NAMNA YA KUPATA WOKOVU (KUOKOKA)
HATUA YA KWANZA;
TAMBUA KUWA WEWE NI MWENYE DHAMBI NA UTUBU DHAMBI ZAKO, KWA KUMAANISHA KUZIACHA.
“Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti, bali karama ya Mungu ni uzima wa milele”
(Rum 3:23).
“Tubuni, mkabatizwe kila mmoja kwa jina la Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu,
nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.”
(Mdo 2:38)
HATUA YA PILI;
MWANINI NA KUMPOKEA YESU MOYONI MWAKO. TOA MAISHA YAKO KWAKE,
AWE BWANA NA MWOKOZI WAKO.
Yule mlinzi wa gereza akamwambia Paulo na Sila
“Bwana zangu, yanipasa nifanye nini nipate kuokoka?
Wakamwambia, mwamini Bwana Yesu, nawe utaokoka pamoja na nyumba yako”
Mdo 16:30-31.
“Kwasababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni
mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu,
UTAOKOKA.
Kwa maana moyo mtu huamini hata kupata haki,
na kwa kinywa hukiri, hata KUPATA WOKOVU.
Rum 10:9-10)
HATUA YA TATU: ISHI MAISHA YA WOKOVU,
MAISHA SAFI YA KUMPENDEZAMUNGU NA KUZISHIKA AMRI ZAKE
(NENO LAKE)
“nawaandikia haya ili kwamba msitende dhambi…
Na katika hili twajua ya kuwa tumemjua yeye (Mungu) ikiwa tunashika amri zake. Lakini Yeye asema neno lake,
katika huyo upendo wa Mungu umekamilika
kweli kweli, katika hili twajua ya kuwa tumo ndani yake….”
1Yoh 2:1-6.
Kwahiyo sasa, anza maisha mapya ndani ya Yesu.
“…mtu akiwa ndani ya Kristo, amekuwa kiumbe kipya, ya kale yamepita, tazama! Yamekuwa mapya”.
2Kor 5:17.
Jitenge na uovu wote na Usiishi katika maisha ya dhambi tena.
Pia soma
Josh 1:8 na
Rum 6:1-23.
MAMBO 12 YALIYOKUTOKEA MAISHANI MWAKO
BAADA YA KUMPOKEA YESU AWE BWANA NA MWOKOZI WAKO.
Mpendwa,
nataka ujue kwamba, Mungu amefanya mambo mengi makubwa katika maisha yako,
tangu saa/siku ile ulipompokea Yesu, kuwa Bwana na Mwokozi na Mwokozi wako.
Ni muhimu uelewe kwamba, wewe si yule wa zamani tena.
Sahau yaliyopita, kwasababu umefanyika kiumbe kipya.
2 kor 5:17.
Yafuatayo ni baadhi ya mambo yaliyotokea kwako tangu ulipofanya uamuzi
huu mzuri na wa busara, wa kumpokea Yesu Kristo,
kuwa Bwana wako na Mwokozi wa maisha yako. KWANZA:
UMEFANYIKA MWANA WA MUNGU
Umefanyika mwana wa Mungu, kwasababu umempokea Yesu Kristo na kuliamini
Jina lake; Kwasababu Biblia inaema “Bali wote waliompokea, aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake
Yoh 1:12.
… Roho (Mtakatifu) mwenyewe, hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa
sisi tu watoto wa Mungu…”
Rum 8:16.
Tangu sasa, wewe ni mmoja wa wana-familia ya Mungu.
Nasi tunakukaribisaha kwa upendo wa Kristo. Karibu sana, Baba (Mungu) na sisi tumefurahi kukuona umerudi nyumbani.
"(This is where you belong. We missed you so much)",
Karibu!
PILI:DHAMBI ZAKO ZOTE ZIMEOSHWA NA
KUSAFISHWA KWA DAMU YA YESU NA UMESAMEHEWA KABISA.
Biblia inasema, dhambi zako zote zimeoshwa na kusafishwa kwa damu ya Yesu naumesamehewa zote kabisa, kwasababu
umekuja kwa Yesu na umekiri dhambi zako;
Kwa maana imeandikwa
“katika yeye huyo (Yesu), kwa damu yake, tunao ukombozi wetu,
msamaha wa dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake
Efe 1:17.
… Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa nyeupe kama sufu
(Isa 1:18)
… maana nitausamehe uovu wao, wala dhambi yao sitaikumbuka tena.”
(Yer 31:34b)
pia soma: Kor 1:14, Ufu 1:5.
TATU:
UMEFANYIKA KIUMBE KIPYA
“Hata imekuwa mtu akiwa ndani ya Kristo;
amekuwa kiumbe kipya; (mambo ya kale yamepita Tazama! Yamekuwa mapya (2Kor 5:17)…
Najua neno moja kuwa, mimi nilikuwa kipofu, na sasa ninaona”
Yoh 9:25
Kwahiyo sahau maisha yaliyopita, sasa anza maisha mapya ndani ya Yesu.
NNE:
ROHO MTAKATIFU ANAISHI NDANI YAKO NA ATAKUWA PAMOJA NAWE MILELE
“Mkinipenda,
mtazishika amri zangu. Nami nitamwomba Baba (Mungu), naye atawapa msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele;
Ndiye Roho wa kweli, ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwakuwa haumwoni wala haumtambui, Bali ninyi
mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu”.
Yoh 14:15-17)
“… Hamjui yakuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu?
Na yakuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu? Kama mtu alikiharibu hekalu la Mungu,
Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi.”
1Kor 3:16-17)
TANO:
UMEHAMISHWA KUTOKA KATIKA NGUVU ZA
HETANI au MAMLAKA YA SHETANI au UFALME WA SHETANI, NA KUINGIZWA KATIKA UFALME (MAMLAKA) WA YESU KRISTO.
“Naye (Mungu Baba) alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza
katika ufalme wa mwana wa Pendo lake (Yesu Kristo)”
Kol 1:13.
“Nanyi mfahamu kwamba, mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo, kwa fedha au dhahabu, mpate kutoka katika
mwenendo wenu usiofaa …”
1Pet 1:18.
SITA:
UMEHAMISHWA KUTOKA MAUTINI KUINGIA UZIMANI
“Amini amini nawaambia, yeye aliskikiaye neno langu, na kumwamini yeye aliyenipeleka, yuna (ana) uzima wa milele,
wala haingii hukumuni, bali amepita kutoka mautini kuingia uzimani .
Yoh 5:24)
“Sisi tunajua yakuwa tumepita kutoka mautini kuingia uzimani…”
(1Yoh 3:14).
Sasa
basi, hakuna hukumu ya adhabu, juu yao walio katika kristo Yesu; kwasababu sheria
ya Roho wa uzima, ule ulio katika kristo Yesu, imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti.
Rum 8:1-2.
SABA:
UMEOKOLEWA AU UMEOKOKA KUTOKA KATIKA GHADHABU NA ADHABU YA MUNGU.
“Kwa maana, ikiwa Mungu hakuwaachilia malaika waliokosa, bali aliwatupa
shimoni, akawatia katika vifungo vya giza,
walindwe hata ije hukumu. Wala hakuachilia ulimwengu wa kale, bali alimhifadhi
(alimwokoa) Nuhu mjumbe wa haki, na watu wengine saba,
hapo alipoleta gharika, juu ya ulimwengu wa wasiomcha Mungu.
Tena akaihukumu miji ya Sodoma na gomora,
akiipindua na kuifanya majivu. Akaifanya iwe ishara kwa wtu watakaokuwa hawamchi Mungu baada ya hayo”
(2 Pet 2:4-6)
“Dunia ile ya wakati ule, iligharikishwa kwa maji ikaangamia, lakini mbingu zasasa na nchi,
zimewekwa akiba kwa moto, kwa neno lilohilo, zikilindwa hata siku ya hukumu, na (siku)
ya kuangamia kwao, wanadamu wasiomcha Mungu …
Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyodhani kukawia, bali huvumilia
kwenu, maana hapendi mtu yeyote apotee, bali wote wafikie toba …waokolewe na kupata kujua yaliyo kweli.
2Pet 3:6-7;
1Tim 2:4.
“Lakini siku ya Bwana itakuja kama mwizi katika siku hiyo, mbingu zitatoweka
kwa mshindo mkuu na vioumbe vya asili vitaunguzwa na kufumuliwa na nchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea…. mbingu
zitfunuliwa, zikiangua na viumbe vya asili vitateketea na kuyeyuka.
Lakini kama ilivyo ahadi yake, tunatazamia mbingu mpya na nchi mpya, ambayo
haki yakaa ndani yake. .
2Pet 3: 9 -13.
Basi zaidi sana tukiisha kuhesabiwa haki, katika damu yake (Yesu),
tutaokolewa na ghadhabu kwa yeye.
(Rum 5:9)
(Kwahiyo)ukimkiri Yesu kwa kinywa chako na kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni
mwako yakuwa Mungu alimfufua katika wafu,
utaokoka kwa maana,
kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, Na kwa kinywa mtu hukiri, hata kupata wokovu,
(Rom 10:9 -10)
Kwa maana mmeokolewa (sio, mtaokolewa) bali; MMEOKOLEWA kwa neema,
kwa njia ya imani, ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu, wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije
akajisfu.
Efe 2:8.
Maana neema ya Mungu, iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa
Tito 2:11)
na itakuwa,
kila atakayeliitia jina la Bwana, ataokolewa (Mdo 2:21) ….
(Petro)Akawashuhudia kwa maneno mengine mengi sana na kuwaonya; akisema, jiokoeni na kizazi hiki chenye ukaidi
(Mdo 2:40)
Walipoyasikia haya, wakachomwa mioyo yao, wakmwambia Petro na mitume wengine;
Tutendeje ndugu zetu? Petro akawaambia,
Tubunimkabatizwe, kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu nanyi mtapokea kipawa cha Roho mtakatif
(Mdo 2:37-38).
Nao waliopokea neno lake, wakabatizwa.
Na siku ile wakaongezeka watu (waume) wapata
elfu tatu (41)………
Bwana akalizidisha kanisa kila siku, kwa wale waliokuwa wakiokolewa
Mdo 2:47
NANE:
JINA LAKO LIMEANDIKWA KATIKA KITABU CHA UZIMA.
“Lakini msifurahi kwa vile peopo wanavyowatii,
bali furahini kwa sababu majina yenu yameandikwa mbinguni (Luk 10:20)…“Na ndani
ya mji mtakatifu) hakitaingia kamwe chochote kilicho kinyonge, wala yeye afanyaye
machukizo na uongo, bali wale walioandikwa katika kitabu cha uzima cha mwanakondoo”
(Ufu 21:27)
…“Na iwapo mtu yeyote, hakuonekan ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto”
Ufu 20:15)
…“Naam, nataka na wewe pia, mjoli wa kweli,
uwasaidie wanawake hao, maana waliishindania injili, pamoja nami, na wale
waliotenda kazi pamoja nami, ambao majina yao yamo katika kitabu cha uzima
Fil 4:3)
TISA:
UMEPEWA (UNAZO) NGUVU NA MAMLAKA
YOTE JUU YA SHETANI NA NGUVU ZOTE ZA GIZA.
Hata wakati ule tulipokuwa wafu kwasababu ya makosa yetu, alituhuisha pamoja na Kristo;
yaani, tumeokolewa kwa neema.
Akatufufua pamoja naye, akatuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho, katika kristo Yesu.
(Efe 2:5-6)
….. juu sana kuliko ufalme wote, na mamlaka, na nguvu, na usultani, na kila jina (au cheo)
litajwalo
(Efe1:21)
(akasema)
”Tazama nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge,
na nguvu zote za yule adui (shetani), wala hakuna kitu kitakachowadhuru
(Luk 10:19)
… “Nami nitakupa funguo za ufalme wa mbinguni, na lolote utakololifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni, na
lolote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni
Math 16:19.
… Angalia, nimekuweka leo juu ya mataifa na juu ya falme, ili kung’oa, na kubomoa,
na kuharibu, na kuangamiza, ili kujenga na kupanda
Jer 1:10.
Kila mahali utakapopakanyaga nyayo za miguu yenu,
mimewapa ninyi …. hapatakuwa mtu yeyote atakeyeweza kusimama mbele yako,
siku zote za maisha yako; kama ulivyokuwa pamoja na Musa, ndivyo nitakanyokuwa pamoja na wewe; sitakupungukia wala sitakuacha
Josh 1:3,5)
… Muwe na kiasi na kukesha; kwakuwa mshitaki wenu ibilisi, kama simba aungurumaye,
huzunguka zunguka, akitafuta mtu ammeze. Nanyi mpingeni huyo mkiwa thabiti katika imani … (Basi mtiini Mungu. Mpingeni shetani, naye atawakimbia
(Yak 4:7)
… “Na ishara hizi, zitafuatana na hao waaminio,
kwa jina langu watatoa pepo, watasema kwa lugha mpya; watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha (kuua), hakitawadhuru
kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya
Mk 16:17-18)
Pia soma:
Dan 7:13,14,27; Yer 51:20 .
KUMI:
UNALINDWA KWA ULINZI WA MALAIKA WA MBINGUNI
Malaika wa Bwana hufanya kituo, akiwaangalia wamchao (Mungu) na kuwaokoa
Zab 34:7.
…“Kwakuwa (Mungu) atakuagizia malaika zake, wakulinde katika njia zako zote
(Zab 91:11) …
Je? hao (Malaika) wote si roho watumikao,
wakitumwa kuwuhudumia wale watakaourithi wokovu?
Ebr 1:7,14.
Nani (Yohana) nikaanguka mbele ya miguu yake
(Malaika) ili nimsujudie; akaniambia, angalia, usifanye hivi, mimi (Malaika) ni nyoli (Mtumishi) wako na w ndugu zako walio na ushuhuda wa Yesu. Msujudie Mungu…
Ufu 19:10.
… Awagusaye ninyi, aigusa mboni ya jicho lake
(Mungu). Kwa maana, tazama, nitatikisa mkono wangu juu yao …
Zek 2:8-10).
Nanyi mnalindwa na nguvu za Mungu, kwa njia ya imani…
1Pet 1:5.
KUMI NA MOJA:
UMEFANYIKA MTUMISHI WA MUNGU.
Watu
wengi waliookoka hawajioni au hawajihesabu kuwa ni watumishi wa Mungu.
Bali huwaona Wachungaji na Wainjilisti kuwa ndio watumishi wa Mungu. Pengine na wewe unajiona hivyo.
Lakini neno la Mungu linasema; SisiKanisa (Yaani:
Jamii ya waaminio au watu waliookoka), sote kwa pamoja, ni mwili wa Yesu Kristo …
Mungu alipomfufua Yesu Kristo kutoka katika wafu, alimtukuza, akamweka mkono wake wa kuume katika ulimwengu wa roho;
Juu sana kuliko falme zote na mamlaka zote, “Akavitia vitu vyote chini ya miguu yake. Akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote, kwa ajili ya kanisa, ambalo ndilo mwili wake…”
Efe 1:20-23
“Naye (Yesu) ndiye kichwa cha mwili, yaani cha kanisa….
Kol 1:18) …
Basi ninyi nimekuwa mwili wa Kristo, na viungo kila kimoja peke yake… kwa maana katika Roho mmoja, sisi sote tulibatizwa kuwa mwili mmoja, kwamba tu wayahudi,
au kwamba tu wayunani; ikiwa tu watumwa,
au ikiwa tu huru; Nasi sote tulinyweshwa Roho mmoja, kwa maana mwili si kiungo kimoja,
bali ni vingi…
Maana kama vile mwili ni mmoja, nao una viungo vingi, na vioungo vyote vya mwili ule navyo ni vingi, na viungo vyote vya
mwili ule navyo ni vingi, ni mwili mmoja, vivyo hivyo na Kristo.
Kor 12,27,13-14,12
… “Basi pana tofauti za karama; Bali Roho ni (mmoja).
Tena pana tofauti za huduma, (lakini) Bwana ni mmoja.
Kisha pana tofauti za kutenda kazi, bali Mungu ni (mmoja) azitendaye kazi zote katika wote.
Lakini Kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa kusaidiana.
1kor 12:4-7.
Angalia hili neno “kila mmoja” “…Mungu amevitia viungo kila Kimoja katika mwili, kama alivyotaka.
Lakini kama vyote vingekuwa kiungo kimoja,
mwili ungekuwa wapi?
Lakini sasa viungo ni vingi, ila mwili ni mmoja. kila mmoja katika mwili, kama alivyotaka.
Lakini kama vyote vingekuwa kiungo kimoja, mwili ungekuwa wapi? Lakini sasa
viungo ni vingi, ila mwili ni mmoja.
“(1Kor 12:18-20
Angalia hilo neno tena “kila kimoja” limejirudia.
“ Maana mtu mmoja kwa Roho apewa neno la hekima; na mwingine neno la maarifa
(kama) apendavyo Roho yeye yule; mwingine (hupewa) imani katika Roho (huyo huyo);
na mwingine hupewa kaama za kuponya katika Roho yule mmoja; na mwingine (hupewa) unabii;
na mwingine (hupewa) kupambanua roho; na mwingine (hupewa) aina za lugha;
na mwingine (hupewa) tafsiri za lugha; Lakini kazi hizi zote,
huzitenda Roho huyo mmoja, yeye yule, akimgawiakila mtu peke yake, kama apendavyo yeye.
(!Kor 12:8-11)
Angalia hilo neno “kila mmoja” limejirudia tena Kwa hiyo, kama vile katika mwili, kila kiungo kina kazi yake (ya kujenga mwili);
Vivyo hivyo,
katika mwili wa Kristo, yaani Kanisa, kila muumini, ana kazi yake ana huduma yake,
na karama yake na wajibu wake, katika kujenga mwili wa Kristo.
Wewe na mimi, tu watumishi wa Mungu.Jione hivyo na ujihesabu hivyo. Mungu anataka utumie karama na uwezo aliokupa,
ili kuuvunja ufalme wa shetani, na kujenga ufalme wa Kristo duniani. Neno la Bwana likamjia,
kusema, kabla sijakuumba katika tumbo, nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa;
Nimekuweka kuwa nabii wa Mataifa. Ndipo niliposema, Aah! Bwana Mungu! Tazama,
siwezi kusema; maana mimi ni mtoto lakini Bwana akaniambia, usiseme mimi ni mtoto;
… usiogope kwasababu ya hao, maana mimi nipo pamoja nawe nikuokoe, asema. Bwana.
Ndipo Bwana,
akanyoosha mkono wake, akanigusa kinywa changu; Bwana akaniambia; Tazamani,
nimetia maneno yangu kinywani mwako; Angalia, nimekuweka leo juu ya mataifa na juu ya falme, ili kung’oa, na kubomoa, na kuharibu,
na kuangamiza; Ili kujenga na kupanda
Yer 1:4 -10.
“… enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi (wangu) mkiwabatiza kwa
jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu;
Nakuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja
nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.
Math 28:18-20.
KUMI NA MBILI:
UMEPEWA AHADI KUBWA MNO NA ZA THAMANI NA MUNGU
Tangu umeingia katika familia ya wana wa Mungu umepewa urithi wa baraka za Mungu.
Umeingizwa katika mkondo wa baraka na ahadi kubwa na nyingi mno katika kriso Yesu.
“Na kwa kuwa ninyi mmekuwa wana (wa Mungu), Mungu alimtuma Roho wa mwanawe
mioyoni mwetu, aliaye Aba, yaani Baba. Kama ni hivyo, wewe si mtumwa tena, bali u
mwana (wa Mungu);
Na kama u mwana, basi u mrithikwa Mungu”
Gal 4:6-7
“Kristo alitukomboa katika laana ya torati, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu…,
ili kwamba, Baraka ya Ibrahimu, iwafikie mataifa ktika Yesu Kristo, tupate kupokea ahadi ya roho kwa njia imani … Na
kama ninyi ni wa kristo, basi mmekuwa uzao wa Ibrahimu, na warithi sawa sawa na ahadi”
Gal 3:13-14,29.
“Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa Baraka zote za rohoni, katika ulimwengu waro ho,
ndani yake Kristo.
Efe 1:3)…
Tena kwa hayo, ametukirimia ahadi kubwa mno za thamani, ili kwamba, kwa hizo
(ahadi na baraka) mpate kuwa washirika wa tabia ya Uungu, mkiokolewa
na uharibifu uliomo duniani, kwa sababu ya tamaa.”
2Pet 1:4
Kwa mfano:-
Ahadi ya Baraka
– Kumb 28:1 – 14; Law 26:1-13
Ahadi ya mafanikio
– Zab 1:1 -3; Josh 1:8-9
Ahadi ya utajiri
– Kumb 15:14; 2Kor 8:9 / 2Kor 9:8,11
Ahadi ya Afya njema
– Kut 15:26: Kumb 7:15
Ahadi ya Ulinzi
– Zab 91:11; Zab 121:1-8
Ahadi ya Akili nzuri
– Zab 119:97-100; Zab 111:10
na
Ahadi ya Wokovu kwa familia - Mdo 16:31; Isa 54:13 – 14
Nasihi ulinzi wake Mungu ukawe juu yako sasa ktkt jina la Yesu Kristo
Ameeeeeen.
Ndo mimi
Ev. Elimeleck S Ndashikiwe.