HAPA NDIPO YULE ASI ATAKAPOJITOKEZA
Pale waIsraeli wanapobadili nia na kuanza kuwa tayari
kupokea wokovu, muovu hatachelewa kuchukua nafasi hii ili kujitoa wazi na kazi yake akiwa masihi wa uongo.
Baada ya kunyakuliwa wale walio na imani,
hofu kuu na wasi wasi itakumba taifa lote la Israeli.
Hali hii itazidishwa na vita pale Israeli itakaposhambuliwa na jeshi ambalo ni muungano
wa mataifa adui wa jadi.
Katika
Ezekieli 38 na 39.
Kwa njia ya miujiza kabisa, Mungu atajitokeza na kuwaokoa waIsraeli kwa njia ya ajabu.
Yeye atawaangamiza maadui wao. Na hapo hapo pia muyahudi mmoja atajitokeza na kuanza kufanya maajabu.
Yeye atapokea shukrani na sifa kimakosa kwani wengi wataamini kwamba yale Mungu amefanya kuokoa taifa la Israeli,
yamefanyika kwa ajili ya uwezo wake.
Atajitokeza na kusema kwamba ni yeye mwokozi wa Wayahudi,
na kwamba ni yeye amewaokoa waIsraeli,
na kwamba ni kutokana na uwezo wake taifa hili limeepuka bala kuu.
Yeye atasema kwamba ndiye Masihi baada ya majadiliano na mikutano viongozi wa taifa watamkubali kuwa ni yeye Masihi.
Mwokozi wetu Yesu Kristo anasema hivi kuhusu jambo hili:
"Nimekuja kwa jina la Baba, na hamjanipokea,
naye yule anayekuja kwa jina lake mwenyewe, enyi mumemupokea"
(Yoh. 5:43).
Huyu muongo ambaye atajaribu kumuiga Masihi na kujaribu kuchukua mahali pake,
ndiye yule ambaye anakuja akiwa amepanda farasi mweupe na ni yeye mpinga Kristo.
Naye hatakawia kujitengenezea makao yake akiwa kiongozi, na atawapa ruhusa waIsraeli
wajengee upya hekalu.
Yeye atafanyia mzaha wokovu ule wale Wayahudi 144,000 wamepokea na kusema kwamba msingi
wa
imani ya hawa 144,000 ni msingi wa uovu ulio kinyume cha mapenzi ya Mungu.
Na akiwa kinyume na mapenzi ya Bwana kuhusu ufufuo wa kiroho, yeye ataelekeza
yote yaliyo ya kiroho kwenye njia ya zamani
(orthodox)
ambayo itahusu kujenga upya hekalu na mwanzo mpya wa matumizi ya sherehe na kafara mbaya.
Kwa ajili ya sababu zilizo wazi hapa, wale
wayahudi ambao wamepokea wokovu wa kweli watakosa kusikilizana na hawa ambao
msingi wao ni huyu masiya wa uongo ambaye amejitokeza.
Hawa wafuasi wa masihi muongo ndio watakuwa wengi.
Hata pale atakapojitokeza na kwenda katika mataifa mbali mbali akijifanya kuwa masiya,
na hapo kuanzisha muungano wa kidini, wengi bado kwa ajili ya kutojua wataungana
naye na kumfuata, na kushiriki naye katika uovu wake.
KUTAKUWA NA MASHAHIDI WAWILI
Wakati huu ambapo kutakuwa na harakati kubwa sana za kuwapotosha waIsraeli,
Mungu atawatuma mashahidi wawili ili kueleza taifa la Israeli kwamba ni jambo la muhimu wao kurudi kwake Mungu wa kweli.
Ufunuo 11:3-12.
Kuna dalili katika maandishi matakatifu kwamba huenda hawa wawili wakawa
Musa na Eliya
ambao walionekaa na Kristo katika mlima tunaona
katika Mathayo 17:1-3.
Na kuhusu Eliya, katika mistari miwili ya mwisho wa Agano la Kale twasoma hivi:
"Angalieni, nitawapekea Eliya nabii, kabla haijaja siku ile ya Bwana, iliyo kuu na kuogofya.
Naye ataigeuza mioyo ya Baba iwaelekee watoto wao,
na mioyo ya watoto iwaelekee baba zao, ili nisije nikaipiga dunia kwa laana"
Mal. 4: 5-6.
Malkia wa Amani Abadilika na Kuwa Fidhuli Pale muda wa dhiki kuu utakapofikia kati kati, makubaliano kati ya waIsraeli na Masihi huyu wa uongo yatavunjika
pale yeye atakapojitangaza kwamba ni yeye Mungu katika hekalu.
2 The. 2:4
"Yule pingamizi, ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu ama kuabudiwa;
hata yeye mwenyewe kuketi katika hekalu la Mungu, akijionyesha nafsi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu."
Akisaidiwa na yule nabii wa uongo,
yeye atajenga na kutengeneza picha yake katika sehemu takatifu zaidi ya yote
katika hekalu, na kulazimisha kila mtu kumuabudu.
Yeye atatupilia mbali kila aina ya maombi
katika hekalu hata ule mtindo maalum wa kuomba ambao zawadi hutolewa kwa Mungu.
Danieli anasema hivi :
"Naye atafanya agano thabiti na watu wengi kwa muda wa juma moja; na kwa nusu ya juma hiyo atakomesha sadaka na dhabihu;
na mahali pake litasimama chukizo la uharibifu;
na hivyo hata ukoma, na ghadhabu iliyokusudiwa imemwagwa juu yake mwenye kuharibu"
Dan. 9:27.
Kwa hivyo,
Danieli anasema wazi kwamba huyu mpinga Kristo atatupilia mbali utaratibu wa maombi ulioko na hata ule ambapo dhabihu
hutumiwa katika hekalu baada ya miaka tatu na nusu ya utawala wake.
Taifa lililo huzunika la Israeli litakataa kuendelea kumfuata huyu masihi wa uongo.
Taifa la Israeli ambalo limekasirishwa na huyu masihi wa uongo litakataa kumtii
huyu ambaye sasa atakuwa amejitangaza kuwa Mungu.
Na kwa ajili ya kufanya hivyo,
wao watamkasirisha huyu masihi wa uongo, naye atataka kukumbana nao na kuwaadhibu.
Yeye akiwa kama mungu atakuwa sawa na yule anayebebwa na yule farasi mwekundu.
Yeye atajitoa kupigana vita na kuangamiza taifa la Israeli na wote wale ambao si watiifu kwake na hawafuati mienendo yake.
Yeye atawaua mashahidi wawili ambao wamejitokeza na kuonya watu kuhusu uovu wake ( Ufunuo 11:7).
Pia yeye ataamuru wote walio na imani katika Kristo wauawe.
Kwa njia ya wazi kabisa, Kristo aliwaonya wayahudi kuhusu taabu itakayoletwa na huyu mpinga Kristo.
"Basi hapo mtakapoliona chukizo la uharibifu,
lile lililonenwa na nabii Danieli, imesimama katikl patakatifu (asomaye na afahamu) ndipo walio katika Uyahudi na wakimbilie milimani; naye aliye juu ya
dari asishuke kuvichukua vitu vilivyomo nyumbani mwake;
wala aliye shambani asirudi nyuma kuichukua nguo yake.
Ole wao wenye mimba na wanyonyeshao siku hizo!
Ombeni ili kukimbia kwenu kusiwe wakati wa baridi,
wala siku ya sabato.
Kwa kuwa wakati huo kutakuwapo dhiki kubwa ambayo haijatokea namna yake tangu
mwanzo wa ulimwengu hata sasa, wala haitakuwapo kamwe.
Na kama siku hizo zisingalifupizwa asingeokoka mtu yeyote; lakini kwa ajili ya wateule
zitafupizwa siku hizo"
Math 24:15-22.
Wakati huu wa dhiki kuu, Wayahudi wengi sana watauawa. Kuhusu jambo hili,
Zekaria anasema: "Hata, itakuwa ya kwamba katika nchi yote mafungu mawili yatakataliwa mbali.
Nao watakufa,
asema Bwana; lakini fungu la tatu litabaki humo"
Zek. 13:8.
Robo tatu itakayobaki itasafishwa na shida zile za dhiki, na pale Kristo atakaporudi,
kutakuwa na makubaliano naye.
Zekaria 13:9:
"Nami nitalileta fungu lile la tatu na kulipitisha katika moto,
nami nitawasafisha kama fedha isafishwayo,
nami nitawajaribu kama dhahabu ijaribiwavyo;
wataliitia jina langu, nami nitawaasikia; mimi nitasema,
watu hawa ndio wangu;
nao watasema, BWANA ndiye Mungu wangu."
WATAKIMBIA HUKU NA HUKO
Ufunuo 12
WaIsraeli watakimbilia jangwani. Hii itatokea pale baada ya hekalu kuchafuliwa,
na kutupiliwa mbali kwa makubaliano kati ya taifa la Israeli na Masihi huyu muongo.
Hili ni tukio ambalo litatokea pale katikati ya muda ule wa dhiki kuu.
Katika Ufunuo 12
ugomvi mkuu kati ya waIsraeli na yule mpinga Kristo unazungumziwa kwa njia maalum,
na hii itakuwa kati ya Ufalme wa Mungu na ule wa shetani.
Yohana anasema hivi kuhusu vita:
"Na ishara kuu ilionekana mbinguni, mwanamke aliyevikwa jua,
na mwezi ulikuwa chini ya miguu yake, na
juu ya kichwa chake taji ya nyota kumi na mbili.
Naye alikuwa na mimba, akilia, hali ana uchungu na kuumwa katika kuzaa.
Ikaonekana ishara nyingine mbinguni; na tazama,
joka kubwa jekundu, alikuwa na vichwa saba na pembe kumi, na juu ya vichwa vyake,
vilemba saba.
Na mkia wake wakokota theluthi ya nyota za mbinguni, na kuziangusha katika nchi.
Na yule joka akasimama mbele ya yule mwanamke aliye tayari kuzaa, ili, azaapo,
amle mtoto wake.
Naye akazaa mtoto mwanamume, yeye atakyewachunga mataifa yote kwa fimbo ya chuma.
Na mtoto wake akanyakuliwa hata kwa Mungu,
na kwa kiti chake cha enzi.
Yule mwanamke akakimbilia nyikani, ambapo ana mahali palipotengenezwa na mungu,
ili wamlishe huko muda wa siku elfu na mia mbili sitini"
Ufu. 12:1-6.
Hapa taifa la Israeli lachukuliwa kuwa sawa na mama aliyeolewa,
sio kama mchumba bikira kama vile kanisa la Kristo lilivyo
(Yer. 31:1-5; Isa. 54:4-8; Hos. 2:15; Mat. 25:1-13; na 2 Kor. 11:2).
Huyu mwanamke anatajwa pia na kusemekana kuwa atakuwa na
nyota kumi na mbili
katika kichwa chake,
na hii ni alama ya makabila kumi na mbili ya Israeli,
pamoja na jua na mwezi ambavyo vimemlenga
Yakobo na Raheli
kama ni wao watu wa kwanza katika taifa la Israeli.
Haya yote yanaweza kulinganishwa na yale yaliyo
katika ndoto ya Yusufu katika Mwanzo ambapo tunasoma hivi:
"Akaota tena ndoto nyingine, akawaambia ndugu zake,
akasema,
angalieni, nimeota ndoto nyingine;
na tazama, jua na mwezi na nyota kumi na moja zikaniinamia.
Akawambia baba yake na ndugu zake;
baba yake akamkemea akamwambia,
Ni ndoto gani hii uliyoiota?
Je! mimi na mama yako na ndugu zako tutakuja tukusujudie hata nchi?"
Mwa 37:9-10;
soma pia Yer. 31:11 na 15 ambapo Yakobo na Raheli wanachukuliwa kuwa kama taifa la Israeli).
Mimba ile ya mama huyu yaweza kuchukuliwa kumaanisha wakati ule wa kuzaliwa Kristo.
Yule mnyama ambaye anajiweka tayari kumla mtoto anapozaliwa bila shaka ni muovu shetani mwenyewe.
Wakati huu, mfalme muovu ni yule Herode.
Ndiye aliyeamua kwamba watoto wote wakiume
wauliwe ili mwokozi wetu Yesu Kristo auliwe.
Hata hivyo Mungu alikuja na kutenda kazi
ya ajabu hapa duniani pale alipofanya kazi yake kuu na kurudi mbinguni kwake BABA yetu aliye Juu.
Muda wake ule wa kutawala na nguvu kabisa utaanza pale atakaporudi mara ya pili.
Ufunuo 2:26-27.
Mpaka pale Kristo atakapokuja tena, muovu shetani anaelekeza nguvu zake zote
kujaribu kupinga ufalme wa Mungu, taifa la Israeli na kanisa.
Baada ya kanisa kunyakuliwa,
yeye sasa atalipatia nguvu zake kwa taifa la Israeli,
kwanza kuhadaa, na baadaye kuangamiza taifa la Israeli ili mpango wa Mungu utimizwe.
Ni wakati huu taifa la Israeli litaamriwa kukimbilia jangwani,
labda kukimbilia Petra ili kuepuka dhiki kuu.
Huko Mungu atawalinda kwa muda wa siku 1260,
ambazo ni kama miaka tatu na nusu.
Hii tunaiita ile miaka mitatu na nusu ya kwanza ya utawala wa mpibgs Kristo,
Itakuwa miaka yautawala wa amani.
Barikiwa sana mpendwa wangu
Guatana nsmi tu usichoke......
Ni mimi ndugu yako
Ev. Elimeleck S Ndashikiwe