tena maana mamlaka ya BABA yako wa mbinguni uliyeamua kumpa maisha yako ni kuu sana na hakuna anayeweza kukudhuru tena
na BWANA YESU atakuwa ndiye anayekuchunga
Zaburi 23:1’
’ BWANA ndiye mchungaji wangu, Sitapungukiwa na kitu. ‘’ .
*Ndugu duniani hapa tunapita tu maana hata kama ukiishi miaka 98 hapa duniani lakini ni bure kabisa kama utapotelea motoni baada ya kufa kwa hiyo bora kumpa YESU maisha yako na utakuwa huru kabisa pia utapata uzima sasa na baadae uzima tele.
YESU anasema katika
Yohana 10:10b’’
mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele. ‘’.
ndugu dunia hii tuliikuta na tutaiacha hivyo ni heri kwa sasa kuishi maisha ya kumcha MUNGU.
Neno la MUNGU linakushauri kwamba ‘’
Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia.
Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake.
Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia.
Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya MUNGU adumu hata milele. ‘
’-1 Yohana 2:15-17
Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho,
amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU
ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
MUNGU akubariki sana.
Ni Mimi ndugu yako
Ev. Elimeleck Ndashikiwe
+255767445846
+255715445846
Monday, 3 October 2016
SOMO;
MACHUKIZO NDANI YA NYUMBA YA MUNGU
(YEREMIA 32:33-34)
“Tena wamenigeuzia visogo vyao, wala si nyuso zao;
ingawa naliwafundisha, nikiondoka mapema na kuwafundisha, lakini hawakusikiliza ili wapate mafundisho.
Bali waliweka machukizo yao ndani ya nyumba iliyoitwa kwa jina langu, ili kuinajisi”.
Machukizo ya aina yoyote hayaruhusiwi ndani ya nyumba ya Mungu na ndani ya nyumba zetu.
( KUMBUKUMBU LA TORATI 7:26 )
“na machukizo usitie ndani ya nyumba yako, usije wewe kuwa kitu cha haramu mfano wake; ukichukie kabisa, na kukikataa kabisa; kwa kuwa ni kitu kilichoharamishwa”.
Machukizo yanatajwa kuwa ni kitu kilichoharimishwa.
Neno machukizo linatokana na neno la lugha ya kiebrania linaloitwa” toebah”.
Neno “TOEBAH” lina maana ya kitu au mtu ambaye ni wa tofauti katika hali. Mtu ambaye ni hatari ukilinganisha na watu wengine.
Yatakuwa ni mambo au tabia ambazo ziko kinyume na asili yake. Machukizo sasa ni vitu vya kipagani ambavyo vimeingia ndani ya nyumba ya Mungu. Yapo mambo ambayo ni machukizo ndani ya nyumba ya Mungu. Mambo ambayo ni haramu kuingizwa ndani ya nyumba ya Mungu.
( i ). Mwanamke kuvaa mavazi ya wanume na mwanamume kuvaa mavazi ya wanawake.
( KUMBUKUMBU LA TORATI 22:5 ). ‘ Mwanamke asivae mavazi yampasayo mwanamume, wala mwanamume asivae mavazi ya mwanamke; kwa maana kila afanyaye mambo hayo ni machukizo kwa BWANA,
Mungu wako”.
Mungu anasema maumbile yetu ndiyo yatufundisheni vazi lipi linafaa kuvaliwa na wanaume na ni nlipi linafaa kuvaliwa na wanawake ( 1 WAKORINTHO 11:14 ). Mitindo ya ushonaji nguo iadizainiwa kutokana
na maumbile yetu. Ndiyo maana wanawake wana mavazi yao na wanaume wana mavazi yao na Mungu ameliweke hilo mwenyewe. Kwa hiyo vazi kama suruali siyo la mwanamke, limedizainiwa kwa ajili ya mwanamume na si vinginevyo.
Katika biblia ni wanaume pekee wanaotajwa wakiwa wamevaa suruali, hatuoni sehemu yoyote ikimtaja mwanamke akiwa amevaa suruali. Ingia katika blog yangu ujifunze somo la “MAVAZI YA KIKAHABA” utajifunza mengi kuhusiana na mavazi.
Suruali kwa wanawake ni vazi la kikahaba kabisa
( MITHALI 7:10 ) ( ii ). Sadaka ya kahaba na Mbwa ni machukizo mbele za Mungu ( KUMBUKUMBU LA TORATI 23:18 ) “Usilete ujira wa kahaba, wala mshahara wa mbwa, katika nyumba ya BWANA, Mungu wako, kwa ajili ya nadhiri yo yote; kwani
haya ni machukizo kwaBWANA, Mungu wako yote mawili”. Mbwa ni mtu anayerawiti au mtu anayerawitiwa. Mshahara wa kahaba na watu wote wanaoshiriki katika uchafu wa kurawiti na kurawitiwa ni machukizo kwa BWANA, Mungu wetu. Hatutakiwi kupokea sadaka zao kwa ajili ya BWANA, ni machukizo kwake. ( iii ). Miungu na chochote kinachohusiana na miungu ni machukizo mbele za Mungu. ( EZEKIELI 8:1-18 ) Namna yoyote ya sanamu tunapoihusisha katika ibada tayari inakuwa ni ibada ya miungu. Mapambo ya aina yoyote ni chukizo mbele za Mungu wetu kwa sababu kuna uhusiano kati ya mapambo na miungu. Ni muhimu kufahamu kuwa mapambo hayakuvaliwa na Waisraeli. ( WAAMUZI 8:24 ) “ Kisha Gideoni akawaambia, Mimi nina haja yangu kwenu, ni yakila mtu kunipa hizo pete za masikio ya mateka yake. ( Kwa maana walikuwa na pete za masikio za dhahabu, kwa sababu walikuwa ni Waishmaeli )”. Waishmaeli walikuwa ni wapagani ( mataifa ) vilele waliitwa Wamidiani. ( MWANZO 35:1-4 ). “……………Yakobo akawaambia watu wa nyumbani mwake na wote waliokuwa pamoja naye, Ondoeni miungu migeni iliyoko kwenu,………..Nao wakampa Yakobo, miungu migeni yote iliyokuwa masikioni mwao, na pete zilizokuwa masikioni mwao…………….”. Mwanamke Yezebeli alikuwa mataifa tena mwabudu miungu. Mwanamke huyo alikuwa staid sana kwa kujipamba na aliingia katika Taifa la Israeli baada ya kuolewa na mfalmeAhabu. Kwa hiyo mapambo yalikuwa yakivaliwa na Waisraeli kwa kuiga tabia za mataifa
( 2 WAFALME 9:30-37;
UFUNUO 2:20 ) Makanisa mengi leo yanahudu mafundisho ya Yezebeli ya kuruhusu mapambo kwa watu wa Mungu. Mungu aliwatumia
mitume kwa ishara na miujiza mikubwa kutokana na injili yao kuwa kinyume na machukizo. Kanisa la kwanza walifundishwa kuwa mbali na mapambo ya kila namna ( 1 TIMOTHEO 2:9-10; 1PETRO 3:3-5 ). Kinyume na asili ya Mungu ndiyo maana ya machukizo ( un contrallel to his nature ). Machukizo kwa asili yalikuwa ni ya mataifa na hayakuwa ya Waisraeli.
( YEREMIA 4:1 ) “Kama ukitaka kurudi, Ee Israeli, asema BWANA, utanirudia mimi; na kama ukitaka kuyaondoa machukizo yako, yasiwe mbele ya macho yangu, ndipo hutaondolewa”.
Kuna uwezekano mkubwa hata wakuu wa makuhani ( maaskofu ) kuruhusu machukizo kuingia nyumbani mwa Mungu. Machukizo yakiingia madhara yake ni makubwa kwa watu wa Mungu. Tunaona katika andiko hilo chini kuwa hata uwezo au mkono wa Mungu wa kuponya unaondoka
( 2 NYAKATI 36:14-16 ).
“Na zaidi ya hayo wakuu wote wa makuhani, na watu, wakakosa mno sawasawa na machukizo yote ya mataifa; wakainajisi nyumba ya BWANA aliyoitakasa katika Yerusalemu. Naye BWANA, Mungu wa baba zao akatuma kwao kwa mikono ya wajumbe wake, akiondoka mapema, na kutuma; kwa sababu aliwahurumia watu wake, na makao yake;
Lakini waliwadhihaki wajumbe wa Mungu, na kuyadharau maneno yake, na kuwacheka manabii wake, hata ilipozidi ghadhabu ya BWANA juu ya watu wake, hata kusiwe na kuponya”. Miujiza ya Mungu ya uponyaji kama wakati wa Yesu na wakati wa mitume haiwezi kuonekana dhahiri kwa watu wanaoruhusu machukizo kwa watu wa Mungu na ndani maskan i(nyumbani) yake Mungu, Utakuta watu wanashughulika na mapepo tu kila siku lakini miujiza ya vipofu kuona, viziwi kusikia, viwete kutembea, mabubu kuongea, wenye kigugumizi kuongea sawasawa, wenye makengeza kuponywa na kila namna ya miujiza mingine kama nyakati za mitume havionekani. Mamlaka waliyokuwa nayo mitue ya kumwambia kuwete ‘ Kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, simama uende ( MATENDO 3;6 )’. Mamlaka haiko leo kwa watumishi wengi sababu ni kwamba wameruhusu machukizo nab ado tu wanaendelea kuyatetea kwa bidii nyingi.
( YOHANA 2:13-17 ) Yesu Kristo alipokuta watu wamegeuza hekalu soko alichukizwa mno na kitendo kile ndipo akaamua kupundua meza zao, na kuwaondoa wote hekaluni kwa kutumia kikoto.
Aliuliza, Yesu hakuyavumilia machukizo nyumbani mwa baba yake. Watumishi wa Mungu leo wanatakiwa kufuata msingi aliouweka
BWANA YESU na si kuyaacha machukizo eti kwa visingizio vya kulinda kundilisipungue, hatuwasaidii washirika wetu. Tunapaswa kumwondoa mwovu miongoni mwetu ili wengine wajifunze kukaa katika viwango vyote vya neno la Mungu.
( iv ). Wanawake wanapaswa kufunika kichwa wakiwa katika ibada. Wanapaswa kufunika wakiwa kanisani, wanapofanya huduma yoyote ya kiroho mfano, kuomba, kuhutubu au kuhubiri.
( 1 WAKORITHO 11:4-5,7,10,13
‘ Sheria inayomkataza mwanamume kumwomba Mungu akiwa amevaa kofia pia inayomkataza kuvaa kofia kanisani hiyo hiyo ndiyo inayomtaka mwanamke afunike kichwa
kwa ajili ya Malaika. Wanaosema ilikuwa desturi za Wakorintho hawayaelewi maandiko vizuri. Biblia inasema ‘ Imempasa mwamke awe na dalili ya kumilikiwa kichwani kwa ajili ya Malaika”. Angalia vizuri neno ‘ imempasa=lazima”. Hakuna Biblia ya Wakorintho pekee yao, tukichambua Biblia hivyo sisi Watanzania hatutabaki na kitabu chichote.Yote yaliyoandikwa, yaliandikwa kwa ajili yetu wote ( WARUMI 2;16 ), Mungu atayahukumu mataifa yote kwa injili hiyohiyo Tukitaka kuziona nguvu za Mungu waziwazi lazima tuwe mbali na machukizo ya aina yoyote. Mafuta ya Mungu yanakuwa juu ya mtu anayechukia machukizo
( WAEBRANIA 1:9 ). Mtu ambaye anatetea machukizo yaliyomo ndani ya maskani ya Mungu lakini akifanya miujiza au maajabu lazima tujiulize ni nguvu ipi inatenda kazi hapo?. Mungu mwenyewe anasema kuwa mahali penye machukizo, ukono wake wa kuponya hauwezi kuwepo ( 2 NYAKATI 36:14-16 ), Pia hawezi kupakwa mafutaNA Mungu ( WAEBRANIA 1:9 ). Nyakati hizi tulizonazo watu wengi hawapendi kuambiwa ukweli, wanapenda kudanganywa. Paulo mtume alitabiri juu ya nyakati hizi jinsi watu watakavyotafuta waliu wa kuwafundisha uongo na kuikataa kweli ya neno la Mungu ( 2 timotheo 4:3-4). Hata wakati wa nabii Isaya walikuwepo watu waliotafuta walimu wengine wa mbali na Isaya aliyehubiri kweli yote. Walisema kuwa wanataka mafundisho laini yadanganyayo ( ISAYA 30;9-10 ).Kama tunataka kuishi na Mungu milele hatuna budi kutubu dhambi zetu kwa kumaanisha kuziacha na kuwa tayari kuyafuata maagizo yote ya Neno la Mungu ( ZABIRI 119:6 ). Tunasafisha njia zetu kwa kutii neno la Mungu na siyo walimu wetu wanaotufariji tuendelee kufanya machukizo mbele za Mungu ( ZABURI 119;9 ). Walimu wanaowatia moyo watu ili waendelee kuvaa mapambo na suruali kwa wanawake wote ni wafariji wa kutaabisha ( AYUBU 16:2 ). Ni sifa ipi ya kutuwezesha kuingia mbinguni? Ni utakatifu (WAEBRANIA 12:14). Ndani yake hakitaingia kamwe chochote kilicho kinyonge (UFUNUO WA YOHANA 21:27). Kinyonge ni kipi? Ni yule anayetenda dhambi. Huyu ni mtu asiyefaa, ni mnyonge! Je, wewe ni mtakatifu? Jibu ni la! Maisha yako yamejaa dhambi, pamoja na kusema una dini; hivyo wewe pia ni mnyonge, hufai kuingia mbinguni. Ukitubu leo dhambi zako zote kwa kumaanisha kuziacha, na kuifuata njia ya Yesu Kristo, ndipo utakapopata rehema ya kuingia mbinguni (MITHALI 28:13; YOHANA 14:6). Je, uko tayari kutubu sasa ili upate rehema hii? Najua uko tayari. Basi fuatisha sala hii ya toba kwa dhati kutoka moyoni; “Mungu Baba asante kwa ujumbe huu. Hakika mimi ni mnyonge, mwenye dhambi. Sistahili kuingia mbinguni. Natubu dhambi zangu zote kwa kumaanisha kuziacha. Kuanzia leo nataka niifuate njia ya Yesu Kristo. Bwana Yesu niwezeshe. Asante kwa kunisikia katika Jina la Yesu. Amen”. Mpendwa msomaji umekubaliwa kuingia mbinguni. Ili uzidi kudumu katika utakatifu mpaka siku ya kuiaga dunia hii, hakikisha unahudhuria mafundisho katika Kanisa linalohubiri wokovu. MUNGU AKUBARIKI !!!
Thursday, 15 September 2016
Hatareeeeeee kwa Vijana
Uzinzi Mungu ametuonya tusi zini. Katika
Kutoka 20:14 imeandikwa,
"usizini".
Kumwacha mke wako au mume wako na kuoa mtu mwingine yaweza kuwa halali kwetu lakini kwa Mungu ni dhambi.
Luka 16:18 inasema
"Kila amwachaye mkewe na kumwoa mke mwingine azini;
naye amwoaye yeye aliyeachwa na mumewe azini." Kutamani mtu asiye mume au mke wako nikuzini katika
Mathayo 5:27 -28 "Mmesikia kwamba imenenwa, usizini; lakini mimi nawaambia, kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini moyoni mwake."
Yesu alimchukulia vipi mwanamke aliyeshikwa akizini?
Yohana 8:10-11 Inasema,
" Yesu akajiinua asimwone mtu ila yule mwanamke, akamwambia mwanamke, wako wapi wale washitaki wako?
je! hakuna aliyekuhukumu kuwa na hatia? akamwambia, hakuna Bwana.
Yesu akamwambia wala mimi sikuhukumu. Endazako;
wala usitende dhambi tena." Nimapenzi ya Mungu tusizini. Imeandikwa katika
1Wathesa 4:3 "Maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu, kutakaswa kwenu, muepukane na usherati."
Yes, dunia inahitaji kizazi bora ili iendane na mfumo sahihi wa maadili