Saturday, 26 September 2015
IMANI KALI
Friday, 25 September 2015
UTHAMANI WA DAMU YA YESU
Damu ya Yesu ina nguvu sana!
Lakini je unajua ni kwa nini ilimwagika katika maeneo tofauti tofauti ya mwili wake? Kwa mfano, tunasoma ya kuwa; “Hata zilipotimia siku nane za kumtahiri, aliitwa jina lake Yesu; …” (Luka 2:21).
Tena imeandikwa katika wakolosai 2:11 ya kuwa: “Katika yeye mmetahiriwa kwa tohara isiyofanyika kwa mikono, kwa kuuvua mwili wa nyama, kwa tohara ya Kristo”.
Hii inaonyesha ya kuwa kutahiriwa kwa Kristo kulikuwa sii tu kwa ajili yake; bali ilikuwa pia kwa ajili yetu sisi tunaomwamini kama mwokozi wetu! Na alipotahiriwa, damu yake ilimwagika!
Jambo hili la kutahiriwa, lilianza wakati wa Ibrahimu (Kama ishara ya mtu kukubali kuingia katika agano na Mungu wa Ibrahimu) Wakati wa kipindi cha Musa, jambo hili liliingizwa kama agizo la Torati. Hili ndilo lililowafanya “baadhi ya madhehebu ya Mafarisayo” waliokuwa wameokoka, kuwaelekeza wale wasiotahiriwa ya kuwa; “msipotahiriwa kama desturi ya Musa hamwezi kuokoka” (Matendo ya Mitume 15: 1,5)
Jambo la kutahiriwa au kutokutahiriwa kwa jinsi ya mwili, lilikuwa chanzo kikubwa sana cha malumbano na kutokushirikiana kwa Kanisa la Mwanzo Mitume walijitahidi kulisuluhisha jambo hili waliloliita “Kongwa juu ya Shingo” (Matendo ya Mitume 15:10), kwa kuweka msisitizo wa damu ya Yesu kusafisha mioyo yetu, na kutupa tohara ya rohoni, na kutupa kukubalika mbele za Mungu kwa kufanana.
Soma katika: Warumi 2: 25 – 29;, Waefeso 2: 11 – 13.
Damu ya Yesu inatupa kuingia katika agano jipya (Luka 22:20),
na kutufanya uzao wa Ibrahimu kwa njia ya Yesu Kristo
(Wagalatia 3:13, 14, 29) -Yesu Kristo alipokuwa anatahiriwa, ilikuwa ni ishara ya kuwa damu yake ina nguvu ya kutuweka mbali na mapokeo ya dini yaliyo kongwa juu ya shingo za watu! Damu ya Yesu ina uwezo wa kutuingiza katika uhusiano na Mungu, kwa njia ya agano jipya! Kwa hiyo, damu ya Yesu inaweza kutumika kuondoa kile kinachofanya wakristo washindwe kushirikiana vyema, kwa sababu tu ya tofauti za mapokeo yao!
Hili limekuwa ni tatizo hata sasa baadhi ya makabila
wamelifanya kama sehemu ya pokeo
kanisani.
Wanapotahiri watoto wao
wanataka na kanisa lihusike
kwaya zikaimbe kwa familia husika.
Wamelishika kama agano
wasijue kuwa ni Kongwa la Utumwa.
MUNGU WANGU WA MBINGUNI AKUBARIKI MPENDWA WANGU
Ni mimi rafiki yako
Ev. ELIMELECK S NDASHIKIWE
+255767445846
+255715445846
elimelck@gmail.com.
KUREJESHEWA NAFASI YAKO
Mwanzo 25: 21-34………Yakobo akamwambia,kwanza niuzie leo haki yako ya mzaliwa wa kwanza……………..Yakobo akamwambia, uniapie kwanza . Naye akamwapia, akamwuzia Yakobo haki yake ya mzaliwa wa kwanza……………. Tunaona historiya ya watoto wawili ambao walikuwa wanapendwa na wazazi wao lakini mtoto mmoja anapenda kuliko mwingine. Tunaona kuwa tangu kipindi cha ibrahimu alikuwa hana mtoto na alipokuja kupata mtoto alikuwa mbarikiwa naye alikuwa ndiye Isaka,naye Isaka anapata mke naye anakuwa tasa kwa muda mrefu alipokuja kupata watoto wawili mapacha Mungu akamwambia una mataifa mawili ndani yako. Mungu aliona wale watoto wawili kuwa mataifa mawili makubwa,taifa moja litamtumikia mwingine naye alikuwa akiimanisha kuwa taifa moja litakuwa hodari na mkubwa atamtumikia mdogo. Mwanzo 27:1-40 Tunaona rebeka anamwambia mwanae mdogo achukue Baraka ya kaka yake na mama anakubari kuchukua laana naye akamchukulia mavazi mazuri ya esau naye yakobo akaenda akachukua baraka ya Esau. Isaka alimpenda Esau kwa sababu alikuwa anakula mawindo yake lakini biblia haijatuambia Rebeka alimpenda Yakobo,huu sio upendo mzuri maana anakula mawindo yake lakini wakati wa baraka alifukuziwa mbali lakini rebeka alimpenda yakobo basi hatuoni alimpendea kwa kitu gani. Esau alikuwa ni mtu wa nyikani na Yakobo alikuwa mtu wa shambani ,mtu wa mtulivu na Isaka alimwamini Esau kwa mapishi kwa namna haipendayo kuliko Rebeka ndio mana alikuwa anapenda chakula Esau naye rebeka alimpenda yakobo kwakuwa esau alichukua nafasi yake ya mapishi. Rebeka aliyashikilia yale maneno ambayo aliambiwa kuwa ndani ya tumbo lako kuna mataifa mawili na mkubwa atamtumikia mdogo. Yakobo alikuwa mkulima na Esau alikuwa mwindaji,yakobo alikuwa hali mbegu lakini esau alikuwa anakula mbegu kwanini maana alikuwa anawinda mawindo na lazima amjerui na kumchinja kulekule porini na kuja na nyama nyumbani ili wale. Leo hii wapo watu wengi wanakula mbegu na wanataka Mungu awabariki,Mungu hawezi kukubariki kwa namna hiyo kama unakula mpaka zaka na dhabihu. Esau aliuza haki yake ya mzaliwa wa kwanza kwaajili ya dengu la siku moja naye akuzingatia baraka ya mzaliwa wa kwanza Kuna wakati watu wanauza Baraka za mzaliwa wa kwanza kwa shetani wakizani kuwa ndio wanaingia kwenye mafanikio uku wakiona kuwa yale waliyatoa kuwa hayana maana sana.
Ni mimi rafiki yako
Ev. ELIMELECK S NDASHIKIWE
elimelck@gmail.com
+255767445846
+255715445846
Thursday, 24 September 2015
MSAMAHA NI MLANGO WA MUUJIZA WAKO
Wednesday, 23 September 2015
WAZAZI MTULEE VEMA
UWEZO WA KUSIMAMA KATIKA NAFASI YAKO
NGAO YA IMANI KWA MWAMINI
NGUVU YA IMANI
Sunday, 20 September 2015
UWEZA WA DAMU YA YESU
Damu ya Yesu ilitustahilisha
na
kutupatia kibali cha kupasogea patakatifu.
Mungu amekuwa mwaminifu kulikomaelezo.
Saturday, 5 September 2015
MAMBO MANNE(4) YA KIJANA MTEULE KUZINGATIA.
Na Mtumishi Peter Mabula |
BWANA YESU atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze mambo muhimu ya kuzingatia kwa kijana na kila mpenda uzima wa milele.
Kuna mambo manne nimekuandalia ambayo ukiyazingatia yatakuwa msaada mkubwa kwako.
2 Timotheo 2:21-26 '' Basi ikiwa mtu amejitakasa kwa kujitenga na hao, atakuwa chombo cha kupata heshima, kilichosafishwa, kimfaacho BWANA, kimetengenezwa kwa kila kazi iliyo njema. Lakini zikimbie tamaa za ujanani; ukafuate haki, na imani, na upendo, na amani, pamoja na wale wamwitao BWANA kwa moyo safi. Walakini uyakatae maswali ya upumbavu yasiyo na elimu, ukijua ya kuwa huzaa magomvi.Tena haimpasi mtumwa wa BWANA kuwa mgomvi; bali kuwa mwanana kwa watu wote, awezaye kufundisha, mvumilivu; akiwaonya kwa upole wao washindanao naye, ili kama ikiwezekana, Mungu awape kutubu na kuijua kweli; wapate tena fahamu zao, na kutoka katika mtego wa Ibilisi, ambao hao wametegwa naye, hata kuyafanya mapenzi yake. ''.
Vitu 4 vya kuvizingatia kijana mteule wa MUNGU.
1. Kijana lazima aitafute toba kwa MUNGU kupitia KRISTO YESU na akisha kutakaswa atakuwa chombo safi kifaacho kwa kila kazi njema na tena kitakuwa chombo safi kimfaacho MUNGU.
-Toba hutafutwa maana haiji yenyewe kama hujaamua kuitafuta kwa BWANA YESU kupitia maombi ya kutubu na kuacha dhambi. ukisha kuupata msamaha wa MUNGU unatakiwa uutafute utakatifu. utakatifu hutafutwa tena hutafutwa kwa bidii sana. usipoutafuta utakatifu utabaki mchafu siku zote na hapo hutakuwa chombo safi kimfaacho BWANA. Utakatifu hauji wenyewe bali hutafutwa hivyo kila kijana ni muhimu sana kuutafuta utakatifu.
1 Petro 1:15-16 '' bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote; kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu. ''
-Iweni watakatifu maana yake ni jukumu lako kuwa mtakatifu.ni agizo kwako kuutafuta utakatifu ili uuishi.
2. Kijana lazima azikimbie tamaa za ujanani.
Tamaa za ujanani ni pamoja na uasherati, kutafuta mali isivyo kihalali, kufanya kila mbinu chafu ili tu uwe kama mtu mwingine, kujiona unao muda mrefu wa kuishi na hivyo kuona kwamba ujana wako ni wakati wa kutenda mabaya ukidhani utatubu uzeeni. hizo ni tamaa za ujanani na Biblia inatuonya kwamba tuzikimbie tamaa za ujanani. Kila kijana lazima ahakikishe anakimbia tamaa za ujanani.
Biblia hapo juu pia imefafanua kwamba tamaa za ujanani zinaweza kuondoa haki, Tamaa za ujanani zinaweza kukuondoa katika imani ya uzima ambayo ni imani katika KRISTO YESU pekee. , Tamaa za ujanani zinaweza kuondoa upendo, Tamaa za ujanani zinaweza kuondoa amani kwako, kwa familia, kwa ukoo na hata kwa taifa.
Kumbe pia Biblia inatushauri vijana kutenda kazi ya MUNGU pamoja na wale wamwitao BWANA kwa moyo safi.
-Kama kijana hatazikimbia tamaa za ujanani ni lazima huyo baadae atakuja kuwaambia watu kwamba '' UJANA NI MAJI YA MOTO''. Ujana umekua maji ya moto kwake kwa sababu hakuzikimbia tamaa za ujanani kama Biblia takatifu inavyoagiza.
1 Yohana 2:15-17 '' Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda BABA hakumo ndani yake. Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na BABA, bali vyatokana na dunia. Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya MUNGU adumu hata milele. ''
3.Kijana mteule ni muhimu kuyakataa maswali ya kipumbavu ambayo siku zote huibua ugomvi na kumnajisi kijana.
-Maswali ya kipumbavu yasiyo na elimu ni mengi hivyo kijana mwenda mbinguni lazima ajiepushe nayo.
Kama ni maswali ya kipumbavu maana yake yanasemwa na mpumbavu, na maana ya mpumbavu ni mtu yule asiyeamini katika MUNGU aliye hai, maana yake mpumbavu hudhani kwamba hakuna MUNGU au hakuna uzima wa milele au hakuna kuokoka.
Zaburi 14:1 '' Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna MUNGU; Wameharibu matendo yao na kuyafanya chukizo, Hakuna atendaye mema.''
-Sifa za mpumbavu husema hakuna MUNGU, Hufanya machukizo na matendo yake ni machukizo kwa MUNGU hivyo uijiepushe na maswali ya kipumbavu maana yanaweza hata kukuondoa katika kusudi la MUNGU.
4. Kijana uliyempokea YESU hutakiwi kuwa mgomvi bali mwanana na mvumilivu kuku ukiwafundisha watu uhumimu wa kuokoka katika maisha yao.
unao wajibu wa kuvumilia maana wakati mwingine unaweza ukapitia maeneo au mazingira yanayohitaji uvumilivu. Kijana mcha MUNGU lazima ahakikishe anawaonya kwa upole wao washindanao naye, ili kama ikiwezekana, MUNGU awape kutubu na kuijua kweli; wapate tena fahamu zao, na kutoka katika mtego wa Ibilisi, ambao hao wametegwa naye MUNGU, hata kuyafanya mapenzi yake. ''.
Na siku zote ili uweze kuvumilia ni lazima uwe na upendo maana upendo unaweza ukazaa uvumilivu,
-mfano kijana anayempenda MUNGU ni rahisi kwake kuvumilia matukano kutoka kwa wapingakristo.
-Kijana aliye na upendo kwa ndugu zake ni rahisi sana kuvumilia dhihaka zao huku haachi kuwashuhudia habari njema za ufalme wa MUNGU.
1 Kor 13:4 ''Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni; ''
-Ndugu,Naamini umejifunza na utachukua hatua njema ya kumpokea BWANA YESU kama hujaokoka ili awe BWANA na MWOKOZI wako tangu leo na utaanza kuishi maisha matakatifu
KAMA UNATAKA KUTUBU RUDIA MANENO HAYA KISHA TAFUTA KANISA LA KIROHO UKAJIUNGE NA KUANZA KUISHI MAISHA MATAKATIFU.
''BABA katika jina la YESU KRISTO Niko mbele zako mimi mwenye dhambi, lakini leo nimetambua kosa langu na naomba unisamehe dhambi zangu zote, nisamehe dhambi ninazozikumbuka na pia zile ambazo sizikumbuki. futa jina langu katika kitabu cha hukumu na uliandike jina langu katika kitabu cha uzima. Neno lako katika Warumi sura ya 10 Mstari wa 9 na wa 10 Neno lako linasema ''Kwa sababu, ukimkiri YESU kwa kinywa chako ya kuwa ni BWANA, na kuamini moyoni mwako ya kuwa MUNGU alimfufua katika wafu, utaokoka. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu '' . BWANA YESU mimi nimekuamini leo na hivyo naamini sasa napokea wokovu wako na hakika nimeokoka. Kuanzia leo Naufunga ukurasa wa dhambi na ninaufungua ukurasa wa matendo mema na matakatifu. BWANA nipe ROHO wako Mtakatifu ili aniwezeshe kushinda dhambi na anasa zote za dunia. Kuanzia leo mimi nimeokoka na ni mtoto wa MUNGU mwenye haki zote. ninafuta laana zote na kila roho ya shetani inayonifuatilia naiharibu kwa jina la YESU KRISTO kama neno la MUNGU linavyosema katika Yeremia sura ya kwanza mstari wa 10. BWANA YESU nakushukuru sana kwa kuniokoa. Yote haya kwa imani nimepokea na niko tayari sasa kwa ROHO MTAKATIFU kunitumia. Katika jina la YESU KRISTO nimeomba na kupokea . Amen.'' Kama umetubu toba ya kweli hakika wewe kuanzia sasa ni mshindi na ni shujaa. Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine. ulishindwa kumpokea BWANA YESU nafasi yako bado ipo na muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula
+255714252292 mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili
JITIE MOYO MWENYEWE KAMA HAKUNA WA KUKUTIA MOYO.
Na Mtumishi Peter Mabula. |
BWANA YESU asifiwe.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU.
Majaribu yapo na yatupasa tuyashinde.
Magumu wakati mwingine huja lakini kuwategemea wanadamu huleta mtego.
Wakati mwingine kama hakuna mtu wa kukutia moyo katika magumu unayopitia hakikisha unajitia moyo mwenyewe.
Kuna watu hata hulalamika kwanini humtii moyo katika jaribu lake.
Ni vizuri kutiwa moyo na wapendwa wako lakini wakati ukiona hakuna wa kukutia moyo hakikisha unajitia moyo mwenyewe maadamu unaishi maisha matakatifu na mngoje BWANA.
Ngoja nikupe mfano mmoja wa mtu aliyekuwa katika magumu ndani ya Biblia.
Ayubu alikuwa na marafiki, na alitarajia marafiki zake wakija basi watamtia moyo lakini ilikuwa tofauti. Kuna wakati Ayubu katika magumu yake alitarajia mkewe ndie angemtia moyo na kumfariji lakini hata mke naye aligeuka na kumwambia amkufuru tu MUNGU ili afe. jiulize hapo ''Yaana anayetakiwa kukutia moyo ndio huyo sasa anataka ufe?''
Ndugu, inawezekana kabisa unapitia magumu na unatarajia sana wapendwa wako wakutie moyo, kama ukiona kimya nakuomba jitie moyo mwenyewe maadamu tu uko katika kweli ya MUNGU.
Ayubu ni mfano mzuri na ninampenda sana maana jaribu lake linatufundisha kitu muhimu sana.
Ayubu alijitia moyo mwenyewe na kusema anauhakika MUNGU atamshindia tu.
Ayubu 19:25-27 ''Lakini mimi najua ya kuwa Mteteaji wangu yu hai, Na ya kuwa hatimaye atasimama juu ya nchi.Na baada ya ngozi yangu kuharibiwa hivi, Lakini, pasipokuwa na mwili wangu nitamwona MUNGU; Nami nitamwona mimi nafsi yangu, Na macho yangu yatamtazama, wala si mwingine. Mtima wangu unazimia ndani yangu. ''
Ayubu alibaki na BWANA maana alijua wanadamu hawako upande wake.
Kazi ya wanadamu na marafiki kwenye jaribu la Ayubu ilikuwa ni kumsimanga, kumcheka, kumlaumu na kumtuhumu kwamba amefanya dhambi.
Ayubu 19:2-5 '' Je! Mtanichukiza nafsi yangu hata lini, Na kunivunja-vunja kwa maneno? Mara kumi hizi mmenishutumu; Hamwoni haya kunifanyia mambo magumu. Ingawaje nimekosa, Kosa langu hukaa kwangu mwenyewe.Kwamba mtajitukuza juu yangu, Na kunena juu yangu shutumu langu;''
-Huu ni mfano wa watu wanaopitia katika magumu.
Kuna familia kila mwaka wanazika lakini ukiwauliza majirani watasema kwamba hiyo ni laana inawatafuna kumbe ni uongo.
Kuna binti kila akitaka kuchumbiwa anaachwa, ukiwauliza wapendwa wake utasikia mara hiki mara kile. mara nyingi ni uongo.
Yohana 16"33 '' Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu. ''
Ndugu unayepitia magumu, nakuomba omba sana na vumilia.
Kesho yako haitakuwa kama leo yako kama tu hiyo kesho ukiikabidhi kwa BWANA YESU.
Dunia inakwenda kasi sana, kuna waliokuwa na kazi nzuri muda mfupi tu uliopita lakini sasa hawana. Ni vyema kukabidhi kwa YESU kazi yako, kipato chako na familia yako lakini pia yakija magumu nakuomba jifunze kuomba na kumshirikisha BWANA YESU ili akushindie.
Mthayo 5:8 ''Heri wenye moyo safi; Maana hao watamwona MUNGU''
Kama kuna leo basi na kesho ipo.
Kama leo imejaa miba inayochoma kwako, kesho yako inaweza kuwa na shangwe ya kudumu kama tu BWANA YESU utamshirikisha katika maombi yako.
Wakati wa dhoruba vumilia na omba sana.
BWANA YESU bado ana ushindi wako na ukivumilia ushindi huo utakuwa dhahiri kwako.
ona mfano huu.
Mathayo 9:2 '' Na tazama, wakamletea mtu mwenye kupooza, amelala kitandani; naye YESU, alipoiona imani yao, alimwambia yule mwenye kupooza, Jipe moyo mkuu, mwanangu, umesamehewa dhambi zako.''
Jipe moyo mwenyewe kama hakuna wa kukutia moyo.
Dumisha utakatifu na hakikisha jaribu lako halikuondoi katika wokovu wa BWANA YESU.
Una heri wewe uliyeokoka na unamtegemea MUNGU.
Ubarikiwe sana na hakikisha Vazi lako la Wokovu wa KRISTO halichafuliwi na chochote.
-Shika Wokovu Asije Mtu Akakunyang'anya.
-Hata Kama Utadharaulika Lakini Mtii BWANA
YESU Na Usimwache Hata Kidogo.
Kumb 6:5 '' Nawe mpende BWANA, MUNGU
wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako
yote, na kwa nguvu zako zote. ''
Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi
tutajifunza tena siku nyingine.na kama
hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea
ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika
jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza
kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani.
MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki
upotelee motoni anataka uende uzimani aliko
KRISTO BWANA. MUNGU akubariki sana
. Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula
+255714252292
mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.
MUNGU Akubariki.
WEWE UKO WAPI?
BWANA YESU asifiwe ndugu yangu.
Ni mara nyingi sana huwa namshukuru MUNGU
ninapoona maelfu ya watu wamehudhuria mbele
ya MUNGU kujifunza neno la MUNGU, Kupokea
uzima wa BWANA YESU , Kumpa maisha yao
BWANA YESU.
Watumishi wa MUNGU hujitoa sana ili tu injili
imfikie kila mtu. Kuna Mchungaji mmoja rafiki
yangu alifunga siku 11 bila kula wa kunywa
chochote ili MUNGU aguse wanadamu ambao
watakuja katika mkutano wa siku 3 wa neno la
MUNGU ambapo mchungaji huyo alikuwa ni
mfundishani. Watu waliokoka na wengi
walifunguliwa, hakika injili inasonga mbele.
Watumishi wa MUNGU wengi hujitoa miili yao
dhabihu kama neno linavyoaagiza ili tu wewe
uokoke.
Warumi 12:1-2 ( Basi, ndugu zangu, nawasihi,
kwa huruma zake MUNGU, itoeni miili yenu iwe
dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza
MUNGU, ndiyo ibada yenu yenye maana. Wala
msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe
kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua
hakika mapenzi ya MUNGU
Wengine hawakulala usingizi ili wewe na mimi
tuupate uzima wa kweli ulio katika KRISTO
YESU.
Yawezekana ulihudhuria mara moja tu mkutano
wa injili kwa lengo la kuponywa ugonjwa wako,
na MUNGU siku hiyo hakukuponya kwa sababu
alikujua unataka kupona tu harafu uondoke na
kwenda kuwasimanga wahubiri.
Yawezekana ulihudhuria mikutano ya injili lakini
umerudi nyuma je kwa sasa huihitaji tena
mbingu?
Yawezekana ulienda kushangaa watu tu.
Ndugu yangu penda mahubiri na penda uzima wa
milele, na kama utapenda uzima wa milele
utakuwa unampenda YESU KRISTO maana uzima
wa milele hauko kwingine nje na yeye. Na siku
zote BWANA anawatuma wahubiri hao
unaowaona ili wewe umruhusu yeye YESU
kutawala maisha yako.
Ni wakati wa kumpa YESU maisha yako maana
kesho huijui itakuwaje.
Kuna watumishi wa MUNGU wameonekana kama
vichaa mbele ya watu ambao ufahamu wao
umetekwa na shetani lakini hawakukata tamaa,
lengo na nia ya mioyo yao ni watu wampokee
BWANA YESU kama BWANA na MWOKOZI wa
maisha yao kama neno la MUNGU linavyosema
''Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa
kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale
waliaminio jina lake; waliozaliwa, si kwa damu,
wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa
mapenzi ya mtu, bali kwa MUNGU-Yohana
1:12-13''.
Ndugu yangu yawezekana hujawahi kuona
umuhimu wa kuhudhuria mikutano ya injili,
yawezekana ukiwaona wahubiri unawaona tu
kama watu waliokosa kazi, yawezekana mahubiri
yao unayaona kama kelele tu lakini napenda
kukutaarifu kuwa mahubiri yote ambao
utayasikia iwe ni redioni, sokoni au popote ni
MUNGU anakuhitaji wewe ili tu usiende motoni.
Maelfu ya watu wanaokoka lakini yawezekana
wewe haumo kwenye orodha hiyo, unadhani ni
kwanini haumo?
Wengi wanakimbilia uzima wewe uko wapi?
Wengi wanamhitaji YESU usiku na mchana je
wewe uko wapi?
Wengi wanaokoka, je wewe uko wapi?
Wengi wanatamani mahubiri kila siku, wewe je?
Wengi majina yao yanaandikwa kwenye kitabu
cha uzima, wewe je?
Nakushauri kumpokea BWANA YESU leo na
utaona mabadiliko makuu sana.
yawezekana
wewe hauko katika orodha hiyo ya wateule wa
MUNGU kwa sababu tu hukuhudhuria mahubiri. Naomba ujue kwamba muujiza mkubwa kuliko yote ni kumpokea
BWANA YESU kama BWANA na MWOKOZI wa
maisha yako. wewe yawezekana huhitaji kuhudhuria
katika ibaada, unadhani ni kawnini? je
huhitaji mbingu? kundi kubwa LA watu
wanamhitaji YESU lakini wewe haumo, je uko
wapi?
watu
wengi tu wanaokoka lakini yawezekana wewe
haumo katika wale wanaompokea BWANA YESU,
unadhani ni kwanini?. watu wengi
wanafunguliwa na kuokoka lakini yawezekana
wewe haumo kwenye kundi la wanaompokea
YESU, unadhani ni kwanini/ je uko wapi? je
huitaki mbingu leo?
Maelfu ya watu wanaokoka, je
wewe uko wapi? . kundi kubwa LA watub
wanamhitaji BWANA YESU je wewe uko wapi/ je
leo huitaki mbingu?
watu wanatoka mbele ili kumpokea BWANA
YESU kama BWANA na MWOKOZI wa maisha
yao. Yawezekana wewe haupo kwa sababu
hukuhudhuria, je utampokea YESU lini? au je leo
hutaki mbingu?. umealikwa mara ngapi
kuhudhuria ibada, semina au mikutano ya injili
lakini hukuona umuhimu wa MUNGU anayetaka
kukuponya na kukuokoa?
maelfu ya watu
wanampokea YESU lakini yawezekana wewe
haumo kwa sababu ulikataa kuhudhuria.
BWANA YESU amenituma kwa ndugu zangu wote na marafiki.
Mwenye sikio LA kusikia na asikie Leo na kuchukua hatua.
Jehanamu inawangoja watenda dhambi lakini ashukuriwe MUNGU maana mbingu inawasubiri watakatifu wa MUNGU.
Kwa leo naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi
tutajifunza tena siku nyingine.na kama
hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea
ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika
jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza
kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani.
ROHO aliyenipa ujumbe huu ana
makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee
motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO
BWANA.
MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako
Peter M Mabula
0714252292
MUNGU akubariki sana uliyesoma
somo hili.
UNAO MUDA MCHACHE, UTUMIE VYEMA.
BWANA YESU atukuzwe ndugu.
Nakuomba usome ujumbe huu hadi mwisho.
Karibu uijue na kuitambua kweli inayoweka huru watu walio tayari kuwekwa huru.
Usiichezee wala kuijaribu Neema ya MUNGU ndugu yangu.
Usione kwamba muda unao sana hata huoni umuhimu wa kuokoka leo.
Usipoteze muda wako katika mambo ambayo hayakujengi kiroho.
Kumbuka kwamba siku ya mwisho hata kazi yako haitakuwa na maana sana hata kama ilikupotezea muda mrefu.
''Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka.-Mathayo 11:12''
-Wanaoupata ufalme wa MUNGU ni wale ambao wamewekeza rohoni na sio mwilini.
-Walioupata ufalme wa MUNGU ni wale waliompokea BWANA YESU na kuishi maisha matakatifu siku zote.
Inawezekana kabisa ka dhambi kadogo tu kamekushinda kukaacha na hujui hata kwanini huachi. Kumbe tatizo ni muda wako unautumia vibaya.
Huna hata dakika 50 kwa siku kwa ajili ya MUNGU lakini muda wa kuangalia filamu au tamthilia unao. muda wa kuangalia mpira au kusikiliza miziki ya kidunia unao.
Muda wa kufanya jambo lolote unao isipokuwa muda wa kwenda kanisani tu ndio huna.
Muda wa kila jambo ulitakalo unao lakini muda kwa ajili ya mambo ya MUNGU tu ndio huna.
Ndugu.
''Kwa maana hiyo siku ya BWANA i karibu juu ya mataifa yote; kama ulivyotenda, ndivyo utakavyotendwa; malipo yako yatakurudia juu ya kichwa chako mwenyewe.-Obadia 1:15''
-Neno la MUNGU lipo na halibadiliki.
Neno linasema siku ya BWANA i karibu, kila mtu atalipwa sawa na matendo yake yalivyo.
Kuna wakati natamani nimfuate kila mtu na kumwambia aokoke na kuanza kuishi maisha matakatifu.
Kuna wakati natamani MUNGU ampe kila ndugu na rafiki yangu moyo wa toba.
Watu wengi leo hawataki neno la MUNGU la uzima.
Kuna wengine husikiliza neno la MUNGU la kweli kama hili lakini halifuati wala kulitii.
Kuna wengine hutii neno la MUNGU kwa sabab tu ya magumu wanayopitia lakini akipata hitaji lake anamsahau MUNGU.
Ni hatari sana.
Ndugu yangu, uzima wa milele n wako binafsi na sio wa jumuiya.
Kama mwenzi wako wa ndoa ndie chanzo cha wewe kumwacha YESU nakupa pole maana bado hujatambua kwamba uzima wa milele hamtashare bali kila mtu sawasawa na matendo yake.
Kila siku MUNGU BABA ananipa ujumbe ili tu ndugu yangu usikose uzima. MUNGU kila siku anawapa watumishi wake mbalimbali neno lake ili tu Mwanadamu usiende jehanamu lakini binadamu waliowengi wanaona kawaida kawaida tu.
Ndugu yangu, nakuomba uone kila kitu cha kawaida kawaida lakini sio Neno la MUNGU.
Anapofariki mtu tunalia na kuomboleza lakini ukweli ni kwamba zamu yake yeye amemaliza na ameenda ama mbinguni ama kuzimu kutegemea na matendo yake. lakini kifo chake ni taarifa kwetu kwamba ipo siku tena inakuja siku hiyo ambapo hata sisi tutaondoka duniani.
Shetani alivyofunga watu unaweza ukaona mtu analia msibani lakini akiondoka hapo anaenda kufanya uzinzi na uasherati.
Mtu analia msibani lakini jioni ya siku hiyo hiyo anaenda dhambi kama kawaida.
Ndugu zangu ni wakati wa neema lakini neema hiyo ina mwisho.
Mwenye sikio la kusikia na asikie leo.
Siku moja katika maono nilimuona BWANA YESU amesimama kwa mbali kidogo na pale nilipokuwa mimi na watu wengine wengi. akaniita nikaenda, nilipoenda alipo akanionyesha kitabu cha uzima, nikaliona jina langu humo na majina machache ya watu ninaowafahamu.
Baada ya kuliona jina langu BWANA akanituma niende nikawaambie wanadamu kwamba wampokee yeye na kuanza kuishi maisha matakatifu.
Lilikuwa jambo la ajabu sana lakini kwenye maono nilijiona nikienda na kuwaeleza wanadamu, kuna ambao nilikuwa mpaka nawaambia na kuwalazimisha waokoke, niliifanya kazi hiyo kwa muda mrefu. kuna waliookoka na wengine hawakuokoka, baadae BWANA YESU akasema inatosha akaniiita niende alipokuwa amesimama yeye, nikaenda.
Ndugu nakushauri kumpokea YESU na kuanza kuishi maisha matakatifu kuanzia leo.
Hatuna injili nyingine zaidi ya Wokovu wa BWANA wetu YESU KRISTO aliye pekee na uzima wetu wa milele.
Wakolosai 3:5-10 '' Basi, vifisheni viungo vyenu vilivyo katika nchi, uasherati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo ibada ya sanamu;kwa ajili ya mambo hayo huja ghadhabu ya MUNGU.Katika hayo ninyi nanyi mlitembea zamani, mlipoishi katika hayo.Lakini sasa yawekeni mbali nanyi haya yote, hasira, na ghadhabu, na uovu, na matukano, na matusi vinywani mwenu. Msiambiane uongo, kwa kuwa mmevua kabisa utu wa kale, pamoja na matendo yake; mkivaa utu mpya, unaofanywa upya upate ufahamu sawasawa na mfano wake yeye aliyeuumba. ''
Ndugu yangu, tunapohubiri injili ya KRISTO inayookoka hatuhubiri jambo ambalo ni labda tu kuwepo, bali tunahubiri jambo ambalo ni ndio katika ndio tena ni kweli katika kweli zote.
Kama kweli wewe binafsi unautaka uzima wa milele nakushauri kimbilia kanisa la kiroho na ukaokoke kisha kuanzia leo anza kuishi maisha matakatifu.
Wokovu ni wako binafsi na sio wa ukoo wala familia yako.
Ukisema kwamba unafuata mila au taratibu za ukoo wako haitakusaidia.
Kama unasubiri hadi baba na mama yako waokoke ndio na wewe utampokea YESU hiyo haitakusaidia.
Neema ipo leo na neema hiyo nakuomba sana uitumie vizuri.
Heri kuokoka kuliko kujifurahisha kwenye dhambi kisha ukifa unaenda kulia milele jehanamu.
BWANA YESU anaokoka na ukimpokea leo hakika unaokoka.
Saa yako moja inaweza kuamua ni wapi utaenda baada ya kufa.
Muda wako wa leo ni muhimu sana kuliko muda wa kesho.
Itumie leo vizuri ndipo utakapoiona kesho yako ikiwa vizuri zaidi.
BWANA YESU amenituma kwa ndugu zangu wote na marafiki.
Mwenye sikio LA kusikia na asikie Leo na kuchukua hatua.
Jehanamu inawangoja watenda dhambi lakini ashukuriwe MUNGU maana mbingu inawasubiri watakatifu wa MUNGU.
Kwa leo naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi
tutajifunza tena siku nyingine.na kama
hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea
ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika
jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza
kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani.
ROHO aliyenipa ujumbe huu ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee
motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO
BWANA.
MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako
Peter M Mabula
0714252292
MUNGU akubariki sana uliyesoma
JE INAWEZEKANA UWE MKRISTO BILA KWENDA KANISANI?
Ndugu nakukaribisha katika somo hili muhimu
kwa maisha ya waenda mbinguni.Na kumbuka
kuwa HUWEZI KUWA MKRISTO KAMA HUNA
KRISTO MOYONI MWAKO. Hivyo hakikisha
kwanza unakuwa na KRISTO maishani mwako
ndipo utakuwa MKRISTO sahihi na sio mkristo
jina.
Je mtu anaweza kuwa baharia bila kwenda
baharini?
Mkristo maana yake ni mfuasi wa
YESU KRISTO. Tunasoma katika Biblia kuwa
YESU alikuwa na desturi ya kwenda hekaluni na
angali anapatikana mahali pa ibada hata leo.
Wakristo ni watu wanaompenda MUNGU, na kwa
hivyo wanawapenda watu wa MUNGU na nyumba
ya MUNGU. Biblia haiwapendekezi Wakristo
pekee, Hata ile hali ya kuwa Mkristo
asiyekwenda kanisani haimfai mtu yeyote. Ni
kama mtu anayeishi kwa kula tu mkate na maji
hali anaweza kupata chakula kizuri kwa afya
yake. Kama alivyosema mwana mpotevu.
''Nyumbani mwa Baba yangu kuna chakula kingi,
wanakula mpaka wanakiacha''(Luka 15:17).
Katika kanisa utapokea mkate wa uzima ambao
ni neno la MUNGU. Kumbuka ya kuwa vitabu
fulani katika Biblia viliandikwa kama barua kwa
makanisa na faida yake kamili inaweza tu
kupatikana unaposhirikiana na wengine..
Ni
afadhali kupata kilicho bora zaidi.
Kumbuka
mwanajeshi hufanya kazi kwenye jeshi .
kaa
la moto likitengwa na mengine litazima.
Hakuna ndoa ya mtu mmoja tu peke yake, Ndoa
ni uhusiano na upendo. Ndoa inakuhusisha na
jamaa wa pande zote mbili.
Hakuna mtu
anayeweza kuwa mkristo wa peke yake tu.
mtu
hawezi kuzaliwa tu peke yake bila ya kuwa na
wazazi na jamaa wa karibu..
Unapozaliwa mara
ya pili yaani unapobatizwa ubatizo wa maji
mengi na pia unapobatizwa ubatizo wa ROHO
MTAKATIFU unafanyika sehemu ya jamii ya
waaminio, Biblia katika Marko 16:16 inasema
''Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini
atahukumiwa'' hivyo kubatizwa pia ni muhimu ili
kuitimiza haki yote ya MUNGU. Jambo hili la
kuamini na kubatizwa lina manufaa makubwa
kwako, huu ni urithi wako na kama mtume Paulo
anavyosema , MKRISTO NI WA AINA MOJA TU-
MSHRIKA WA MWILI WA KRISTO.
Sisi ni washirika wa mwili wake katika
ulimwengu huu. Kanisa liko duniani kwa sababu
sisi sio roho tu bali pia ni watu wenye mwili na
damu. BWANA aliliunda Kanisa hapa duniani
kwa manufaa yetu na ametukirimia vipawa
kutoka mbinguni ili tuweze kupata nguvu kutoka
kwa wenzetu na kufurahia ushirika wa KIKRISTO
na upendo. Maandiko yamejaa habari za ushirika
na kutushauri kwamba tusiache kutumia nafasi
nzuri za ushirikiano na kushauriana na kwamba
tusiache kukusanyikana pamoja kumwabudu
MUNGU wetu.
JINSI YA KUWA KRISTO MWENYE AFYA .
1: Kula chakula kizuri yaani NENO LA MUNGU.
2: Kunywa maji mengi yaani ROHO MTAKATIFU.
3: Fanya mazoezi yaani MTUMIKIE MUNGU NA
KUTENDA KAZI KWA AJILI YAKE.
4: Pata hewa safi yaani HUSIKA KATIKA IBADA
NA SIFA.
J5: iburudishe yaani KWENYE USHIRIKIANO NA
WAKRISTO WENGINE.
MUNGU awabariki sana na kama hujamba
BWANA YESU maisha yako wakati wa kufanya
hivyo ni sasa maana hakuna uzima wa milele
bila YESU KRISTO (Yohana 14:6) hivyo kwa
sababu ndugu unataka uzima wa milele mpe
YESU maisha yako na utakuwa huru mbali na
uonevu wa shetani.
MUNGU akubariki tena
Ni mimi ndugu yako Peter Michael Mabula.
KWANINI SASA NI NYAKATI ZA MWISHO?
Na Peter M Mabula |
BWANA YESU asifiwe ndugu zangu.
Karibu tujifunze.
Ndugu Zangu Huu Ni Wakati Wa Mwisho.
Wakati Kibiblia Unaweza Kumaanisha Miaka
Kadhaa Ambayo MUNGU Ndie Ajuaye. Nyakati
Moja Inaweza Hata Kuwa Na Zaidi Ya Miaka
1000.
2 Timotheo 3:1-7, Lakini ufahamu neno hili, ya
kuwa siku za mwisho kutakuwako nyakati za
hatari. Maana watu watakuwa wenye kujipenda
wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu,
wenye kiburi, wenye kutukana, wasiotii wazazi
wao, wasio na shukrani, wasio safi,
wasiowapenda wa kwao, wasiotaka kufanya
suluhu, wasingiziaji, wasiojizuia, wakali,
wasiopenda mema, wasaliti, wakaidi, wenye
kujivuna, wapendao anasa kuliko kumpenda
MUNGU; wenye mfano wa utauwa, lakini
wakikana nguvu zake; hao nao ujiepushe nao.
Kwa maana katika hao wamo wale wajiingizao
katika nyumba za watu, na kuchukua mateka
wanawake wajinga wenye mizigo ya dhambi,
waliochukuliwa na tamaa za namna nyingi;
wakijifunza siku zote, ila wasiweze kabisa
kuufikia ujuzi wa kweli.
Siku moja kama miezi miwili iliyopita nilikuwa
kwenye gari la abiria maarufu kama costa
nikitoka Kawe kwenda Ubungo, njiani kabla ya
kufika Mwenge kuna dada mmoja alipanda gari
na kukaa siti jirani na mimi, Dada yule alikuwa
anasoma Gazeti ambalo nilipoliangalia nililiona
kama jipya kwangu lakini la kidini, gazeti lile
lilikuwa na vichwa vya habari vizuri sana na
hakika ni gazeti linalovutia, nilitamani kulinunua
gazeti hilo jipya la kikristo ambalo hakika halina
udaku bali mambo mengi ya Biblia, nilimuomba
dada yule aniambie linauzwa wapi.
Nilipomwambia tu hivyo akanipa na kusema
nichukue tu maana yeye anayo mawili ya toleo
moja, muda kidogo yule dada akashuka kabla
hata ya Mlimani city, Nilimshukuru kwa tendo
lake jema la kunipa gazeti. Sikusoma kwa muda
huo bali nilikusudia kusoma nikifika ubungo, ni
kweli baadae nilianza kusoma na ndipo
nilipojisemea kwamba ''Mwisho wa dunia
umefika''. Gazeti hilo lilikuwa na kichwa cha
habari kimojawapo kiitwacho ''KRISTO
ANATAWALA NA KANISA'', Nilipenda kichwa cha
habari hicho lakini nilipofungua ndani kuhusu
ujumbe wa kichwa hicho cha habari nilikutana na
kasheshe ambalo sijawahi kulisikia kabla. Yule
Kristo anayetajwa sio BWANA YESU
tunayemfahamu mimi na wewe bali ni
mwanadamu mmoja ambaye kwa sasa ni
marehemu na alikuwa kiongozi wa dhehebu moja
la kikristo. huyo ndio anaitwa Kristo na licha ya
kufariki bado waumini wake wanajua kwamba
bado anatawala. Ufafanuzi wa taarifa hiyo ya
kishetani gazetini ni kwamba BWANA YESU ni
KRISTO wa kwanza lakini kizazi Hiki cha sasa
eti MUNGU ameletwa kristo wa pili ambaye ni
mwafrika wa Tanzania. Niliumia sana na kuwaza
mengi sana na binafsi hadi leo naamini kwamba
viongozi wa dhehebu hilo ni mawakala wa
shetani na wapo kwa ajili ya kuhakikisha
waumini wao hawaendi mbinguni. Waumini wa
dhehebu hilo mimi siamini kama huwa
wanasoma Biblia bali huwa wanasomewa tu.
Nilichojifunza ni kwamba dhehebu hilo halina
mpango wa waumini wake kwenda mbinguni. hili
dhehebu ni hatari kama wachawi walivyo hatari,
Hakika ni siku za mwisho.
Tunajua Kwamba Hizi Ni Siku Za Mwisho Kwa
Sababu Ya Dalili Zilizoko Kwenye Biblia. Kama
Wewe Unavyoweza Kujua Dalili Za Mvua Baada
Ya Kuona Mawingu Ndivyo Hivyo Mwisho
Umekaribia baada ya kila dalili kuonekana.
( 1 Yohana 2:18-23, Watoto, ni wakati wa
mwisho; na kama vile mlivyosikia kwamba
mpinga Kristo yuaja, hata sasa wapinga Kristo
wengi wamekwisha kuwapo. Kwa sababu hiyo
twajua ya kuwa ni wakati wa mwisho. Walitoka
kwetu, lakini hawakuwa wa kwetu. Maana kama
wangalikuwa wa kwetu, wangalikaa pamoja nasi.
Lakini walitoka ili wafunuliwe kwamba si wote
walio wa kwetu. Nanyi mmepakwa mafuta na
Yeye aliye Mtakatifu nanyi mnajua nyote.
Sikuwaandikia ninyi kwa sababu hamwijui iliyo
kweli, bali kwa sababu mwaijua, tena kwamba
hapana uongo wo wote utokao katika hiyo kweli.
Ni nani aliye mwongo ila yeye akanaye ya kuwa
YESU ni KRISTO? Huyo ndiye mpinga Kristo,
yeye amkanaye BABA na MWANA. Kila
amkanaye MWANA, hanaye BABA; amkiriye
MWANA anaye BABA pia. ).
Dalili za siku za mwisho ni nyingi, baadhi ni
hizi:
1. Wapingakristo watatokea:hawa ni dini au
watu binafsi ambao wanakataa ukombozi kupitia
YESU KRISTO.
2. Watu kuliacha fundisho la KRISTO.
-Waongo ni wale wanaomkataa YESU na jambo
la kukumbuka ni kwamba anayemkataa YESU
huyo anamkataa MUNGU, Hakuna mtu aliye
upande wa MUNGU kama amemkataa KRISTO
katika maisha yake.
Hakika Ni Siku Za Mwisho.
3. Makristo Wa Uongo Wameshakuja( Mathayo
24:5,Kwa sababu wengi watakuja kwa jina langu,
wakisema, Mimi ni Kristo; nao watadanganya
wengi. ).
-Wengi hata sasa wameshakuja waongo na
kuleta dini zao na wao kusimama kama nembo
(icon) ya dini hizo, hawa hujifanya wakombozi
wa watu na kwa hali hiyo hujifanya KRISTO.
-Wengi wanahubiri kama wanamhubiri KRISTO
lakini ndani yao wana ajenda za kuzimu za
kuwapotosha watu, hawawezi kukemea dhambi
wala kufundisha toba.
4. Manabii Wa Uongo Wapo Na Hawakawii
Kukwambia Kwamba YESU Atarudi Akiwa Shehe
( Mathayo 24:24-27, Kwa maana watatokea
makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao
watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate
kuwapoteza, kama yamkini, hata walio wateule.
Tazama, nimekwisha kuwaonya mbele. Basi
wakiwaambia, Yuko jangwani, msitoke; yumo
nyumbani, msisadiki. Kwa maana kama vile
umeme utokavyo mashariki ukaonekana hata
magharibi, hivyo ndivyo kutakavyokuwa kuja
kwake Mwana wa Adamu. )
-Ndugu zangu, kuna watu hukimbilia miujiza,
ndugu zangu sio kila wafanya miujiza ni
watumishi wa MUNGU aliye hai, hata shetani
naye ana watumishi wake ambao anawatumia.
-Mtu akileta fundisho tofauti na fundisho la
KRISTO huyo ni nabii wa uongo.
-Wanaotangaza tarehe za kuja kwa YESU hao
ndio hata hawajui walifanyalo.
Ndugu zangu mwisho umekaribia ila hakuna
ajuaye siku wala saa, sisi tulichopewa kujua ni
dalili tu na hakika dalili huonyesha kwamba
mwisho umekaribia..
1 Petro 4:7 '' Lakini mwisho wa mambo yote
umekaribia; basi, iweni na akili, mkeshe katika
sala. ''
5. Nyakati Za Mwisho Watu Watapenda Pesa
Kuliko MUNGU Tena Wasaliti ( 2 Timotheo 3:1-7)
6. Nyakati Za Mwisho Watu Watasikiliza
Mafundisho Ya Mashetani
7. Watajitenga Na Imani
8. Na Watazuia Watu Kuoa
9. Na Watakataza Watu Kula Baadhi Ya Vyakula
1 Timotheo 4:1-4 ''Basi ROHO anena waziwazi
ya kwamba nyakati za mwisho wengine
watajitenga na imani, wakisikiliza roho
zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani; kwa
unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa
moto dhamiri zao wenyewe; wakiwazuia watu
wasioe, na kuwaamuru wajiepushe na vyakula,
ambavyo MUNGU aliviumba vipokewe kwa
shukrani na walio na imani wenye kuijua hiyo
kweli. Kwa maana kila kiumbe cha MUNGU ni
kizuri, wala hakuna cha kukataliwa, kama
kikipokewa kwa shukrani; ''.
10. Siku Za Mwisho Watu Watajaa Dhihaka 2
Petro 3:3-4 '' Mkijua kwanza neno hili ya
kwamba katika siku za mwisho watakuja na
dhihaka zao watu wenye kudhihaki, wafuatao
tamaa zao wenyewe, na kusema, Iko wapi ahadi
ile ya kuja kwake(YESU)? Kwa maana, tangu
hapo babu zetu walipolala, vitu vyote vinakaa
hali iyo hiyo, tangu mwanzo wa kuumbwa. ''
11. Watu wengi watakua Hawana ROHO
MTAKATIFU( Yuda 1:18-21, ya kwamba
waliwaambia ya kuwa, Wakati wa mwisho
watakuwako watu wenye kudhihaki, wakizifuata
tamaa zao wenyewe za upotevu. Watu hao ndio
waletao matengano, watu wa dunia hii tu, wasio
na ROHO. Bali ninyi, wapenzi, mkijijenga juu ya
imani yenu iliyo takatifu sana, na kuomba katika
ROHO MTAKATIFU, jilindeni katika upendo wa
MUNGU, huku mkingojea rehema ya BWANA
wetu YESU KRISTO, hata mpate uzima wa
milele. ).
Ndugu Zangu Wanamume Kwa Wanawake YESU
KRISTO Anatuita Kwenye Ufalme Wake. Amua
Vyema Leo Kwa KUOKOKA.
Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi
tutajifunza tena siku nyingine.na kama
hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea
ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika
jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza
kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani.
MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki
upotelee motoni anataka uende uzimani aliko
KRISTO BWANA.
MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako
Peter M Mabula
0714252292
mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.